Watanzania tusiwe wa kupinga kila kauli ya mkuu wa nchi

expedition

JF-Expert Member
Jul 16, 2016
923
2,962
Kwanza nianze kwa kuwapongeza kutoka na jinsi mnavyo i challenge serikali ya awamu ya tano, challenge hizi ndizo zinazomfanya mkuu asijisahau katika kuwatumikia watanzania.

Napenda sana mkuu akosolewe anapokosea lakini apongezwe anapokuwa sawa. Wengi wetu tumepinga vikali kauli ya mkuu ya kutokuwasomesha wazazi eti tu atakuwa kawanyima haki yao ya kupata elimu.

Hivi ni lini binti kapata ujauzito na akarudi shule kwa njia halali kuendelea na masomo katika hizi shule zetu za serikali?

Tusimlaumu mkuu kwa hili kwani anafanya tu muendelezo wa mfumo wetu wa elimu ulivyo. Ukimpa ujauzito mwanafunzi adhabu yake inajulikana na hivyo hivyo binti alopewa ujauzito huwa kajiondoa shule moja kwa moja.

kitendo cha kuruhusu tuwape ujauzito then warudi shule kutawafanya waone mimba ni kitu cha kawaida tu na wasiweke mkazo katika masomo.

ukweli shule za serikali wanafunzi wengi hawana muamko wa elimu na huwa wanasoma bora tu wahitimu. Tulopitia huko tunakufahamu vizuri.

Tumuungeni mkono kwa hili la mimba kwa wanafunzi maana hata katika familia nyingi vijjjini binti akipata mimba hufukuzwa nyumbani iweje shuleni!!
 
Anapingwa na kukosolewa Mungu na baadhi ya watu kwenye kila kitu itakuwa huyo magufuli
 
Si ndio walivofundishwa makamanda.
Mbowe kawaambia wapinge kila kitu
Naunga mkono Hoja ya Mkuu ; Hakuna kusomesha wake za watu...
lazima elimu iheshimiwe.
ndio maana baadhi ya nnchi ukikutwa unaibia majibu kwenye mtihani ni jela moja kwa moja.

Hizo ni miongoni mwa sheria za elimu na hakuna anaepinga ,kwa maslahi ya wanafunzi wenyewe
 
nikikukumbuka shule niliosoma mimi wangeruhusu huu mchezo szani kama kuna mtu angemaliza salama nazani shule ingekuw maternity ward
 
Wangeiondoa kwanza kwenye ilani yao ya 2015-2020 maana imebidi nii download kushuhudia kilichokuwa kimeahidiwa ndani ya ilani.
 
Back
Top Bottom