Watanzania tusipotezwe kwenye hoja,hawa jamaa nchi imewashinda,tusikubali kujadili kauli zao tata

iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,438
14,916
Naona kama watanzania tunaondolewa kwenye hoja.

kuna viongozi wanapeana zamu kutoa kauli tata,kukashifu,kujitoa akili,kufanya mikutano eti wasikilize hoja za wananchi,kufuta hati mashamba ya watu,tena wengine kwenye mikutano yao,wanaongea kama waliochanganyikiwa.

Mimi nawaona hawa kama waliopewa kazi maalum kuwavuruga watanzania kimawazo ili wasijadili suala zito,jamani nchi imenasa kwenye tope,tena tope zito sana na hakuna mwenye upeo wa kuinasua.

Kinachofanyika ni kuibua vihoja uchwara ili kutuondoa kwenye mada,wataibua hoja ya uhakiki ya watumishi hewa,wakapiga kelele mwaka mzima,mida mrefu ambao wangeutumia kufanya miradi ya maendeleo,heeee!!Zitto kabwe kawaumbua,kawaambia,jamani kama kweli mmetoa wafanyakazi hewa elfu kumi na saba,mbona bili ya mshahara iko vile vile!!,kwa aibu,wakaacha na sasa wamehamia kujadili sijui wa kigezo kipi aende chuo au asiende.

Jamani hawa ni watu ambao wana hoja za kujibu,wasitutoe kwenye hoja,hawa watu wameshindwa kukopesha wanafunzi wa vyuo,hawa watu benki zinakufa mbele ya macho yao,hawa watu viwanda vinakufa mbele ya macho yao,hawa watu hawajui hata maana ya fixed deposit account na faida yake,hawa watu wansema elimu bure kumbe huko mashuleni ni majanga,hawa watu hawajui taratibu za utumishi wa umma,hawa watu hawajapeleka milioni hamsini kila kijiji,hawa watu hawana hata ramani ya viwanda,hawa watu hawajapeleka pesa za maendeleo kwenye halmashauri

hawa watu mwaka jana walichoma bilioni 200 kwenye katiba mpya na wakaiweka kwenye ilani,leo aliyepewa ilani anasema mambo ya katiba hayamuhusu

jamani,tusitoke kwenye hoja,hii janja janja ya vimikutano uchwara ni kututoa barabarani
 
Kwahiyo anaamini ktk nguvu za hirizi? Na anakwenda kanisani? Au ni lile la walevi? Mungu ashushe neema kwake ili ampokee Roho Mtakatifu atamsaidia
 
Sifa yao nazani ni kuongoza wanyama.uko nazani wana taaluma nao..!nchi imewashinda total.mazingaombwe tuh!
 
Sizonje timu imemshinda!! Amepagawa!!

Sio siri tuseme wazi bila ushabiki Sizonje hakufaa hata kwa ratili moja kuvaa viatu alivyopewa....
 
Kwahiyo anaamini ktk nguvu za hirizi? Na anakwenda kanisani? Au ni lile la walevi? Mungu ashushe neema kwake ili ampokee Roho Mtakatifu atamsaidia
Rejea video ya Kakobe. Alimtaja jina kisha akauliza makondakta umeokoka wewe? Una vimada wangapi, rudi msalabani. Jikonda hakukanusha wala kumshitaki Kakobe
 
Iparamasa;
Umepata wapi uhodari huu?? Bujibuji, angalia begani kaka, nyuma salama huko?? Nawaombea Mola awape ulinzi tu. Ukweli ukipayukwa huitwa uchocheaji. Miye simo nasema simo.
 
Ile hoja ya zito nilivyofikiri mimi ni kwamba Wameteuliwa Watumishi/viongozi wengi wapya kushika madaraka ya UDc, Uded nk na wale wa awali ambao ni wengi kuendelea kulipwa mishahara ileile wakipangiwa majukumu mengine au wakisubiri kupangiwa. So Kwa mfumo wetu wateuliwa hulipwa vizuri zaidi ya watumishi wa kawaida. Tuwe na subira tu, mambo yatakuwa mazuri mbeleni.
 
Naona kama watanzania tunaondolewa kwenye hoja.

kuna viongozi wanapeana zamu kutoa kauli tata,kukashifu,kujitoa akili,kufanya mikutano eti wasikilize hoja za wananchi,kufuta hati mashamba ya watu,tena wengine kwenye mikutano yao,wanaongea kama waliochanganyikiwa.

Mimi nawaona hawa kama waliopewa kazi maalum kuwavuruga watanzania kimawazo ili wasijadili suala zito,jamani nchi imenasa kwenye tope,tena tope zito sana na hakuna mwenye upeo wa kuinasua.

Kinachofanyika ni kuibua vihoja uchwara ili kutuondoa kwenye mada,wataibua hoja ya uhakiki ya watumishi hewa,wakapiga kelele mwaka mzima,mida mrefu ambao wangeutumia kufanya miradi ya maendeleo,heeee!!Zitto kabwe kawaumbua,kawaambia,jamani kama kweli mmetoa wafanyakazi hewa elfu kumi na saba,mbona bili ya mshahara iko vile vile!!,kwa aibu,wakaacha na sasa wamehamia kujadili sijui wa kigezo kipi aende chuo au asiende.

Jamani hawa ni watu ambao wana hoja za kujibu,wasitutoe kwenye hoja,hawa watu wameshindwa kukopesha wanafunzi wa vyuo,hawa watu benki zinakufa mbele ya macho yao,hawa watu viwanda vinakufa mbele ya macho yao,hawa watu hawajui hata maana ya fixed deposit account na faida yake,hawa watu wansema elimu bure kumbe huko mashuleni ni majanga,hawa watu hawajui taratibu za utumishi wa umma,hawa watu hawajapeleka milioni hamsini kila kijiji,hawa watu hawana hata ramani ya viwanda,hawa watu hawajapeleka pesa za maendeleo kwenye halmashauri

hawa watu mwaka jana walichoma bilioni 200 kwenye katiba mpya na wakaiweka kwenye ilani,leo aliyepewa ilani anasema mambo ya katiba hayamuhusu

jamani,tusitoke kwenye hoja,hii janja janja ya vimikutano uchwara ni kututoa barabarani
Mbowe ndio amefilisika hadi ameshindwa kulipa madeni yake
 
Back
Top Bottom