Watanzania tunathamini umuhimu wa Serikali na tuko imara kuilinda: Rais tunaomba utuongezee nguvu

Criterion

JF-Expert Member
Jan 8, 2008
11,798
11,881
Watanzania tulio wengi, hatuna uraia pacha, na tunajua hapa ndipo nyumbani kwetu, japo tunaweza kwenda matembezini lakini mwisho wa siku hapa ndipo kwetu. Kwa mantiki hiyo, kiu yetu ni kuhakikisha nyumbani kwetu panadumu kuwa mahala safi na salama kwa ustawi wetu na vizazi vyetu vijavyo.

Tunajua maisha ya ukimbizini ni utumwa na kukosa makao ni laana. Kwa msingi huo japo tuna viwango tofauti vya uelewa, mitazamo na itikadi, lakini sisi kwa pamoja tuko imara kuilinda serikali na nchi yetu kwa kutokuruhusu, migawanyiko, vurugu ama njama za kiharifu za aina yoyote kutamalaki katika taifa letu.

Katiba ya JMT, imekupa mamlaka ya kuwa Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amir Jeshi Mkuu, kwa maana ya kwamba kila kitu katika nchi hii hiko chini yako isipokuwa Sheria (Sura ya Pili ya katiba, Sehemu ya kwanza Ibala ya 33 - 46b).

Kwa nafasi uliyonayo, wewe ndiye mwenye uwezo wa kutuongoza na kutupa nguvu ya kusimamia na kutekeleza azma za kujenga taifa lenye mtangamano. Hali iliyopo kwa sasa ni dhahiri haiaksi manukato ya ushindi wa vita tunayopambana nayo dhidi ya ujinga, umaskini, maradhi, rushwa na ubinafsi.

Lakini wahenga walisema umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu. Mheshimiwa raisi, pamoja na yote naomba utambue kwamba kuna jeshi kubwa liko nyuma yako, lenye utayari wa kupambana na maadui hao niliowataja hapo juu, na kinachotakiwa ni wewe kutuunganisha na kutuogonza katika mapambano. Hauko peke yako Rais wetu.

Pamoja na hayo, kwanza naomba utusaidie kuturejeshea ari kwa kujua kwamba na sisi tunathaminiwa na kujaliwa utu wetu kwa kujali hali na changamoto tulizonazo ambazo zinavunja mioyo watu na kujiona ni watu duni katika jamii yao.

Pili jipambanue kwamba uko na sisi katika vita hivi, na kwamba tutakuwa salama bila kutelekezwa wala kusalitiwa katikati ya mapigano. Tatu Jikite katika kuunganisha taifa, badala ya kustawisha makundi na migawanyiko inayojeruhi watu kwa sababu hii inaasisi unrest, kama si leo basi kesho.

Kwa kukumbusha tu, naomba Mheshimiwa rais, jipambanue uko na sisi kwa kulinda na kutetea katiba ya Jamhuri ya MUUngano ambayo uliapa kuilinda.

1. Unajua kuna watu 19 wanaohudhuria vikao vya bunge kwa gharama zetu ambao ama
a) Si wabunge wa kuchaguliwa na wananchi.
b) Si wabunge kutoka barala za wawakilishi Zanzibar,
c) Si wabunge wa kuteuliwa na Rais.
d) Si wanasheria wakuu wa Serikali wala si Speakers wa bunge.

Kwa muktadha wa sheria za JMT, uwepo wa wabunge hawa ni kinyume na katiba ambayo Mheshimiwa rais umeapa kuilinda. Ili tuendelee kupigana vita hivi pamoja, tukiamini Mh. Rais uko na sisi, tunaomba suala la wabunge wasio na vyama bungeni, lishughulikiwe ili kutujengea imani wananchi juu ya usafi na umakini wa Serikali yetu.

Yako malalamiko mengi sana juu ya utendaji kazi wa jeshi la polisi ambayo kama hayatashughulikiwa yanaweza kuzaa madhara katika jamii. kuna makala nyingi zinatoka zinazoangazia uharifu wa kibinadamu unaofanywa na jeshi la polisi ambao unaashiria uwepo wa mfumo dhurma ambao haujengi umoja wa kitaifa. Kwa hali ilivyo sasa bila mkakati wa kufumua jeshi hili, hatma ya taifa itakuwa mikononi mwa wenye nguvu.

Kuna mifano mengi ya utendaji wa jeshi hili ambao hauashirii ustawi wa taifa. Mfano kubambikiziwa kwa kesi, udanganyifu, n.k. Yote haya ni dhurma za haki za binadamu na bila tiba, sumu hiii italitafuna taifa.

Mheshimiwa rais, wewe ni shahidi namna ambayo chmbo cha kutoa haki (TAKUKURU), vile kimeshindwa kuchukua hatua za waharifu walioandikwa kwenye report ya CAG, hadi umewalazimisha wachukue hatua. Hii inatosha kukuonyesha ni namna gani chombo hiki kinahitaji kufumuliwa kabisa. Kama kinashindwa kuchukua hatua za kutekeleza uchunguzi uliofanywa na CAG, utaamini vipi kwamb taarifa za chunguzi wanazofanya wao hazinawa comromised? Unaondoaje picha ya mashaka kwa haki za wanyonge wasiojulikana na CAG, wanapeleka malalamiko kule wakitegemea kupata haki? Utaamini namna gani hata kwa amuri yako, kwamba watasimamia kesi kwa weledi kama tayari wameshatake sides za watuhumiwa?

Waziri Mkuu aligundua wizi wa mabilioni ya fedha hazina kwa malipo hewa. Lakini hatukusikia hatua yoyote imechukuliwa. Lakin iwizara hiyo hiyo inaendelea business as usual huku wakichukua maamuzi mengi mabovu ya kuumiza wananchi pasipo kujali.

Itatia moyo angalau tukijua kwamba ni halali kwa fedha za umma kulipwa kwa vocha za malipo kwa MKT, DSO, SKN, bila hata narration ya kazi wanazyofanya mwenye hivyo vijina. Pengine itabidi tujifunze pattern mpya ya kufanya malipo ya kazi maalumu, ambazo haziko kwenye malipo yake ya mishahara, na authorizing officers wakaridhia, na check zikatoka kwa hizo initials. Labda tufahamu kama hiyo ni system ya Idara zote za Serikail ama ni wizara ya fedha tu. Kwa vyoyote vile, inakatisha tamaa sana kuona serikali inalinda wizi, na kutokuwachukulia hatua wezi hao wakati ikilalamika haina hela na kulazimiska hata kushindwa kulipa malipo halali ya watu maskini. Kwa kuanzia Mheshimiwa unda tume maalumu ya watu kutoka nje ya wizara za Serikali ifanye uchunguzi juu ya ubadhirifu wa namna hii ili kurejesha imani ya Wananchi juu ya utunzwaji na matumizi ya raslimali za umma.

La mwisho nakuomba Rais wetu, jiepushe na malumbano yanayoanzishwa ili kukuchukulia muda na kukuondoa kwenye reli. Pata watu sahihi wasiokuwa wanafiki, wasio wezi, wenye uchungu na taifa wakusaidie kuchapa kazi kazi iendelee. Tuko pamoja na wewe.
Kwa leo naomba niishie hapa.

Ninapoishia, hapa ,iwapo kuna mwingine mwenye ushauri kwa rais wetu, anaweza kuweka hapa. Angalizo, naomba michango yenye staha.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom