Watanzania Tunashukuru Mungu kwa kutupa Rais Samia, yule Baba angetutoa roho

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
Salaam Wakuu,

Pamoja na mapungufu ya mambo ya vyama vya Siasa na Malalamiko ya Demokrasia, safari hii nafuu kuliko wakati ulopita.

Rais Samia anaiongoza Tanzania. Na hatoki kwani bado anautamani Urais na ziara za hapa na pale.

Watu wanaojipanga kumtoa kwenye kiti chake kwa karatasi, msitegemee atawaletea uji kwenye kijiko cha dhahabu, Munatakiwa Mjipange kiakili ikibidi ombeni msaada nje ya Nchi, ongea na Waasisi wa Nchi hii ili wawasaidie kumshawishi matakwa yenu.

Vinginevyo mtaishia kupiga kelele. Kikwete aliwahi kusema, Kelele za Mlango, hazimzuii mwenye nyumba kulala.

Kwa Upande wangu Namshukuru Mungu kwa kutoondolea balaa, Janga na jitu lisilofungwa Kengele.

Asingekuwa Mungu, yule Baba angetutoa roho.

Thread hii nimeiandika kichwani Mwangu nikiwa Mifereji ya damu inayotiririka ya Watanzania Ben Saanane, Alfonce Mawazo na Wengine wengi.

Zama za majizi za kuchukua pesa kwenye akaunti za beni za Wavuja jasho kisha kuwafungulia kesi za uhujumu uchumi na kuwataka waombe msamaha, imekwenda na maji. Sasa akaunti unaacha hela kesho asubuhi ukiamka unaikuta salama.

Mungu ni mwema
 
Kwahilo hata mimi namshukuru mungu. Kwanza gaidi kawekwa ndani.

Pili wale waliojifanya wakimbizi wa kisiasa wakae hukohuko wasije kabisa wasije wakaambikizwa ugaidi na mkubwa wao
 
Hizi chuki kwa Magufuli kama zingeelekezwa chuki kama hizi kwa ccm basi nafikiri Mungu angekuwa amefanya jambo na ccm ingekuwa historia tungekuwa tunamshukuru huyo Mungu sasa hivi.
 
Hizi chuki kwa Magufuli kama zingeelekezwa chuki kama hizi kwa ccm basi nafikiri angekuwa amefanya jambo na ccm ingekuwa historia tungekuwa tunamshukuru huyo Mungu sasa hivi.
Najua Mtanikumbuka Siyo Kwa Mabaya Lakini Mazuri
 
Salaam Wakuu, Kwa Upande wangu Namshukuru Mungu kwa kutoondolea balaa, Janga na jitu lisilofungwa Kengele. Asingekuwa Mungu, yule Baba angetutoa roho. Mungu ni mwema
Hivi hatuwezi kumsifu rais Samia bila kumponda JPM?. Jee wajua hata JPM ulikuwa ni mpango wa Mungu kwa Tanzania?. Jee wajua ni sisi Watanzania wenyewe ndio tulimlilia Mungu atuletee mtu kama JPM?.




P
 
Back
Top Bottom