MURUSI
JF-Expert Member
- Jun 25, 2013
- 4,472
- 8,692
Hii nchi Utamaduni wetu ni kila mmoja aonekane ana Biashara yake, awe na Basi lake liandikwe jina lake apate sifa mtaani na kadhalika, hizi ndo aina za Biashara tunapenda sisi.
Watanzania biashara zetu zimejengwa juu ya msingi wa Udondo mtupu hasa pale itakapo kuja swala la Ushindani wa kutisha kutoka nje.Biashara zetu asilimia kubwa haziwezi kuhimili ushindani wa kutoka nje.
Nitatoa Baadhi ya Mifano Michache ninayo iona;
UJENZI
Tuna makampuni mengi sana ya Ujenzi ya wazawa yako mengi balaa, lakini angalia ni kampuni zipi zinapewa tenda ya kujenga Majumba makubwa na pia kujenga Barabara za lami nchini, Utaona ni Wazungu, Wachina na Wahindi ndo wanao tujengea Barabara zetu huku sisi tukiwa na utitili wa makampuni ya Ujenzi, Mpaka sasa hatutaki kujifunza na tumekomaa kila mtu na kikampuni chake tunasubilia janja janja na huruma tupate tenda za kuchonga Barabara za vumbi za mitaani, Hakuna hata single Company ya Ujenzi inaweza hata robo kushindana na Wachina au Wazungu.Ila Kampuni zetu zingeungana wakawa na kampuni yenye nguvu wanaweza, shindana hatutaki kwa sababu kila mmoja anataka aonekane.
USAFIRISHAJI
Hakuba haja ya kuwa na utitili wa wamailiki Daladala kwenye miji kama Dar, pale Kampuni hata 6 kubwa zinatosha kabisa kutoa huduma, ipo siku watu watakuja watamwaga Mabasi na tunaanza kulia ni Vidaladala vyetu, tunashindwa kusoma alama za nyakati kabisa,
UTITIRI WA VIWANDA
Siku hizi kumeibuka kutoka SIDO wanatoa mfunzo ya kuzalisha Sabuni, mara mafuta, Unga lishe na kadhalika, unakuta mtaa mmoja kuna Wazalisha Sabuni za maji kama 100 hivi na kila mtu anakomaa mwenyewe, hawa wana Idea inafanana ila waambie waungane asieee hutawaona na watakuja na sababu Miliona 1 za kwa nini hawataungana. Hivyo viwanda haviwezi fua Dafu kokote kule kwenye ushindani, na vingi vimekuwa vinajifia vyenyewe, Wachina unakuta Kiwanda kimoja kina share holder kama 600 hivi, Wachina kampuni zao nyingi ni Muungano wa watu wengi sana wenye malengo sawa, na ndo hao wanaotoa kichapo kwenye viwanda vyetu.
VI MIN SUPER MARKET
Hizi ni nyingi sana hasa Dar kila mtu anaona sifs kuea nacho cha kakwr, ila kusanya Min Super Markrt 100 Dar haziwezi shindana na Supet market moja kama Shorppers, na zinginezo kama Village Super Market.
Hizi Min nyingi watu wangeweza kuungana wakaja na Super market za kutoa ushindani lakini wapi hilo haliwezekani kabisa.
Sekita Ziko nyingi sana ambazo Watanzania hakika tusipo unganisha nguvu ipo siku tutaenda kulilia chooni, hatutaweza shindana na Viwanda vya India, China, Ulaya, na hawa walivyo wajanja wanakuja hata kusimika kiwanda huku huku kwetu.
Watu wanakuja na Mitaji yao wanayo pewa kutoka kwao, na watafanya vitu vikubwa ambayo sisi biashara zetu itabidi tufunge, na shida kuu tumekalia negativity kwamba Ohoo Watanzania hatuwezi ungana, hilo haliwezekani na kadhalika, Ok tungoje tuendelee kufixiwa na Wachina.