Watanzania tunauthubutu kama wahindi au wamalawi au tuwe kama thailand?

msambaru

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
245
250
Wanajf, Binafsi nimependezwa na maamuzi waliyofanya wahindi na wamalawi ktk chaguzi nchini mwao, je kwa hamasa na woga tulionao na tunavyotishwa ktk kufanya mageuz twaweza? au tuwe kama Thailand?
 
makubazi

JF-Expert Member
Feb 15, 2013
2,048
1,195
Ooyooo kwa longo longo na domo ndio ushindi na humo humo kuna wasaliti na wanafik tena kuwajua ni tabu na kuwatambua
 
Honolulu

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
5,649
1,225
Watanzania ni ukame wa fikra na njaa zinawasumbua. Ili wapate mang'amuzi ya kweli itahitaji muda na nguvu nyingi.
 
iMad

JF-Expert Member
Aug 4, 2013
1,833
0
Tanzania inasikitisha sana..mm wakati mwingine nasema ccm watafune nchi mpaka watu watembee na funza miguuni ndo labda watabadilika.. watu ka tundu lisu nk wanaacha kazi kwenye mashirika ya kimataifa wanawapigania lkn wapi..kuna shida somewhere
 
Elly B

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
1,194
1,195
Wanajf, Binafsi nimependezwa na maamuzi waliyofanya wahindi na wamalawi ktk chaguzi nchini mwao, je kwa hamasa na woga tulionao na tunavyotishwa ktk kufanya mageuz twaweza? au tuwe kama Thailand?

Tatizo la kwanza la Watanzania ni elimu duni. Elimu duni ya kuwafanya waelewe kuwa hii nchi ni yao na siyo ya watawala. Elimu ya kuwafanya waelewe kuwa watawala wanapata mamlaka na nguvu za kutawala kwa ridhaa ya wananchi wao. Elimu ya kuwafanya wajue kuwa ni jukumu lao kuwasimamia na kuwawajibisha viongozi wao pale wanapokuwa kinyume.

Leo wananchi wengi wanadhani nchi ni mali ya CCM na serikali na wao hawana la kufanya! Leo mwananchi haoni kama kudorora kwa uchumi na maendeleo ni uzembe wa watawala, wanadhani ni fate. Hawajui kama kodi wanazolipa, ambazo tayari ni nyingi, mpaka imekuwa kero, ndizo zinazotakiwa kuleta maendeleo yao. Leo mtu kodi unalipa halafu unaambia barabara, hela hakuna. Na wakati huohuo serikali hiyohiyo inaendelea kuongeza mzigo kwa kuendelea kugawa mikoa na wilaya mpya, huku kukiwa na wizara ambazo hata hazijulikani zinafanya nini!

Wanachi wa aina hii nadhani, mbali ya hamasa wanhitaji elimu ya kuwawezesha kujitambua, Halafu ndiyo lifuate la hamasa. Kwa hali ya sasa, kudhani kunaweza kuwa na hamasa katika elimu duni ni sawa na kungojea mvua mahali pasipo na maji wala miti!
 
Elly B

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
1,194
1,195
Tanzania inasikitisha sana..mm wakati mwingine nasema ccm watafune nchi mpaka watu watembee na funza miguuni ndo labda watabadilika.. watu ka tundu lisu nk wanaacha kazi kwenye mashirika ya kimataifa wanawapigania lkn wapi..kuna shida somewhere

Not somewhere, vichwani, to be specific. Na mpaka shida hiyo itakapoondolewa, tutaendelea na maisha hayahaya ya kijinga. Kwamba serikali inashindwa kutekeleza wajibu, hali ya uchumi inakuwa ngumu, maisha yanapanda mpaka mtu anapata mlo mmoja kwa siku, halafu mtu huyohuyo unamkuta kesho amejifunga kibwebwe na mayunifomu ya chama hichohicho kinachomtia umaskini.

Ndiyo maana naungana na wanoamini kuwa umaskini wa kukosa akili, ni umaskini wa kiwango cha juu kuliko umaskini wowote.
 
Jp Omuga

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
4,094
2,000
Tanzania nchi ya bora liende! Lakini tuseme ukweli ukipata jibu la watu gani ni wengi nchini kati ya walioenda shule wakaelimika na ambao hawajaelimika (pamoja na wengine kwenda shule) utakuwa umelijua tatizo la taifa hili!
Hivi kweli kama ni taifa la watu wenye akili inaingia akili kwa katibu mkuu wa chama tawala kuzunguka nchi nzima huku akikikosoa chama chake na serikali yake hadharani alafu utakuta anapigiwa makofi na kushangiliwa kama shujaa!

Nchii mazuzu wengi! Hawapendi kusoma; hawapendi kujielewesha mambo muhimu wao wenyewe! Wanapenda kusimuliwa simuliwa tu! Hawapendi hoja fikirishi! Wanapenda kuwa kama mapipa ya tàka; kutumika kujaza uchafu tu!
 
mfianchi

JF-Expert Member
Jul 1, 2009
9,727
2,000
Tanzania inasikitisha sana..mm wakati mwingine nasema ccm watafune nchi mpaka watu watembee na funza miguuni ndo labda watabadilika.. watu ka tundu lisu nk wanaacha kazi kwenye mashirika ya kimataifa wanawapigania lkn wapi..kuna shida somewhere

Mkuu bado wengine huko vijijini wanafikiri raisi bado ni Nyerere na wanaamini ni mwiko kukipigia kura ya hapana chama ambacho si cha Nyerere.Pia ukitaka kujua Watanzania wengi tulivyo na akili mgando nafiri uliona wajumbe wa bunge la katiba mambo waliyokuwa wanayafanya,hapo ndio ujue safari yetu ilivyo ndefu.
 
iMad

JF-Expert Member
Aug 4, 2013
1,833
0
Mkuu bado wengine huko vijijini wanafikiri raisi bado ni Nyerere na wanaamini ni mwiko kukipigia kura ya hapana chama ambacho si cha Nyerere.Pia ukitaka kujua Watanzania wengi tulivyo na akili mgando nafiri uliona wajumbe wa bunge la katiba mambo waliyokuwa wanayafanya,hapo ndio ujue safari yetu ilivyo ndefu.
Ni kweli mkuu na sasa kama bunge la katiba ni vile..mtu anakremishwa maneno ya kusema je..mwananchi wa kawaida wapinzani wameimba wee, wamerisk maisha yao wamekoswa na mabomu na risasi wapi..! watu kama kileo kaacha mke na watoto kaenda kuwekwa rumande igunga tabora..lakini wapi..
 
iMad

JF-Expert Member
Aug 4, 2013
1,833
0
Not somewhere, vichwani, to be specific. Na mpaka shida hiyo itakapoondolewa, tutaendelea na maisha hayahaya ya kijinga. Kwamba serikali inashindwa kutekeleza wajibu, hali ya uchumi inakuwa ngumu, maisha yanapanda mpaka mtu anapata mlo mmoja kwa siku, halafu mtu huyohuyo unamkuta kesho amejifunga kibwebwe na mayunifomu ya chama hichohicho kinachomtia umaskini.

Ndiyo maana naungana na wanoamini kuwa umaskini wa kukosa akili, ni umaskini wa kiwango cha juu kuliko umaskini wowote.
Ni kweli mkuu..watu wanasema vijijini nenda mjini hapo mbagala uone watu wanavyopigania mabasi na kusimama kwenye mabasi..lkn anzisha mjadala wa kukichambua chama tawala uone watu wanavyo kuponda.. na mtu mzima na akili zake anakuponda huku kasimama kashika bomba hata kugeuka hawezi.. lkn atakwambia chama kimeleta maendeleo bana..
 
ROBERT MICHAEL

JF-Expert Member
Oct 23, 2012
4,922
2,000
Tanzania kuna watu walio wengi waliokata tamaa ambao wanaohisi umasikini ndio Mungu aliowaumba nao.
 
May 5, 2014
92
0
Ni kweli mkuu..watu wanasema vijijini nenda mjini hapo mbagala uone watu wanavyopigania mabasi na kusimama kwenye mabasi..lkn anzisha mjadala wa kukichambua chama tawala uone watu wanavyo kuponda.. na mtu mzima na akili zake anakuponda huku kasimama kashika bomba hata kugeuka hawezi.. lkn atakwambia chama kimeleta maendeleo bana..

Mkuu umenichekesha sana dah!
 
Malafyale

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
13,020
2,000
Tume ya uchaguzi ya Malawi ipo huru na HAIFUNGAMANI na chama chochote na ndiyo maana jana Mwenyekiti wa Tume Jaji Kimbendera aliwaita waandishi wa habari na kuwaambia bila kumung'unya maneno kuwa madai ya Rais Banda kama uchaguzi una kasoro nyingi HAYANA ukweli wowote na yapuuzwe!

Jaji Lubuva akisema hivyo kwa Rais JK anafutwa kazi usiku huo huo!Watendaji wa Tume wakiwa huru ndiyo sauti ya watz kupitia sanduku la kura itaonekana!
 
WENYELE

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,291
2,000
Wanajf, Binafsi nimependezwa na maamuzi waliyofanya wahindi na wamalawi ktk chaguzi nchini mwao, je kwa hamasa na woga tulionao na tunavyotishwa ktk kufanya mageuz twaweza? au tuwe kama Thailand?

Je,unazijua sera za wapinzani waliopita India na Malawi?
Je na wao walukua wanatembelea Chopa na kupigana Matofari? Na wao walifukuzana kwa usaliti? Je na wao walikua wanafanya Maandamo na kusababisha vurugu?
 
Kichoi

JF-Expert Member
Apr 13, 2014
212
195
Watanzania nahiai tumelaaniwa! Kama hatuja laaniwa tumelishwa sumu, tumepumbazwa.
Watanzania tunadharau mambo madogo madogo ambayo madhara yake ni makubwa. Wahenga walisema Mdharau Mwiba.... Mtamalizia.
Tumeshiudia chaguzi nyingi zikifanyika, tumejiuliza?
Baadhi ya wanunge wetu wamejitahidi kutufungua akili je! Tumefunguka?
Nchi sasa imekuwa Mali ya ccm, watz tuko wapi? Kwa nini tumeacha haya yote yatokee?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom