Watanzania turudi kwenye UMOJA wetu

kibito

Member
Jul 12, 2015
49
26
Ndugu wana jamvi, heri iwe kwenu.

Lengo la kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi lilikuwa ni kupanua demokrasia ili kila mtu aweze kuwa na sehemu ya kutolea maoni yake kwa uhuru na bila kuvuruga Umoja na Amani ya nchi yetu.

Mfumo huu siyo mbaya, isipokuwa naona kuna sehemu tumejichanganya kidogo...Uniform na Bendera za vyama vya siasa. Mimi naliona hili ni tatizo kubwa kwa jamii yetu hasa ukichukulia uchanga wa demokrasia yetu. Ili kuendelea kulinda Amani na Umoja wetu, mimi napendelea kuondoa 'Unform' za vyama vyote na bendera zao ili nchi ibaki na bendera moja tu ya TAIFA na nyingine ambazo hazihusiani na vyama vya siasa.

Hii itasaidia kupunguza kutugawa kwenye makundi ya wazi ya kisiasa. Itapendeza hata kwenye mikutano ya vyama watu wakawa na bendera ya Taifa hata kama watakuwa hawana 'uniform' ya kitaifa ili kuondoa mgawanyiko wa wazi wa kisiasa kwenye jamii yetu.

Nawasilisha.
 
Napenda ccm imara na upinzani imara.
Tatizo lililo kuwepo huko nyuma ni ccm dhaifu na upinzani dhaifu.
Lakini sasa naona ccm imara na itaimarika chini ya mwenyekiti mpya imara mwezi huu.
Kinachonisikitisha wenzetu wapinzani wanakuwa dhaifu.
 
Napenda ccm imara na upinzani imara.
Tatizo lililo kuwepo huko nyuma ni ccm dhaifu na upinzani dhaifu.
Lakini sasa naona ccm imara na itaimarika chini ya mwenyekiti mpya imara mwezi huu.
Kinachonisikitisha wenzetu wapinzani wanakuwa dhaifu.

Tatizo naoana CCM ikichukua mkondo wa ukandamizaji mkubwa na upinzania ukikosa mbinu sahihi kukabiliana na kitisho hicho.Kususia bunge kisa Naibu Spika nadhani ni udhaifu wa hali ya juu.
 
Back
Top Bottom