Watanzania tunaweza....tuendelee kukaza buti


October

October

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2009
Messages
2,146
Likes
9
Points
135
October

October

JF-Expert Member
Joined Oct 5, 2009
2,146 9 135
Nimefurahishwa sana na jinsi watanzania walivyoamka katika Uchaguzi huu. Hii inadhihirisha jinsi Watanzania walivyochoshwa na miaka 50 ya CCM ambayo haikuwa na manufaa kwa watanzania. Kilichonifurahisha zaidi ni jinsi vijana walivyojitolea kwa moyo wote kulinda kura na kushinikiza matokeo hata pale wachakachuaji walipotaka kuchakachua matokeo.
Watanzania tunaweza kuiweka madarakani serikali tuliyoichagua kama tukiendelea na moyo huu. Watanzania tunaweza komesha wizi wa kura unaoweza kufanya ili kunufaisha CCM. Kama Mwanza, Ubungo Arusha, Shinyanga, Mbeya wameweza shinikiza matokeo kutangazwa, Kwanini sehemu nyingine za Tanzania washindwe kukaza Buti ili matokeo halali yatangazwe?
Kinachoendelea sasa hivi ni psychological warfare (vita ya kisaikolojia). Kuchelewesha matokeo ya Ubungu eli wapate fursa zaidi za kuchakachua kura, Pili Kutangaza matokeo ya Uraisi katika majimbo ambayo ni Obvious kuwa JK angeshinda na kutotangaza yale mengine aliyoshindwa vibaya. Hii ni kuwaandaa watu psychologically ili wayakubali matokeo yanayochakachuliwa.
Watanzania Tusichoke na wala tusirubuniwe nah ii Psychological warfare inayoendeshwa, tuwe macho kwa sababu tukiondoka vituoni tu basi tujue matokeo yatakuwa siyo ridhaa ya wananchi tena.

....Tusidanganyike mpaka Kieleweke......

Tanzania si mali ya CCM, ni yetu sote na wote wana haki ya kuongoza. Kwanini wang'ang'ania hata pale wasipotakiwa
 

Forum statistics

Threads 1,263,855
Members 486,093
Posts 30,166,218