Watanzania tunatakiwa kuwatembelea watoto yatima na kuwafariji

buffaro89

JF-Expert Member
Jul 12, 2016
592
378
Habari wakuu,

Ninamshukuru Mungu kwa kunipa kibali cha kuona siku nyingine kama hivi leo.
Binafsi napenda tusisitizane katika kuendeleza upendo, amani na umoja, kama ilivyo kwa Mungu wetu mwenye upendo, amani na yeye ni mmoja kuna jamii, inatuzunguka ya watoto wasio jiweza na waliofiwa na wazazi wao, watoto yatima.

Sisi kama watanzania, ni vizuri kuwatembelea na hata kuwapelekea chochote maana, hakuna msaada mwingine wanaweza kuupata zaidi ya watu na jamii kwa ujumla. Unapo fanya hayo, Mungu anakuona, na huwezi kupata mikosi na mabaraha! Maana wewe una asili ya kimungu kama alivyo Mungu mwenye upendo na huruma.

Yawezekana ni mtaani kwenu au pengine popote pale, kuna watoto hawa wenye hari ngumu, piga moyo konde, mchukuwe hata mmoja, mtunze kama mwanao, hakika nakwambia kweli, Mungu atakubariki na hata ukifa, utahesabiwa haki.

Watanzania, tuache kulea michepuko na kuipangishia nyumba, tuache kuwapelekea fedha makahaba na wanawake wasio na future, fedha hizo, tuzielekeze kwa hawa watoto, na wao wapate haki zao za msingi, ili kutimiza ndoto zao, na ionekane maana ya sisi kuishi duniani.

Ni hayo tu wakuu! Tuzitafute baraka sio mikosi na mabaraha!
 
tz}ccm.gif

Kidumu chama cha mapinduzi!!
 
Back
Top Bottom