Watanzania tusidanganyike Magu tupe katiba ya Warioba kwanza...kama unania ya dhati na hii nchi

baba anjela

JF-Expert Member
Mar 17, 2013
385
250
Mimi nashindwa kumwelewa Magu na Watanzania... Fisadi mkubwa wa hii nchi ni katiba tuliyonayo... kigugumizi kinatoka wapi kwa mkuu kutupa katiba ya Warioba...

Tusidanganyane bwana,leo tunapeleka mikataba ya kipindi cha kikwete na mkapa bungeni....lakini ya Magu hatuipeleki sasa tunafanya nini... tunajua nini kimefanyika kwenye mikataba yake... au yeye ni nabii

Warioba na tume yake ...wako wapi...hivi kweli mtu anasema kipaumbele chake si katiba mpya...leo anasema anania ya dhati na nchi yetu...katiba mpya hataki kutupa...au nikulinda kinga ya maraisi waliyopewa katika hii katiba ya kifisadi.


Ushauri.

1.Katiba mpya tupate ....kama mambo ya accacia yalivyopelekwa spidi na mchakato wa katiba mpya tunataka hivyo hivyo.

2.Bunge kabla ya kujadili hiyo mikataba...ya madini ,watunge sheria mpya...serikali kutosaini mikataba yoyote yenye maslahi mapana ya nchi mpaka .. mpaka bunge lijadili mikataba hiyo na kupitishwa....

3.Wazee wa ndiyooo kwa kila kitu...au hapanaaaa kwa kila kitu.... ushauri wangu kwa haya magroup 2....tuwekeni uchama pembeni....taifa kwanza....

wangetembea baadhi ya nchi kujifunza...wengine wanafanyaje kazi...katika huu mfumo wa vyama tofauti bungeni...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom