iparamasa
JF-Expert Member
- Nov 14, 2013
- 13,438
- 14,916
Naona kama watanzania tunaondolewa kwenye hoja.
kuna viongozi wanapeana zamu kutoa kauli tata,kukashifu,kujitoa akili,kufanya mikutano eti wasikilize hoja za wananchi,kufuta hati mashamba ya watu,tena wengine kwenye mikutano yao,wanaongea kama waliochanganyikiwa.
Mimi nawaona hawa kama waliopewa kazi maalum kuwavuruga watanzania kimawazo ili wasijadili suala zito,jamani nchi imenasa kwenye tope,tena tope zito sana na hakuna mwenye upeo wa kuinasua.
Kinachofanyika ni kuibua vihoja uchwara ili kutuondoa kwenye mada,wataibua hoja ya uhakiki ya watumishi hewa,wakapiga kelele mwaka mzima,mida mrefu ambao wangeutumia kufanya miradi ya maendeleo,heeee!!Zitto kabwe kawaumbua,kawaambia,jamani kama kweli mmetoa wafanyakazi hewa elfu kumi na saba,mbona bili ya mshahara iko vile vile!!,kwa aibu,wakaacha na sasa wamehamia kujadili sijui wa kigezo kipi aende chuo au asiende.
Jamani hawa ni watu ambao wana hoja za kujibu,wasitutoe kwenye hoja,hawa watu wameshindwa kukopesha wanafunzi wa vyuo,hawa watu benki zinakufa mbele ya macho yao,hawa watu viwanda vinakufa mbele ya macho yao,hawa watu hawajui hata maana ya fixed deposit account na faida yake,hawa watu wansema elimu bure kumbe huko mashuleni ni majanga,hawa watu hawajui taratibu za utumishi wa umma,hawa watu hawajapeleka milioni hamsini kila kijiji,hawa watu hawana hata ramani ya viwanda,hawa watu hawajapeleka pesa za maendeleo kwenye halmashauri
hawa watu mwaka jana walichoma bilioni 200 kwenye katiba mpya na wakaiweka kwenye ilani,leo aliyepewa ilani anasema mambo ya katiba hayamuhusu
jamani,tusitoke kwenye hoja,hii janja janja ya vimikutano uchwara ni kututoa barabarani