Watanzania tusiwe wajinga tuliopitiliza

Mwana Mtoka Pabaya

JF-Expert Member
Apr 22, 2012
15,118
16,470
Katika hali ya kushangaza, nimepanda daladala na pale Morocco Hotel na humo ndani nimekuta mjadala ambao sijui umeanzia wapi lkn sikuamini masikio yangu kuwa wachangiaji wake ni watu wazima na si watoto (tena wa kike).

Kwa kifupi, kuna baadhi ya Watanzania wanaamini kuwa Muammar Gaddafi alikuwa akitoa $50,000 kwa kila kijana wa Libya anayefunga ndoa. Hii ikanikumbusha mjadala kama huo ambao ulikuwa mtaani kwetu kipindi kile huyu Dikteta ameuawa, lkn tofauti na leo, wachangiaji wake walikuwa vijana wa kijiweni ambao hata ukiwauliza mji mkuu wa Libya unaitwaje, hawajui.

Ya leo imenichefua kuona watu wazima, tena wanaume wanaongea ujinga ule. Mmoja wa wachangiaji ni Mwarabu (koko) ambaye alishuka kituo cha Yemen na kuacha mjadala ukiendelea. Kwa wingi wao na kwa kupeana zamu, walimsifu Gaddafi na kuwalaaani Walibya wakisema kuwa sasa wanajuta kwa kuwa Elimu bure, maji na umeme bure, pamoja na muamala wa $50,000 kwa kila ndoa inayofungwa haupatikani.

Nilichojiuliza mimi ni hiki: Je hivi mawazo haya tunayo kweli akilini mwetu au ule ni utani? Hivi kama Rais wa nchi anatoa $50,000 nikifunga ndoa, nani analima huko Libya? Ni nani anazalisha ikiwa pesa zinagawiwa mifukoni?

Kwa kweli nimesikia kichefuchefu, hivi tukipimwa akili zetu kwa mawazo yetu si tutaaibika?
 
Mkuu kwanza nikupe pole kwa maumivu hayo uliyopata.Ila binafsi naona kama umeyataka mwenyewe kuwa kutaka kulazimisha watu wote wawe na mawazo sawa na wewe,kitu ambacho hakiwezekani.

Kwanza nikubaliane na wewe kwamba hao watu hawana ushahidi wa hicho walichokuwa wakiongelea,lakini pia kwa upande mwingine hata wewe huna ushahidi wa kuwaprove wrong!Ushahidi unaoweza kutoa ni wa kimazingira kwamba haiwezekani kuwagawia watu pesa mifukoni,lakini na wao wanatumia ushahidi wa jinsi Gadaffi alivyobadili nchi ya jangwa kuwa mahali pazuri pa kuishi binadamu.

Kwa mtazamo wangu,mambo ya Libya tungewaachia walibya wenyewe wajue kama jamaa alikuwa dicteta au kiongozi wao anayestahili heshima.
 
Back
Top Bottom