Watanzania tunaweza kujifunza mengi kupitia telenovela/tamthilia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania tunaweza kujifunza mengi kupitia telenovela/tamthilia

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nonino, May 4, 2012.

 1. nonino

  nonino Member

  #1
  May 4, 2012
  Joined: Apr 11, 2012
  Messages: 32
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  watanzania wengi si wapenzi wa kusoma vitabu na magazeti(isipokuwa ya udaku),lakini ni wapenzi wa kuangalia telenovela zinazorushwa katika vituo mbalimbali vya televisheni.Wito wangu kwa vituo vya tv waonyeshe telenovela ambazo ni endelevu zaidi zinazoweza kuchochea mabadiliko kiuchumi,kisiasa nk

  Nakumbuka telenovela LA REVANCHA,iliwahi kurushwa 2005 na tvt kama sijakosea ni moja ya telenovela endelevu ninayozungumzia,ngoja niwapakulie kidogo ;

  LA REVANCHA telenovela,kuna madada wawili,Isabela na Soledad ambaye baba yao aliuwawa na mzee Rodrigo(muuaji,mfanya biashara haramu),baada ya kujua muuaji wa baba yao ni nani;Isabela alisema hatapumzika mpaka amuone Rodrigo yuko jela na ahukumiwe kunyongwa,Soledad ambaye anawawakilisha watanzania wengi alisema adhabu ya Rodrigo kutengwa na familia yake,baada ya wao kufahamu maovu yake inatosha haina aja ya kumpeleka jela ,haina haja ya ahukumiwe kifo,Mungu mwenyewe atamuadhibu.

  Rodrigo ni nani tanzania? ni serikali ya kifisadi,isiyo jali maendeleo ya nchi na wananchi wake isipokuwa kujinufaisha wenyewe.Soledad(watanzania) wanajua kabisa taabu zao zote zinatokana na nani,lakini hawachukui hatua yoyote wanamuachia Mungu.Isabela ametumika kuamsha ari ya mabadiliko,hamna mtu atakayeondoa machungu uliyonayo,zaidi ya wewe mwenyewe kutafuta haki yako.

  Shime jamani ,turushe tamthilia zenye kufundisha na kuburudisha sio zenye kuonyesha mapenzi tu ya kusadikika,na twende hatua moja mbele tuwe kama wenzetu wafaransa,kabla tamthilia haijarushwa wanaielezea maudhui yake,imebeba ujumbe gani,falsafa ya mwandishi je inahitaji parental guide,nk baadaye watu wakija kuiona wanaelewa zaidi ,sio kuangalia mavazi ya waigizaji.
   
 2. D

  Donell Member

  #2
  May 4, 2012
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 50
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  kweli kabisa,mjenga nchi ni mwananchi
   
 3. Mshuza2

  Mshuza2 JF-Expert Member

  #3
  May 4, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 4,119
  Likes Received: 1,749
  Trophy Points: 280
  Hii kitu ungepeleka kule FB ingekua mwaake!
   
Loading...