Mpitagwa
JF-Expert Member
- Feb 10, 2012
- 2,339
- 1,119
WanaJF, nimefuatilia kwa kina jinsi watanzania wa kawaida kwa nafasi yetu kama waajili wa serikali na kugundua kuwa tunafanya uzembe mkubwa wa kusimamia serikali yetu kwa kukubali kubadilishiwa CD kila uchwao. Lakini Mtanzania mwenzetu kipanya yeye amejipambanua tofauti kwa kung'ang'ania hoja ya kwanza na kugoma kusikia CD ifuatayo. Tokea limetokea tatizo la mgao wa umeme yeye aliamua kuwa cartoon zake zote zitakuwa na dack background ikiwa ni alama ya kuwakumbusha viongozi kuwa tunatatizo la umeme bado lipo na umepita zaidi ya mwaka bado analia na giza la mgao wa umeme na sasa mgao unarudi tena. Je watanzania wote tungekomaa kila mtu kwa nafasi yake tatizo la umeme lingefika hapa? Watanzania matatizo yetu ni mengi na hawezi kwisha kwa pamoja au kwa kubadilishawa CD. Sasa hivi ni muda mwafaka kwa wote kukomalia tatizo moja then likitatuliwa ndoo tuhamie lingine. Hongera Kipanya kwa hili na kwa kutukumbushia suala la hatima ya wabunge waliofukuzwa na vyama vyao, na mengine mengi unayotujuza.