Watanzania tupendane, tusaidiane, tushirikiane na tushikamane, lets stand as one. Ila pia tuelezane ukweli, why tumekula ng'ombe mzima tukabakiza mkia

Na uombe isitokee vita kati ya Tanzania na nchi yeyote ya jirani kwa sasa, maana hujaona bado chuki na mgawanyiko uliokolezewa moto na Serikali hii ya awamu ya 5.. Vita vya Kagera 1978 wananchi walikuwa wanajitolea (bila ya shuruti) mpaka vyombo vyao vya usafiri kwa sababu ya uzalendo.. Ikitokea vita sasa, nahisi majeshi yatakayotushambulia yatapewa mpaka hifadhi na baadhi ya wananchi wengi..

Wenye mapenzi mema na nafasi za uongozi, walifanyie kazi huu ni mpasuko mkubwa sana..
Watanzania tunapendwa na serikari yetu na tunapendana kama anavyotuhakikishia mkuu wa kaya.
 
Upuuzi mtupu..
1. Kiongozi lazima alinde maslahi ya sasa na yajayo..huwezi hurumia machozi ya wavunja sheria kwa gharama ya kizazi kijacho, laana wanayo wao wenyewe kwa kukaidi kutii sheria, na kiongozi hayupo hapo ili raia wote wafurahi NEVER! wavunja sheria na wabinafsi watakuja na misemo kama hii aliyoandika huyu.

2. Waislamu wenyewe baadhi ndiyo wabaguzi namba moja! lakini tuwe wakweli tu, ukitizama mabadilishano ya awamu kila alipoongoza muislamu mambo yanaparaganyika, rushwa, upendeleo, uzembe mwingi kila mahali, dharau nk..huwezi teua watu kufuata imani yao, mbona wapagani wasio na dini za kuletwa hatujawasikia wakilalama kutengwa, lakini wapo! yanayofanyika leo ni matkeo ya uharibifu uliofanywa na waliotangulia, maumivu haya wa kulaumiwa ni yule aliyesababisha kasoro hizi zinazoshughulikiwa sasa kutokea, halafu niseme wazi tu, baadhi ya waislamu wana mentality mbovu kabisa ya utegemezi, kwamba kila kitu yupo mtu wa kusaidia hata kwa vitu ambavyo anaweza kuvifanya..ndio maana mikoa mingi yenye waislamu wengi ni masikini, Lindi, mtwara, Tabora, kigoma, Pwani..kwa nini siyo kagera, Kilimanjaro..WHY??

3. Maana ya kiapo ni kulinda na kutetea wanyonge na ndicho Rais anafanya! wanyonge wa Tanzania wanamuelewa sana na kumuombea Baraka zote, baraka anatoa Mungu si kwa wishes za binadamu, kama kinachofanyika ni kile ambacho aliyekuumba anataka! katiba, sheria vinatungwa na binadamu na vinaweza kuwa na madhaifu, hivyo huwezi tii jambo lina udhaifu simply limeandikwa kwenye katiba..! tenda yale Mungu anataka hata kama binadamu wooote watakuwa kinyume na wewe!

Ndege kushikiliwa ni jambo dogo sana kati ya yote anayofanya Rais, mpaka sasa ameshaweka legacy hata kabla ya muda wake kwisha..na hao wanatoa mfano eti vita ikitokea tutashindwa, mtashindwa nyinyi wa mijini wabinafsi na walafi, watanzania wa vijijini wako na Rais hadi tone la mwisho la damu!

Hebu tuonyeshe wakulima wanaosimama na Magufuli ambao maisha yao yameboreka na iwapo leo atatoka madarakani basi watapata tabu. Mnawalisha maneno watu wa vijijini maana hawajui lolote na hawana pa kusemea. Hao wanakijiji tunawaona na umasikini wao tunaujua. Hakuna yoyote ambaye maisha yake yamebadilika mpaka useme rais huyu ni mkombozi wao.
 
Paskali, mfano mzuri ni pale hamasa ya wtz iliposhuka ghafla baada ya Bashite kuimilikisha CCM timu yetu taifa stars wkt wa Afcon huku akijua timu ni ya watz wote. Mambo haya madogo madogo yanaligawa taifa . Aliyeanza haya madai ya kijinga kuwa kuna watu ndio sababu ya kushikiliwa ndege yetu ni huu musiba wa taifa ambaye amekuwa akilindwa kwa nguvu zote aendelee kuigawa nchi vipande vipande. Huo upendo unaohubiri utatoka wapi!
 
Mimi siyo msukhuma
Wanabodi,

Leo ni Jumatatu nyingine, nimepata fursa za kuendelea na zile makala zangu za “Kwa Maslahi ya Taifa”, kwa vile sakata la kushikiliwa kwa ndege yetu nchini Afrika ya Kusini, kunaendelea, nami leo naendelea na kuzungumzia kushikwa kwa ndege hiyo lakini katika muktadha wa tukio hili, lituimarishe katika uzalendo wetu kwa nchi yetu, tuongeze upendo baina yetu kwa kuipenda nchi yetu, serikali yetu na viongozi weke, na badala ya kulitumia kufarakana, tulitumie kutuongezea mshikamano baina yetu na baada ya kukombolewa kwa ndege yetu, then sisi Watanzania, tukae chini na kuambiana ukweli, na kwa uwazi bila kuficha ficha, ni nini haswa kilichosababisha mdeni wetu huyu asilipwe deni ambalo tumeishakula ngombe mzima, tukabakiza tuu mkia na kuamua kukataa kulipa.

Hili la kushikwa kwa ndege yetu ni janga, wakati wa majanga, ndipo unaweza kubaini nani ni rafiki wa kweli na nani sii rafiki, majanga badala ya kuleta tafrani na utengamano, huleta upendo, ushirikiano na mshikamano, natoa wito kwa hili la ndege, Watanzania tuungane tuwe kitu kimoja chini ya serikali yetu wakiwemo wanasiasa, vyama vyote, Watanzania wote, lets stand as one, wakiwemo CCM na Wapinzani, tuwe kitu kimoja, tusimame pamoja na serikali yetu na tuongee lugha moja na sauti moja, ndege yetu iachiwe.

Wanasiasa wa pande zote, badala ya kuanza kunyoosheana vidole nani kafanya nini, tuhubiri zaidi upendo, ili kujenga mshikamano wa kweli kwa serikali, CCM, Wapinzani na Watanzania wote kwa ujumla, hili tukio, lituunganishe, lituongezee upendo wa kupendana kwa dhati, kuheshimiana, na kushirikiana kuleta maendeleo kwa taifa letu kwa sababu, its only together we can!. Maadam sote tunajenga nyumba moja ya Tanzania, tunagombea fito za nini?.

Upendo ndio amri kuu kuliko zote humu duniani ambayo Mungu ametupa. Naomba kuazima hii mistari kutoka kitabu fulani kuhusu upendo "Upendo huvumilia, upendo hufadhili; upendo hauna wivu au majivuno. Upendo hauna kiburi na haukosi kuwa na adabu. Upendo hau tafuti kujipendeza nafsi; haukasiriki upesi, hauweki orodha ya mabaya. Upendo haufurahii mabaya, bali hufurahia kweli. Upendo huvumilia yote, huamini yote, hutumaini yote, hustahimili yote"

Kwa vile CCM ndio chama tawala na serikali yake, viongozi wake wote kuanzia juu kwa Mwenyekiti hadi kwa mjumbe wa shina, na viongozi wote wa serikali, kuanzia rais wa nchi hadi mwenyekiti wa serikali ya mtaa, wana wajibu na jukumu sio tuu la kuhubiri upendo kwa maneno tuu, bali kwa kufanya matendo yanayoashiria upendo wa kweli, (practicing what you preach) kwa kuwapenda kwa dhati Watanzania wote, na watu wote, wakiwemo wapinzani ambao nao ni Watanzania, itawaheshimu wote, haitawanyanyasa, haitawabagua, haitawadharau, haitawabeza, wala kuwa tweza na itawatendea haki, wananchi wote.

Kama serikali ya CCM itaonyesha upendo wa dhati zaidi, pia itachukua yale mazuri ya wapinzani na kuwashirikisha katika kuya implement kwa mustakabali mwema wa taifa letu.

Kwa kwa hali ilivyo sasa kati ya CCM na Wapinzani ni kama paka na panya, hali inayopelekea taifa linapokumbwa na majanga kama hili la kushikwa kwa ndege yetu, CCM, serikali na wale wenye mapenzi mema na taifa letu, tunaumia kuona ndege yetu imeshikwa, huku baadhi ya wapinzania na wenzetu wengine wasiolitakia mema taifa hili, wakishangilia na kubeza kila kinachofanywa na serikali ya CCM, huu sio uzalendo.

Kuna dhana imejengeka kwa CCM ikijiona ndio pekee yenye hati miliki ya kutawala taifa hili la Tanzania milele, hivyo yoyote atakayetishia status quo ya CCM kutawala milele, kuonekana kama ni adui, na sisi jf tukiwemo, hivyo CCM inawaona wapinzani kama maadui wenye lengo la kuwapokonya tonge mdomoni, au kutaka kukitia mchanga kitumbua chao, hivyo kutumia kila mbinu kuhakikisha inabakia madarakani by hooks and crooks, ikiwemo kutumia mbinu ya bao la mkono, kuminya demokrasia, kuminya uhuru wa habari, uhuru wa kujieleza, uhuru wa kutoa maoni, uhuru wa kukusanyika, kukandamiza upinzani hata ikibidi kuikanyaga katiba, wataikanyaga kwa lengo la kuwakomoa wapinzani kumbe wanawakomoa wapinzani sio kuwakomoa wapinzani bali ni kuwakomoa, Watanzania wenzetu.

Kwa tukio kama hili la ndege yetu kushikwa na jinsi Watanzania tulivyogawanyika, kunapelekea mtu kujiuliza, hivi sisi Watanzania tuna upendo wa kweli na upendo wa dhati miongoni mwetu sisi kwa sisi bila kujali itikadi za vyama vyetu?, jee tunaupendo wa kweli na wa dhati kwa taifa letu?, haiwezekani taifa liwe kwa majanga halafu sisi tukagawanyika. Huu sio uzalendo. Tukio hili lituunganishe tuwe wamoja na kuongea kwa sauti moja.

Tanzania ni yetu sote, hii nchi sio mali ya CCM au mtu yoyote, ni mali ya Watanzania wote wakiwemo CCM wenye dhamana ya kutawala lakini pia Wapinzani na wengine wote hata wasio na vyama ndio maana tukaweka vipengele vya haki za kila mtu na wajibu wake kwenye katiba yetu, hivyo linapotokea tatizo la kitaifa, bila kujali limesababishwa ni nini, hatua ya kwanza ni kwa sisi Watanzania, kusimama pamoja kutatua tatizo, likiisha tatuliwa, ndipo tutakaa chini kufanya tathmini ni nani aliyetufikisha hapa, tukikutana kuna ushauri mbaya, watu wawajibike na tukikuta kuna usaliti, sheria ichukue mkondo wake.

Katika kushughulika kila jambo, CCM na serikali yake wana wajibu wa kuiheshimu katiba, sheria taratibu na kanuni ili kuonyesha upendo wa dhati kwa Watanzania wote wakiwemo wapinzani, nayo pia itapendwa na wote, na kuheshimiwa na wote wakiwemo wapinzani hivyo sote tutapendane kwa dhati kama Watanzania, tutaheshimiane na kushirikiana katika shida na raha, na katika kuleta maendeleo ya taifa letu.

Kwa kuanzia, kwanza naunga mkono hoja ya heshima, ni two way traffic, kwa mkubwa aheshimu mdogo na mdogo aheshimu mkubwa. Heshima ya kweli huwa earned na sio heshima ya kuwa forced. Mzizi wa heshima ya kweli ni upendo wa dhati. Hivyo upendo ndio utangulie kwa watu wote tupendande, bila kujali tofauti zetu, ndipo heshima ya kweli ifuatie na ipatikane, kwenye upendo wa kweli kunakuwa na heshima, amani, umoja na mshikamano. Kwenye hili la ndege yetu Watanzania tushikamane na serikali yetu.

Viongozi wa chama tawala wawapende kwa dhati Watanzania wengine wote wakiwemo wapinzani, kikiwa na upendo wa dhati, CCM itawaheshimu wapinzani na wapinzani wataiheshimu CCM na kushirikiana nayo kwa pamoja kuleta maendeleo endelevu ikiwemo kuwa kitu kimoja kwenye furaha na huzuni.

Natoa wito kwa serikali yetu kuwa wakweli na wawazi, sio kuhusu nini kilichosababisha ndege yetu kukamatwa, bali nini kilichosababisha tusimalizie kumlipa deni letu mdai wetu huyu.

Kwenye maisha ya kila siku ni kawaida sana kwa binaadamu kukopa, kudaiwa au mkopo au fidia, na kiukweli kabisa kudaiwa sio kosa, kosa ni kushindwa kulipa unachodaiwa, na ikifika mahali, ukazidiwa na madeni hadi yakawa hayalipiki, unakuwa muwazi tuu kuwa deni hili ama sio realistic, halilipiki, na hivyo kukaa na mdeni wako ukamuomba myamalize, hiki ndicho kilichofanyika kati lile deni la dola bilioni 190 la Acacia, tumafanya mazungumzo tukakubali kusamehe na sasa tutalipwa kifuta machozi cha dola milioni 300.

Kwenye kesi ya Richmond, kiukweli kabisa serikali yetu ilishauriwa vibaya, tukavunja mkataba, tukashitakiwa, tukashindwa tukadaiwa fidia, tukayamaliza kimya kimya. Ndege yetu ilipozuliwa Canada, tulidaiwa tukayamaliza kimya kimya, hili deni la huyu mdai nalo tulilipa tena ngombe mzima, tukabakiza mkia tuu, serikali yetu iwe wazi ni kwa nini hatukumalizia kulipa hadi tunakuja kudhalilishwa kiasi hiki?. Tuwe wakweli ili ukweli utuweke huru.

Deni hili limekuwa likionekana kwenye taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali mwaka hadi mwaka, pamoja na madeni mengine, kwa vile sasa tumeisha umwa na nyoka, na ndege zetu bado zinapaswa kuendelea na safari za nje, chonde chode serikali yetu, tusidharau mwiba mguu wetu ukaota tende, kinga ni bora kuliko tiba, tukae na wadeni wetu, tusemezane nao kwa uzuri, ili tukio kama hili lisije kujirudia tena kwa siku za usoni.

Tanzania ni yetu wote, tupendane kwa dhati kwa upendo wa kweli, tuheshimiane, tuijenge nchi yetu kwa kushirikiana na kwa mshikamano kwenye shida na raha. Tukipendana, tutaheshimiana na tutashirikiana kuleta maendeleo ya kulijenga taifa letu na kuliletea maendeleo.

Nawatakia Jumatatu Njema.
Paskali
 
Watapongeza hao hao kina Mayalla
Tarehe saba kuna mbunge mmoja alishambuliwa bila huruma. Baadae ulikuja kutetea humu kuwa cctv zaweza tolewa muda wowote ule endapo mmiliki wake ataona inafaa hilo likapita

Mbowe amesukwasukwa sana leo mahakamani kesho lockup keshokutwa mkutano wake umevurugwa na askari kwa maelezo toka kusiko julikana. Hilo likapita
Mikutano ya kisiasa, n.k

Watumishi wanapigishwa kwata ilianza uhakiki wakavumilia uhakiki ukaisha hakuna nyongeza, madaraja yao ya mishahara sasa wanaambiwa kukaa miaka 5+ ndipo wapandishwe kwa matamshi yake mwenyewe alisema kulikoniwaongezee bora ninunue ndege
unategemea upendo unao hubiriwa hapa ufanyiwe kazi?
 
Simpendi Idd Amin kwa sababu Idd Amin ni muuaji! by JK Nyerere- 1971 BAK
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Wao wanendelea kujidanganya kuwa nchi ina umoja kumbe wapi

Paskali ili ndege iachiwe serikali ilipe deni kama vile inavyotulazimisha sisi kulipa madeni inayotudai, huwa hatusomi dua isiyaone madeni inayotudai.
Huwezi kuwa na umoja na upendo kama shangazi anapompendelea mtoto mmoja katiyenu, akilamba sukari mnapigwa mliotoka shule! Ubayaubaya tu liwalo na liwe.
 
Serikali hii imesababisha kufungwa kwa baadhi ya kampuni na biashara kwa penalt/faini za madeni ya kodi kabla ya awamu ya tano tena bila huruma.Nina wahanga kama watano kwenye ukoo wangu wamerudi mtaani kwa sababu ya kufungwa kwa kampuni walizokuwa wanafanyia kazi.
My concern hapa serikali nayo ilipe deni la yule mkulima wa R.S.A isitake huruma kutoka kwetu wananchi kwa sababu haikuwa na huruma kwenye kufunga biashara na kampuni za ndani ya nchi na kuongeza jobless mtaani.UBAYA ,UBAYA TU HAIJARISHI KAFANYIWA NANI.
 
Mkuu Pascal unaandika haya hapa kwa uthibati wa moyo wako? ama moyoni hakuna kitu? unaandika tu kwamba Fulani akiona bandiko langu ama Makala yangu nitapata huenda nitapata ulaji Fulani?
 
Why watanzania wa kijijini pekee wawe na raisi? Kwani huyu ni raisi wa vijijini.Naona unapata shida sana kumtetea rais wako ila jua tu kuna makundi mengi mno hapa nchini includes hao unaosema wa kijijini walioumia kutokana na maamuzi ya utawala huu..
Upuuzi mtupu..
1. Kiongozi lazima alinde maslahi ya sasa na yajayo..huwezi hurumia machozi ya wavunja sheria kwa gharama ya kizazi kijacho, laana wanayo wao wenyewe kwa kukaidi kutii sheria, na kiongozi hayupo hapo ili raia wote wafurahi NEVER! wavunja sheria na wabinafsi watakuja na misemo kama hii aliyoandika huyu.

2. Waislamu wenyewe baadhi ndiyo wabaguzi namba moja! lakini tuwe wakweli tu, ukitizama mabadilishano ya awamu kila alipoongoza muislamu mambo yanaparaganyika, rushwa, upendeleo, uzembe mwingi kila mahali, dharau nk..huwezi teua watu kufuata imani yao, mbona wapagani wasio na dini za kuletwa hatujawasikia wakilalama kutengwa, lakini wapo! yanayofanyika leo ni matkeo ya uharibifu uliofanywa na waliotangulia, maumivu haya wa kulaumiwa ni yule aliyesababisha kasoro hizi zinazoshughulikiwa sasa kutokea, halafu niseme wazi tu, baadhi ya waislamu wana mentality mbovu kabisa ya utegemezi, kwamba kila kitu yupo mtu wa kusaidia hata kwa vitu ambavyo anaweza kuvifanya..ndio maana mikoa mingi yenye waislamu wengi ni masikini, Lindi, mtwara, Tabora, kigoma, Pwani..kwa nini siyo kagera, Kilimanjaro..WHY??

3. Maana ya kiapo ni kulinda na kutetea wanyonge na ndicho Rais anafanya! wanyonge wa Tanzania wanamuelewa sana na kumuombea Baraka zote, baraka anatoa Mungu si kwa wishes za binadamu, kama kinachofanyika ni kile ambacho aliyekuumba anataka! katiba, sheria vinatungwa na binadamu na vinaweza kuwa na madhaifu, hivyo huwezi tii jambo lina udhaifu simply limeandikwa kwenye katiba..! tenda yale Mungu anataka hata kama binadamu wooote watakuwa kinyume na wewe!

Ndege kushikiliwa ni jambo dogo sana kati ya yote anayofanya Rais, mpaka sasa ameshaweka legacy hata kabla ya muda wake kwisha..na hao wanatoa mfano eti vita ikitokea tutashindwa, mtashindwa nyinyi wa mijini wabinafsi na walafi, watanzania wa vijijini wako na Rais hadi tone la mwisho la damu!
 
Kwa kuongezea ni kuwa hao watu wa vijijini anaodai wamesimama na raisi ndo hao sisi wa mjini tulikuwa tunawatumia hela za mbolea na za kuandaa mashamba siku hizi hali ngumu hatutumi wataanzaje kumpenda huyo mtu alietutoa uwezo wa kusaidiana kwenye ukoo na familia.KASABABISHA TUONEKANE SIKU HIZI TUNA ROHO MBAYA KWA NDUGU ZETU UPENDO NA MSHIKAMANO WA KIFAMILIA NA UKOO UMEPOTEA KWA SABABU TUNAKIMBIANA MAISHA NI MAGUMU.
Vijiji vya wapi unavyoviongelea? Kuna vijiji hawataki kulisikia hata jina lake maana amewasababishia umaskini kwa sera zake mbaya:

1) mahindi mkoa wa Njombe, Ruvuma na Rukwa yalishuka bei mpaka sh 9,000 kwa gunia kutokana na serikali yake kuzuia yasiuzwe nje

2) kwenye korosho, alitufanya tuishi kama wahalifu. Ukionekana na korosho zako unasafirishs, ni kama vile unasafirisha madawa ya kulevya. Watu walikamatwa, walinyang'anywa na kuwekwa ndani. Wameziozesha korosho kwenye maghala, halafu webye kprosho wanaambiwa wakazichukue kwa vile hazina ubora

3) biashara iliyokuwa inalipa sana kwa mikoa kama Mbeya, Njombe na Iringa, ni biashara ya mbao. Wateja wazuri walikuwa ni Wakenya. Kutokana na chuki zake kwa Wakenya, hata ikasababisha vipingamizi vingi kuruhusiwa kupeleka mbao Kenya kama namna ya kulipiza kisasi kwa chuki walizokuwa wakifanyiwa Wajenya na serikali ya awamu hii

4) wakulima wa maparachichi walikuwa wakipata fedha nzuri kutokana na wanunuzi wa kutoka Kenya. Mwakajana kukawa hakuna soko kwa sababu Wakenya walisema wanasumbuliwa sana mpakani

5) wafugaji wa nyuki Mpanda, mwakajana na mwakajuzi walikuwa hawana soko la asali kwa sababu wanunuzi wazuri wa Kenya hawakuweza kununua kutokana na shida ya mpakani

Hii ndiyo legacy ambayo wewe unajivunia kwa awamu hii?
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Kama alivyo MUUAJI magufuli aliyewaua Ben Saanane, Azory Gwanda, lissu kaponea kudra za Mwenyezi Mungu na Erick Kabendera na wale Watanzania wenzetu waliookotwa kwenye viroba kule ufukweni mwa bahari.

Simpendi Idd Amin kwa sababu Idd Amin ni muuaji! by JK Nyerere- 1971 BAK
 
Vijiji vya wapi unavyoviongelea? Kuna vijiji hawataki kulisikia hata jina lake maana amewasababishia umaskini kwa sera zake mbaya:

1) mahindi mkoa wa Njombe, Ruvuma na Rukwa yalishuka bei mpaka sh 9,000 kwa gunia kutokana na serikali yake kuzuia yasiuzwe nje

2) kwenye korosho, alitufanya tuishi kama wahalifu. Ukionekana na korosho zako unasafirishs, ni kama vile unasafirisha madawa ya kulevya. Watu walikamatwa, walinyang'anywa na kuwekwa ndani. Wameziozesha korosho kwenye maghala, halafu webye kprosho wanaambiwa wakazichukue kwa vile hazina ubora

3) biashara iliyokuwa inalipa sana kwa mikoa kama Mbeya, Njombe na Iringa, ni biashara ya mbao. Wateja wazuri walikuwa ni Wakenya. Kutokana na chuki zake kwa Wakenya, hata ikasababisha vipingamizi vingi kuruhusiwa kupeleka mbao Kenya kama namna ya kulipiza kisasi kwa chuki walizokuwa wakifanyiwa Wajenya na serikali ya awamu hii

4) wakulima wa maparachichi walikuwa wakipata fedha nzuri kutokana na wanunuzi wa kutoka Kenya. Mwakajana kukawa hakuna soko kwa sababu Wakenya walisema wanasumbuliwa sana mpakani

5) wafugaji wa nyuki Mpanda, mwakajana na mwakajuzi walikuwa hawana soko la asali kwa sababu wanunuzi wazuri wa Kenya hawakuweza kununua kutokana na shida ya mpakani

Hii ndiyo legacy ambayo wewe unajivunia kwa awamu hii?
Kwanza Rais hajaja na sera mpya,sera ni zile zile amekuja na uthabiti wa usimamizi tu! kama kuimarisha usimamizi ndiyosababu ya umaskini unaousema, nadhani akaze zaidi ili wakulima wa kweli wajulikane na si madalali wa wakulima kwa jina la wakulima..katika ziara zote ambazo Rais anapita vijijini aina ya mapokezi na shauku ya kuongea nae kuonyesha kuridhishwa na anavyoongoza nchi ni vitu kila mmoja mwenye akili timamu anaona wala hawezi kupinga na kuanza kubishana kama watu wasio na akili..wewe ndio ulete ushahidi wa vijiji, tena acha vijiji watu hata 10 tu ambao wanadai amewasababishia umaskini..onyesha!
Watanzania wengi wanatambua kuwa kiongozi mzuri ni yule anayeweka misingi imara ya ustawi wa nchi na watu wake kwa muda mfupi na muda mrefu, taifa hili haliishi kesho, hatuwezi kuishi kwa kufikiria leo tu, kama binadamu wote wangekuwa na mtizamo wa kufikiri tu hapo walipo sidhani hizo nguo ulizovaa ungezipata, au hata ungeweza kufikia umri huo ulio nao, ni wajibu kutizama mbele zaidi, ni bora kutokula mlo wa mchana leo ili kesho mpate milo mitatu! kwa wanaosoma historia za mataifa yaliyoendelea hayajafika hapo kwa lelemama za ujinga mnaoutaka, maendeleo yanataka sacrifice!
Wakulima wa Tanzania hawawezi kubadilisha kilimo chao kwa mtindo wa kulanguliwa mazao yao kiholela na wanunuzi wa msimu kutoka huko unakotaja..ili wakulima wanufaike na kazi yao, serikali inaweka miundombinu yote, barabara, huduma za ughani, mfumo mzuri wa kupima mazao, pembejeo nk ili soko la uhakika liwafikie wakulima na kununua mazao yao kwa bei inayostahili..hizo sarakasi mnazotaka za kufanya mambo holela hazijawahi kuleta faida yoyote kwa mkulima.
Wakulima wanahitaji elimu kwa watoto wao, huduma bora za afya, miundombinu imara na usimamizi thabiti wa kilimo mambo ambayo serikali inafanya kwa sasa.
Mwalimu aliwahi kusema, dawa ya kuondoa umaskini kwa watanzania walio wengi ni kusomesha watoto wao..ndio maana watanzania wa vijijini hawana muda na mabishano ya kijinga sababu wanajua kile serikali inafanya kwa ajili ya mustakabali wa maisha yao.
 
Sio rahis kupendana kama baba anawabagua na kuwanyanyasa baadh ya watoto wake ambao wanamwono tofauti na mawazo yake,kwa mfano baba yangu alikuwa mkali sana na misimamo migum sana lkn nilichompendea alikuwa anapokea ushaur wangu hata kama alikuwa anaamin kile alichoamin hvyo bas huyu Mzee tulie nae anaroho mbaya na wa kutaka kusifiwa hata kwa baya sasa wanaoenda kinyume kimawazo yeye lazima awashughulikie bila huruma hata kama wanamawazo chanya!
 
Back
Top Bottom