Watanzania tunapitia kipindi kigumu kiuchumi kuwahi kutokea

Mpinzire

JF-Expert Member
Jan 18, 2013
7,200
12,890
Binafsi kwa upande wangu na wanaonizinguka wote hali mbaya zaidi kiuchumi! Hakuna biashara yani full mdororo ila ndiyo kwanza naona EWURA wanapandisha bei za mafuta na mitungi ya Gas nayo inapenda bei huku hali za kibiashara zikiendelea kudorola kabisa kabisa.

Unaweza sema Hayati aliharibu uchumi lakini si kama sasa aisee! Hayati alitumianisha kuwa wavumilivu cos alikuwa na miradi mikubwa ambayo ingekuja kusaidia hapo mbele tuishi maisha mazuri, kabla hajatufikisha huko alikokuona Mungu akamuita sasa katuachia Samia lakini Samia amekuja kwa kukamua zaidi watu wa chini!

Katika uhalisia walikuwa wanajua bei ya mafuta katika soko la Dunia itapanda, lakini ajabu na wao ndiyo wakaongeza tozo! Sasa kila mwezi mafuta yatakuwa yanapanda tu, mbali na ilo akaona aweke na makato katika miamala yetu yani ile VAT akaona haitoshi na tozo ni lazima kama kodi tu lakini hana habari.

Sijui kama tunakokwenda ni kuzuri kwakweli.
 
Sasa hiyo miradi imekwisha?!!

Nani wa kuimaliza baada ya kuanzishwa?

Mh.Rais SSH amekataza TASK FORCES za kukusanya Kodi kwa NGUVU...je leo zile BUREAU DE CHANGES zilizokuwa zimefungwa hazijaanza KUFUNGULIWA?!!

Mh.Rais amewafutia TOZO ya 6% wanufaika wa mikopo kutoka HESLB....je hii si nafuu kwao ?!!!
 
Mipango INAENDELEA.....

Mh.Rais ametuelezea malengo ya TOZO kuwa itarudi kwa wananchi kwa kuzijenga barabara za vijijini ili ziwe TIJA NA NAFUU kwa wakulima.....je hili si sawa na mipango ya JPM kutokuajiri vijana na kututia moyo kuwa anajenga kwanza SGR na BWAWA LA MWALIMU NYERERE?!!!

Mh.SSH aliinadi ilani ya miaka 5 ambayo bado ipo na anatembelea JUU YAKE.....Kumlaumu kwa muda huu mfupi ni kumuonea tu.....

#KaziIendelee
#SiempreSSH
 
Sasa hiyo miradi imekwisha?!!

Nani wa kuimaliza baada ya kuanzishwa?!!

Mh.Rais SSH amekataza TASK FORCES za kukusanya Kodi kwa NGUVU...je leo zile BUREAU DE CHANGES zilizokuwa zimefungwa hazijaanza KUFUNGULIWA?!!

Mh.Rais amewafutia TOZO ya 6% wanufaika wa mikopo kutoka HESLB....je hii si nafuu kwao ?!!!
Unafuu wake unakuja wapi wakati hawajapata ajira bado!? Ajira zimekuwa ngumu sana ata watoe mkopo bure haisaidii kitu
 
Mipango INAENDELEA.....

Mh.Rais ametuelezea malengo ya TOZO kuwa itarudi kwa wananchi kwa kuzijenga barabara za vijijini ili ziwe TIJA NA NAFUU kwa wakulima.....je hili si sawa na mipango ya JPM kutokuajiri vijana na kututia moyo kuwa anajenga kwanza SGR na BWAWA LA MWALIMU NYERERE?!!!

Mh.SSH aliinadi ilani ya miaka 5 ambayo bado ipo na anatembelea JUU YAKE.....Kumlaumu kwa muda huu mfupi ni kumuonea tu.....

#KaziIendelee
#SiempreSSH
Tozo zinatoka kwa wananchi ambao kipato chao hakijaongezeka kwa mda mrefu! W.kazo wa umma kwa zaidi ya miaka 6, w.kaz wa private hali mbaya na ajira hamna kitu mda mrefu. Yeye raisi anatoa wapi ujasiri wa kuongeza tozo hizo? Na watu wanacompensate wapi hela wanayopoteza!? Naomba uache kiherehere cha kutetea ujinga ww wa kula na kulala. Hali ni ngumu na ni heri wakachukue mkopo watuache na deni tu kuliko kutukwapua kidogo tulichonacho!!! Bladifakeni ww
 
Back
Top Bottom