Watanzania tunataka nchi gani? Bila kujibu hili swali kamwe hatutafanikiwa!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania tunataka nchi gani? Bila kujibu hili swali kamwe hatutafanikiwa!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kamundu, Aug 15, 2012.

 1. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #1
  Aug 15, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Watanzania tumechukua utamaduni wa waingereza wa kupenda kulalamikia kila kitu. Mara nyingi tunapenda kutumia maneno kama wao, wale kuimanisha sio mimi. Ukweli ni kwamba nchi hazibadilishwi na viongozi pekee bali wanannchi ndiyo wanaotaka maendeleo na viongozi wazuri wanafuata matakwa ya wananchi. Ni lazima Tanzania tujibu maswali yafuatayo kama kweli tunataka mabadiliko. Je ni nchi gani tunaitaka?

  1. Mfumo kama wa Marekani: Mfumo wa Marekani ni kwamba serikali kwenye katiba inatakiwa kufanya vitu tu ambavyo watu hawawezi kufanya wenyewe!. Jeshi, Barabara, mifumo tu kwenye elimu, Afya, kodi, madeni ya nchi,uhamiaji, usalama wa anga,usalama wa airports, polisi, Fire, uangalizi wa maji safi, hewa safi na kutoa vibali vya hifadhi za uchimbaji wa mafuta na kulinda hifathi za wanyama vilevile wana mahakama huru. Serikali ni ya vyama vingi na kuna ushindani wa haki. Serikali haijihusishi kwenye biashara. Kwenye Mfumo huu huwezi kusingizia au kutegemea serikali ifanye kila kitu na huwezi kulalamikia serikali kwenye kila kitu

  2. Mfumo wa China: Serikali ndiyo inatoa madaraka yote na ni mfumo wa chama kimoja. Uhuru wa habari unachujwa na serikali inafanya biashara kama kampuni za ujenzi, usafirishaji, ndege, banks, shule, hospitali, ni za serikali. serikali inajihusisha na ulinzi wa nchi, mahakama. Kwenye mfumo huu faida zake ni kwamba utekelezaji wa agenda ni mrahisi lakini kama agenda na viongozi ni wa zuri. Kama agenda na viongozi ni wa baya wananchi hawana jinsi ya kuwabadilisha viongozi kwasababu hakuna demokrasia ya vyama vingi. Hakuna demokrasia ya huru ya vyombo vya habari. Mfumo huu kama tunautaka inabidi tuwape uwezo serikali na sisi wananchi tufuate wanachofanya na kuwaamini kwamba wanachofanya ni sahii na ni kwa manufaa ya nchi. China haina mchanganyiko wa utamaduni kama Tanzania hivyo inaweza ikawa ngumu na vilevile tunapenda sana demokrasia. hivyo mimi sijui kwenye hii system kama itawezekana au la

  3. Mfumo wa Rwanda: Mfumo wa Rwanda unafanana na wa China lakini tofauti ni kwamba China nguvu iko kwenye chama na Rwanda nguvu iko kwenye uraisi wa nchi. Hatuwezi kuwa na mfumo huu na kuwa na demokrasia wakati huohuo! hatuwezi kutaka na kupata vyote!. Huu mfumo ni kwa raisi kama una raisi mzuri nchi inaweza kwenda kwa kasi lakini kama unaraisi mbaya nchi inaweza kwenda chini kirahisi.

  Mimi kwa mawazo yangu Watanzania tunajichanganya tunataka demokrasia ya Marekani lakini mfumo wa China na hii haitawezekana. Je Watanzania wenzangu ni lazima tufanye uamuzi na kama unamawazo ya system nyingine tueleze.
   
 2. mooduke

  mooduke JF-Expert Member

  #2
  Aug 15, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 619
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Hili ndilo ambalo watanzania hawalijui na wana kalia kupigakelele na hawajui wanacho hitaji hasa hapokwenye nyekundu
   
 3. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #3
  Dec 18, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Nashangazwa sana na Tanzania maana wanasiasa ambao ndiyo watu wanaotakiwa kujua na kujadili policy za nchi kama hizi wanakimbia hizi topic kwasababu niwatupu!! hata kama hujui huwezi kujifunza bila kujaribu. Nawashauri hasa wanasiasa kusoma topic hii muhimu na kutuambia watafanya nini au mawazo yao ni yapi. Kupigana madongo kwa nyama vya siasa hakutoshi.
   
 4. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #4
  Feb 16, 2013
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Bado hakuna jibu!!!??
   
 5. m

  musa ndile Senior Member

  #5
  Feb 16, 2013
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 105
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  pole sana nadhani wengi tumekudharau ndo maana hatuwezi hata kukupa majibu una elimu gani kijana baada ya udhaifu mkubwa wa ccm leo unaleta hilo pole sana mjomba
   
Loading...