Watanzania tusifurahie, hapatokuwa na jipya katika baraza la mawaziri la hivi karibuni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania tusifurahie, hapatokuwa na jipya katika baraza la mawaziri la hivi karibuni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Chaimaharage, May 1, 2012.

 1. Chaimaharage

  Chaimaharage JF-Expert Member

  #1
  May 1, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimesema maneno hayo nikimaanisha kwamba siyo mara ya kwanza JK anafanya mabadiliko ya baraza lake la mawaziri pasipo kuwa na tija yoyote. Nitakupeni mfano; hivi walipo ondoka akina Msabaha na Karamagi uteuzi uliofuatia kujaza nafasi zao ulileta mabadiliko yoyote? jibu ni hapana hilo liko wazi kwa sababu kwanza ndio ufisadi umezidi.

  Je, kwa nini mabaraza yote anayoteua JK yamekuwa mabovu? jibu ni rahisi; Ni kwamba huyu jamaa anatumia formula/kanuni zile zile katika uteuzi wake. Haangalii mambo ya msingi yenye tija kwa taifa anapokuwa ana teua majina. Mara nyingi huwa anaweka ushikaji mbele na mengine ndipo yatafuata. Unadhani kwa mfano anaweza kuweka waziri wa fedha ambaye atamwambia "tuchote fedha" akatae? n.k. Wizara zote nyeti hawezi kuweka mawaziri makini nikimaanisha umakini wao katika uadilifu na kuweka maslahi ya taifa mbele.

  Piga pangua hawezi kwa mfano kumpatia Magufuli uwaziri mkuu, Mwakyembe labda katiba na sheria, Sitta fedha au nishati na madini n.k. Nyie mtaona uteuzi wake, watu wa ajabu ajabu tu..na hiyo ni kutokana na formula anayotumia niliyosema hapo juu.

  Kwa hiyo kwa kifupi TUKUBALI MAUMIVU MIAKA 10 IMEPOTEA BURE KATIKA UTAWALA WA HUYU JAMAA. Tumuombe Mungu atuweke hai na tupate serikali mpya yenye mawazo mapya, sera mpya, sura mpya, itikadi mpya 2015. Bila shaka siyo magamba tena. Tusijidanganye wala tusitarajie chochote kizuri chini ya utawala wa JK.

  Labda tu utokee muujiza kabla ya 2015 unaoweza kutuondolea huyu mtu. Lakini nina imani kwa hali ilivyo sasa akifikisha muda huo basi atakuwa na miungu yake na siyo Mungu nimjuaye.
   
Loading...