mshikachuma
JF-Expert Member
- Dec 2, 2010
- 2,853
- 627
Nikiwa kama mtanzania wa kawaida ambae ninaipenda nchi yangu,sina budi nikitoa maoni yangu.
Nimejaribu kufatilia sana siasa za Tanzania tokea uchaguzi wa vyama vingi mwaka 1995 kipindi cha kampeni. Nakumbuka uchaguzi wa mwaka huo chama kikuu cha upinzani kilikuwa ni Nccr mageuzi
ya akina Mrema against chama tawala ccm ambacho mgombea wake alikua Benjamini mkapa.
Ukiachilia vyama vyote vya upinzani wakati huo,chama ambacho kilikubarika na watu ni Nccr mageuzi
Ccm walipogundua kuwa Nccr ni hatari na nitishio kwao,wakaenda mafichoni,waliporudi wakaja na pro
paganda ya kuwa Nccr mageuzi ni chama cha kikabila [wakimaanisha wachaga] na maana ya NCCR ni
Ni Chama Cha Rabsha. Kwakua kipindi hicho baadhi ya watanzania wengi tulikuwa na mawazo mgando
tukainyima kura Nccr na Mrema wake. Tukaipa kura ccm na mkapa akashinda japo si kwa kishindo.
Uchaguzi wa mwaka 2000 ikatokea chama kingine chenye nguvu na sera mzuri against ccm nacho ni
CUF,kikiongozwa na mh.Lipumba kwa huku Bara na visiwani kikiwakirishwa na Seif sharif Hamadi.
Ccm kama kawaida yao walipoona CUF inakubarika na wananchi,wakaingia tena mafichoni, waliporudi
tu wakaja na bonge la propaganda ya kuwa CUF ni chama cha kidini [hapa walilenga uwislaam].
Haitoshi wakaagizia mapanga nje ya nchi na yakaja kwenye contena yakiwa yana bendera za CUF.
wakaviita vyombo vya habari kuja kushuhudia ugaidi wa Cuf! kumbe si kweli bali propaganda tu!.
Kwahiyo yale ya mwaka 95 yaliyomkuta Lyatonga na Nccr yake,ndio yaliyemkuta mh.Lipumba na
cuf yake. Watanzani tukaigopa Cuf kama ukoma na kura zote tukaipa ccm,na wakashinda tena kwa
propaganda zao
Uchaguzi wa mwaka 2005 nao ukaja na vitukovyake. kwanza wapinzani hawakuwa na nguvu kama
chaguzi zilizopita. kwahiyo ccm kama kawida yao wakazama mafichoni,walivyorudi huko wakaja na uo
ngo unaofanana na propaganda kwa wadanganyika [walikuja na vitu 3] ili tuwachague tena.
Kwanza walisema chagua ccm maisha bora kwa kila mtanzania.Pili wakasema mgombea wao [mh.kikwete] ni 'handsome'yaani ni mzuri ki umbo. Tatu wakasema kikwete ni chaguo La mungu. Wadanganyika tukaichagua ccm,na kikwete akashinda kwa kishindo.kumbe uongo mtupu!
Lakini mambo yaliyotokea ndani ya miaka hiyo mitano hakuna asiyejua! ni vurugu tupu hakuna cha
maisha bora wala babu yake maisha tamu! Badala yake tukashuhudia ufusadi wa kutisha na maisha
kuendelea kuwa magumu kwa watanzania tulio wengi.
Uchaguzi uliyopita wa mwaka huu 2010 ulikuwa wa aina yake kwa wananchi wengi kuwa na mwitikio.
Pamoja na vyama vyote vilivyoshiriki uchaguzi huo,chama ambacho kilikuwa na nguvu ya ajabu na kukubarika na wanchi kwa kasi ya ajabu ni Chadema ambacho kwenye kampeni zake kiliongozwa na
Dr Slaa na timu yake iliyo makini. Hakika hiki ni Chama cha upinzani ambacho hakijawai tokea Tanzania. Chama ambacho kilikuja na sera mzuri,viongozi imara,wasomi na wenye uchungu wa Tanzania na raia wake! Hakika waliichambua serikali ya ccm kuanzia utosini hadi unyayoni na watanzania tukaamka for first time.
Lakini kama kawada ya ccm,wakaenda mafichoni waliporudi huko wakaja na bonge la propaganda lenye sumu kali. Wakasema Chadema ni chama cha kidini [hapa walilenga ukristo]na ukabila.
Kwa watu kama sisi ambao tunazijua propaganda za ccm tukasema Nooo! thiz time we have to vote for change,na tukaipa kura chadema. Ila kwa wale waliokuwa teyari kuipa kula chadema wakati huo huo hawazijui propaganda za ccm 'hasa vijijini' waliposikia sumu za ccm wakabadilisha mawazo na wakaipa kura ccm au hawakwenda kabisa kupiga kura. kwahiyo ikawa faida na neema kwa ccm na
hasara kwa Chadema. ccm ikashinda tena japo si kwa kishindo kama chaguzi zilizopita.
Narudia tena, Chadema ni chama ambacho hakijawahi tokea Tanzania bara! kimetuonyesha kina
sera mzuri,uongozi imara,na kina future ya Tanzania tunayoitaka! kimepata wabunge wengi bara kuliko chama chochote cha upinzani. Ni chama ambacho kimekubarika pande zote za Tanzania bara!
Na isingekuwa propaganda za ccm,basi Chadema ingeshika Dola na leo ingekuwa story nyingine.
Hitimisho langu ni-
Watanzania tusikubari propaganda hizi za Ccm! Ni hatari sana hawa watu hasa wanapoona kuna chama cha upinzani makini na chenye uongozi imara,hapo wao wako teyari waivuruge nchi kwa
propaganda za sumu ili mladi waendelee kutawala! Camooon guys tuamkeni watanzania! hii ni
nchi yetu wote na tunawajibu ya kuipigania kwa manufaa ya walio wengi! Ahsanteni.
Nawakilisha.