Watanzania tusitegemee maajabu kwenye baraza la Mawaziri, CCM ni ile ile na watu wake ni wale wale

ibesa mau

JF-Expert Member
Sep 17, 2015
2,109
1,692
Watu wanadhani baraza la Mawaziri atakalo liunda Magufuli litakuwa la ajabu sana kana kwamba litawahusisha malaika toka mbinguni. CCM ni ile ile na watu wake ni wale wale wala usitegemee kitu kipya sana sana sura za akina January Makamba, Nchemba, Migiro, Nyarandu n.k ndio tutegemee kuziona.

Wala usitegemee watu kama nchemba , januari kukosekana mbona patachimbika . wewe unafikiri baada ya kizazi cha akina kikwete ndani ya ccm kizazi kinachofuatia ni cha akina nani ndani ya CCM.

Acheni mawazo ya kudhani kwamba baraza la Mawaziri la Magufuri litajaa Malaika. Nyani ni wale wale na msitu ni ule ule.
 
Hata Magufuli alipoteuliwa kugombea Urais mlisema vivyo hivyo kuwa ataathiriwa na mfumo. Sasa anachanja mbuga umeshikwa na kwikwi na sasa mnaanza kuimba ngonjera nyingine
 
Watu wanadhani baraza la mawaziri atakalo liunda Magufuri litakuwa la ajabu sana kana kwamba litawahusisha malaika toka mbinguni. CCM ni ile ile na watu wake ni wale wale wala usitegemee kitu kipya sana sana sura za akina january makamba, nchemba, migiro, nyarandu n.k ndio tutegemee kuziona. wala usitegemee watu kama nchemba , januari kukosekana mbona patachimbika . wewe unafikiri baada ya kizazi cha akina kikwete ndani ya ccm kizazi kinachofuatia ni cha akina nani ndani ya ccm.

Acheni mawazo ya kudhani kwamba baraza la mawaziri la magufuri litajaa malaika tu

Hata JPM siyo Malaika, ndiyo maana sijamsifia kama wajinga wengi wanavyofanya
 
baada ya kizazi cha akina kikwete kinachofuatia ni kizazi cha akina makamba , mwigulu, nape. baada ya hao kinafuatia kizazi cha akina makonda , ritz, n.k
 
hata magufuli alipoteuliwa kugombea urais mlisema vivyo hivyo kuwa ataathiriwa na mfumo. Sasa anachanja mbuga umeshikwa na kwikwi na sasa mnaanza kuimba ngonjera nyingine

mbuga ipi aliyochanja?! Bidhaa zimeshuka bei?! Mbolea imeshuka bei?! Madawati yanatosha?! Dawa mahospitalini?! Nk?! Hata kikwete alianza na porojo za umaarufu kama huyu! Kwa taarifa yako watu tunaamini katika matokeo!
 
Hata Magufuli alipoteuliwa kugombea Urais mlisema vivyo hivyo kuwa ataathiriwa na mfumo. Sasa anachanja mbuga umeshikwa na kwikwi na sasa mnaanza kuimba ngonjera nyingine

kama hajaathiriwa mbona jana CC ya ccm wamekataa baadhi ya majina ya watu alio wateua uwaziri na kumtaka kuyaondoa baadhi ya majina kwa madai kwamba hawana mchango wa maana ndani ya ccm, huku wakimtaka kuingiza watu ambao CC inawaona wanamchango kwa ccm
 
kwani hivi ukawa wangekuwa na baraza gani la mawaziri kama sio walewale wanafiki na wazandiki wasikuzote.......
 
Hakuna mtanzania anatetegemea Magufuli ateue malaika. Tanzania ina binadamu tu, tutegemee binadamu kuteuliwa kuwa mawaziri..tena binadamu wenye madhaifu mengi. Lakini wakivurunda, sheria itafanya kazi yake.
Hizo hadithi zako wala hazina mashiko.
 
kama hajaathiriwa mbona jana cc ya ccm wamekataa baadhi ya majina ya watu alio wateua uwaziri na kumtaka kuyaondoa baadhi ya majina kwa madai kwamba hawana mchango wa maana ndani ya ccm, huku wakimtaka kuingiza watu ambao cc inawaona wanamchango kwa ccm

ccm ni ile ile
 
kama hajaathiriwa mbona jana CC ya ccm wamekataa baadhi ya majina ya watu alio wateua uwaziri na kumtaka kuyaondoa baadhi ya majina kwa madai kwamba hawana mchango wa maana ndani ya ccm, huku wakimtaka kuingiza watu ambao CC inawaona wanamchango kwa ccm

embu shuka utupe ubuyu ilikuwaje majina mangapi wameyakataa wanataka walafi

Kweli serikali iendelee na wale wale, michango ccm kuwa mbunge sio mchango kwao naona duh.
 
Ndani ya ccm ile ile na watu wale wale hatugemei jipya kwenye huu utawala wa ccm tena
 
Hakuna mtanzania anatetegemea Magufuli ateue malaika. Tanzania ina binadamu tu, tutegemee binadamu kuteuliwa kuwa mawaziri..tena binadamu wenye madhaifu mengi. Lakini wakivurunda, sheria itafanya kazi yake.
Hizo hadithi zako wala hazina mashiko.

Umeifunga hii thread, tena vema kabisa.
Bravo!!!!
 
Watu wanadhani baraza la Mawaziri atakalo liunda Magufuli litakuwa la ajabu sana kana kwamba litawahusisha malaika toka mbinguni. CCM ni ile ile na watu wake ni wale wale wala usitegemee kitu kipya sana sana sura za akina January Makamba, Nchemba, Migiro, Nyarandu n.k ndio tutegemee kuziona.

Wala usitegemee watu kama nchemba , januari kukosekana mbona patachimbika . wewe unafikiri baada ya kizazi cha akina kikwete ndani ya ccm kizazi kinachofuatia ni cha akina nani ndani ya CCM.

Acheni mawazo ya kudhani kwamba baraza la Mawaziri la Magufuri litajaa Malaika. Nyani ni wale wale na msitu ni ule ule.

Nchi hii inahitaji mtu mmoja tu kurudisha mambo kwenye mstari unaoeleweka. Magufuli amedhihirisha ni wapi tulijikwaa.
 
Back
Top Bottom