Watanzania tunapaswa kuambiwa na kujua ukweli kwamba Gesi inayochimbwa Mtwara si yetu

Sio lazima ulete siasa chonganishi unaweza kutuwekea hapa yaliyokuwa mapendekezo ya kambi ya upinzani juu ya uvunwaji wa gesi yetu na namna yatakavyotekelezwa ili kuleta faida nchini. Nchi ni yetu wote sio kwamba wapinzani ndio wenye akili kuliko wengine hapana hata wao nibinadamu wanakosea. Acha siasa leta mawazo yako mwenyewe hili nijukwaa watu wanaweza kujifunza na kuhamasika
Sioni hata sababu ya kuyaweka hapa coz hamkuwasikiliza Sasa hivi itasaidia nn. Ukisema niache Siasa hv huko bungeni tunaingia wananchi wote? Lazima ujue wananchi wanaweza kuwa na mawazo mazuri sana ila yasiwe na nguvu kwa sababu wapo wawakilishi wenye nguvu kubwa ya kupitisha mikataba ya maendeleo kuliko mm mwananchi. Nachoshauri wananchi tuwe nyuma ya wale wabunge wanaotoa maoni sahihi kuhusu Jambo Fulani na ikiwezekana tukosoe siriaz pale tunapoona mikata ya kijinga inapitishwa na wenye nchi.
 
Mkuu Kishina cha Mshahara, Salary Slip , humu duniani hakuna kitu kizuri kama ukweli, the truth, na ukiwa mkweli mno sometimes, there is a price to pay!. Mimi ni kada wa CCM, ila ni miongoni mwa makada wachache ambao ni makada contemporary toka kundi la ma lumpen proletarians wakati CCM kama chama kimeshikwa, na kundi la ma bourgeoisies ambao ndio huamua kila kitu kwa ajili yetu. Japo ukweli huu ni mchungu ndio ukweli wenyewe, CCM ndio kila kitu!, CCM ndio Tanzania!, bila CCM hakuna Tanzania!. Nakuomba na wewe kuwa tuu mkweli toka ndani ya nafsi yako kwa ukweli kabisa wa dhati ya moyo wako, kuwa ni kweli CCM ndio imetufikisha hapa, lakini kwa vyama vilivyopo, hivi hivi vilivyo, kuna chama gani credible cha kuikabidhi ikulu yetu?. Nakuhakikishia, hakuna!. Sasa kama kilichopo ni CCM only na hakuna kingine, then what?. Jibu ni CCM only!. Kubali, kataa!.
P

Huu ni Ukweli Mchungu labda ndio maana watu wanahangaika kutafuta mbadala!
Ingawa bado hakuna Mbadala!
Umeeleza Vyema Mnooo
Labda Itokee miujiza Huko Mbele ndio Pascal Mayalla anaweza amua vinginevyo...
Lakini kwa hali ya sasa Ameeleza kila kitu!
 
Kuna vitu eidha unachanganya ama unaandika kishabiki.

1. Nisaidie kujua hao artmas walikua wanazalisha umeme kisha wanaupeleka wapi na plant ya kuzalisha umeme ilikua imejengwa wapi?

Kwa kumbukumbu zangu kampuni iliyosaini HGA ni Wentworth mwaka 2004. Kampuni hiyo ikauza hisa zake 51% kwa M&P mwaka 2009 ila hadi kufikia 2015 M&P walikua na 60% na hao Wentworth wakiwa na 40% za exploration ownership ya Mnazi Bay.

Kwa kumbukumbu zangu pia ni kwamba Wentworth anamiliki 31% shares, M&P 48% na TPDC anamiliki 20% ya operations.

Kuna tofauti kati ya exploration ownership na operations ownership.

2. Unalinganisha vitu 2 tofauti, kwamba nani atabeba gharama za bwawa. Ukatolea mfano daraja la kigamboni.

Daraja la kigamboni limejengwa kwa hela za wafanyakazi waliokua wanachangia hela zao NSSF hivyo zile hela sio za nchi, ni za wafanyakazi hivyo lazima zilipaswa kurudishwa. Bwawa la Nyerere linajengwa kwa kodi za wananchi walipa kodi, hizo serikali ina mamlaka ya kuzitumia itakavyo kwa maslahi ya watu wote ama ya nchi.

Hivyo gharama za bwawa tayari zinabebwa na wananchi wote sio kama hela za NSSF hizo ni za wafanyakazi wamekatwa kwenye mishahara yao na sio kodi ile.

Kuna mambo umeandika kishabiki hadi inatia shaka jinsi unavyofikiri. Huoni faida ya bwawa zaidi ya umeme, ila husemi ni umeme wa bei nafuu, umeme wa maji Duniani kote ndio wa bei nafuu kuliko kitu chochote, sasa wewe huelewi kwamba kukiwa na umeme wa kutosha na wa bei nafuu kutasisimua sekta nyingine za uchumi?

Hilo la kwanza, bwana wa mtera lilijengwa anablengo lake ilikua kudhibiti mafuriko ndio baadae ikaja wazo la kuweka ama kuzalisha umeme, je toka Mtera imejengwa umewahi kusikia mafuriko hilo eneo?

Kwa msingi huo bwana la Nyerere litasaidia kuzuia mafuriko kama yale yaliyotokea mwaka jana huko Rufiji, huoni hii kama ni faida, wewe unaona umeme tu?

Ukiachia kudhibiti mafuriko, kuna uvuvi, utalii, kilimo cha umwagiliaji kwani kunakua na uhakika wa maji ya kutosha maeneo ya jirani, hilo huoni kama ni faida, wewe faida unayoiona ni umeme tu.

Jambo la tatu ni kwamba bwana linategemea kuwepo zaidi ya miaka 50 ijayo, hiyo gesi unayoisema ikianza kuchimbwa kwenye large scale haiwezi kuwepo zaidi ya miaka 20, itaisha ila maji hayaishi Duniani.

Kudos Kaka...
Uneelezea kitaalam sana
Umempa na Multiplier effects ya bwawa kusisimua sector nyingine kiuchumi!
Kifuoi Kwenye Gas kuna Watu wachache watafaidika Kielimu zao za gas na wengine Kupiga,Ila Kwenye Bwawa la maji watafaidika watanzania wengi,Kitu ambacho wachache wataumia sababu hawatafaidika Over.
 
Hii yote kikwete kama alivyotufanya ktk escraw na nyinginezo!
Mikataba hii ya gas ilipitishwa kwa hati ya dharura na bunge letu dhaifu sana kupindukia.
Unapokuwa na chombo dhaifu na goigoi cha kutunga sheria haya ndio matokeo yake.
 
Shida ni elimu yetu ya sayansi na teknolojia ni ndogo au ya kukopi au hatuna wataakanu competent katika nyanja nyingi na hatuna UZALENDO toka kwa viongozi hadi sisi wananchi wa kawaida.

Ngoja nikupe mfano hai; hivi sisi kama nchi hatuwezi kuwa na kampuni ya ujenzi inayoweza kutandika mataruma ya reli ya SGR??----- tufanye hatuna hayo makampuni, basi je ilishindikanaje hiyo kampuni inayojenga SGR kupewa Contract ya kujenga kutoka Dar hadi tuseme Moro tu ambapo katika umbali huo Makampuni yetu au wataalamu wetu wa ndani waweze kujifunza namna ya utandikaji ili utandikaji kutoka Moro--- Mwanza---Kigoma tufanye sisi wenyewe!!! , lazima kutakuwa na changamoto, mfano ujenzi wa madaraja na mahandaki, kazi hizo tuna subcontract.

Kifupi ni kwamba Ubinafsi na ujinga vimetuandama mno sisi Waafrika na ndio maana Wazungu wana take advantage.

Its orchestrated na viongozi wetu wenyewe,...anae hujumu mwafrika ni mwafrika mwenzie, hamna mtu mwingine, wewe umejiuliza hilo swali, mimi nakupa swali gumu zaidi, kwann waafrika tunaishi maisha ya ajabu sana despite miaka 60 ya uhuru? Bado zaidi ya asilimia 70 ya watu wanaishi umasikini wa kutisha sana, nyumba za ajabu, maji ya shida, miji yetu haijapangwa, elimu duni that will never transform us or our mindset, uharibifu wa mazingira, etc, just ask yourself why?

Mungu ametupa resources nyingi sana, zimetusaidia nini? Zaidi sana viongozi wanaingia mikataba ya kuumiza vizazi na vizazi kikubwa wao wamepata 10%, kila bara duniani wamefanya progresses kubwa sana, waarabu, asians, etc except ngozi nyeusi tunahangaika na matatizo yale yale!!!!!! dhahabu, gas, ardhi, na resources zitakazo patikana in future hazitatukomboa. Ndio nature yetu, ni ngumu sana kupata viongozi wanaumia kuona vijana hawana kazi, watu mamillion wnaishi nyumba za tope, it doesnt bother them, political position kwao ni jackpot kutajirika. Ila mimi nasema tu Ole wao, sababu hawa masikini wanavyohaingaika na kufa maisha ya shida wakati Mungu aliweka resources hapa ziwasaidie, Ole wao, sababu kila nafsi pumzi itamtoka na hukumu inatusubiri, machozi ya hawa watu hayatapita bure.

after all, miaka 50 au 100 ijayo nani atakuwepo???, kiburi chao na kujiona wao wanafaa sana kuliko hawa masikini kitakuwa wapi? lakini hukumu ya Mungu haitawaacha, kila dawa feki au pesa ya kununua dawa unayokula, masikini anakufa kwa kukosa huduma hiyo damu inakusubiri. Furahi leo una madaraka lakini adhabu ya kaburi haitakuacha.
 
Uko sawa, ila tusisubiri kaburi, wezi ni familia chache watu wachache kama millioni moja hadi tatu. Waliobaki ni wananchi maskini. Tukiamua tunawajibisha. Watanzania kwa hulka zao ni watu wanaopenda amani na kuwasikiliza viongozi wao. Ila sio waoga Harakati za ukombozi kusini, barani Afrika, vita vya Uganda, mchango, ujasiri wa Mtanzania unaonekana.

Tatizo ni systems (mifumo) yetu zinatupa viongozi dhaifu sana. Suluhisho ni kubadilisha mifumo yetu, katiba mpya.

Si vigumu kufanya hivyo wote tusipoenda kazini wiki moja tu serikali inaanguka, sit down protest, maandamano ya amani nchi nzima. Tatizo la maandamano huwa yanaingiliwa na serikali na wahalifu.
 
Hii yote kikwete kama alivyotufanya ktk escraw na nyinginezo!
Mikataba hii ya gas ilipitishwa kwa hati ya dharura na bunge letu dhaifu sana kupindukia.
Unapokuwa na chombo dhaifu na goigoi cha kutunga sheria haya ndio matokeo yake.

Tubadilishe hivi vyombo vyetu vitavyotunga sheria, kupitia mikataba, kuiwajibisha serikali, kwa kuwa na Katiba mpya. Kuwe na uwazi, ukweli, maoni ya wananchi yazingatiwe.
 
Uko sawa, ila tusisubiri kaburi, wezi ni familia chache watu wachache kama millioni moja hadi tatu. Waliobaki ni wananchi maskini. Tukiamua tunawajibisha. Watanzania kwa hulka zao ni watu wanaopenda amani na kuwasikiliza viongozi wao. Ila sio waoga Harakati za ukombozi kusini, barani Afrika, vita vya Uganda, mchango, ujasiri wa Mtanzania unaonekana.

Tatizo ni systems (mifumo) yetu zinatupa viongozi dhaifu sana. Suluhisho ni kubadilisha mifumo yetu, katiba mpya.

Si vigumu kufanya hivyo wote tusipoenda kazini wiki moja tu serikali inaanguka, sit down protest, maandamano ya amani nchi nzima. Tatizo la maandamano huwa yanaingiliwa na serikali na wahalifu.
Inatakiwa watanzania wenye akili kama yako wawe wengi....wafike asilimia angalau 50 esp mijini. Na kuhusu mifumo inatoa viongozi dhaifu upo sahihi 100%
 
Inatakiwa watanzania wenye akili kama yako wawe wengi....wafike asilimia angalau 50 esp mijini. Na kuhusu mifumo inatoa viongozi dhaifu upo sahihi 100%

Upo vizuri kwenye uwezo wa kufikiri. Watafikia hiyo critical point baada ya rushwa, uhuni, unanijua mimi ni nani, ujambazi, wizi kushamiri kila sehemu.
 
Mkuu Hakimu Mfawidhi , hili la gesi wewe ndio umelijua leo?.
Hali hiyo ilikuwa zamani, lakini sasa tuna sheria mpya ya madini na extractive industry yoyote, kila kinachopatikana, asilimia 16% ni mali ya Watanzania. Yaani serikali yetu ina own 16% ya migodi yote, hivyo japo ni kweli kila kinachovunwa ni mali ya mmiliki, hivyo Watanzania ni wamiliki wa hiyo 16% ya free carried shares kwenue rasilimali zote za extractive industry.
P
Kwa maana hiyo ule usemi wa Nyerere kuitwa Mazuzu huko pale pale
Bora TPDC imekuwa Machinga maana imekosa umachknow.
 
Kuna mambo bado hayajawekwa sawa na yakaeleweka vyema.

Gesi inayochimbwa Mtwara sio ya watanzania, ile gesi ni ya makampuni ya kigeni na sio ya Watanzania.

Ieleweke pia kwamba Gesi ile iko 18% nchi kavu na 82% majini ama baharini kwenye kina kirefu.

Ieleweke zaidi kwamba shirika la mafuta na petroli la Taifa ama TPDC wao ni watu wa kati kati ama middle man wa gesi inayozalisha umeme Tanzania.

TPDC wao wananunua gesi kutoka kwa makampuni ya kigeni yanayochimba gesi na kisha kuiuzia TANESCO, yaani makampuni yanachimba, yanapiga gharama za uchimbaji na faida yake, yanaiuzia TPDC, kisha TPDC anaweka cha juu na yeye anaiuzia TANESCO halafu TANESCO anazalisha umeme anauzia wananchi.

Kwa kiswahili chepesi ni kwamba, kwenye gesi ya mtwara TPDC ni dalali ama machinga wa gesi, yeye mwenyewe hana gesi ila kutokana na sheria za nchi, ana umiliki kidogo wa hisa kwenye hayo makampuni yanayochimba gesi. Serikali ama TPDC hawana kisima hata kimoja cha gesi, wao pia wananunua.

Hivyo basi ifahamike kwamba umeme wa gesi hautakuja kua bei Rahisi Tanzania kwa sababu gesi ina madalali ama inapitia mikono mingi na kila wakala ama dalali anaweka cha juu hadi kumfikia TANESCO na tanesco kuwafikishia walaji ambao ni wanachi.

Hivyo ifahamike zaidi kwamba gesi iliyoko kusini 90% ilishauzwa na wamakonde wakae wakijua hawana gesi pale, sio yao ni ya makampuni ya kigeni.

Na hao unaosikia wanasema uanzishwaji wa kiwanda cha kuchakata gesi utabadili maisha ya watanzania ama wanaita game changer huo ni uongo wa wazi kwani kiwanda hicho faida pekee ambayo tutaipata kwa Tanzania ni ajira, kodi na vitu vidogo vidogo lakini sio hasa keki ama nyama yenyewe ya gesi kwani gesi sio yetu.

Ukitaka kujua kitakachotokea kwenye gesi kwa kujenga mtambo wa LNG ni kuangalia faida tunayopata kwenye viwanda vya sukari, je tunafaidi uwepo wa bei ndogo ya sukari ama tunafaidi vitu vidogo vidogo kama ajira ya watu wachache, kodi na vitu vingine vidogo vidogo ila bei ya sukari iko juu.

Tunapeana matumaini ila ukweli ni kwamba we are fucked up.

Habari ndio hiyo.
Moja ya mambo ya hovyo ya serikali ya Kikwete

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Ngozi nyeusi kwakweli... ni vituko sana duniani...Yani tupo kama takataka tu. Mtu mweusi hawezi mkomboa mweusi mwenzie zaidi ya kuhakikisha vizazi na vizazi vinakaa kwenye umasikini kikubwa yeye na familia yake wamekimbiza mabillioni nje. Kama kweli Mungu yupo kuna watu watapata tabu sana.
Weusi mmezidi mno gubu na roho mbaya!! Mungu mwenyewe mlimgeuka !! aka watosa sasa leo mnalilia nini?? tena aliwaambia ''mtajiuza kwa adui yenu na hakuna atakae wanunua!! mtakosa thamani mnooo!!'' ndo haya sie twajua tulieni dawa iwaingie!

hao viongozi wanao kimbiza hela nje wanaya jua haya nyie hamna maana kuwageuka ni dakika sifuri tu sasa akae hapo kwa nini??
 
TPDC wao wananunua gesi kutoka kwa makampuni ya kigeni yanayochimba gesi na kisha kuiuzia TANESCO, yaani makampuni yanachimba, yanapiga gharama za uchimbaji na faida yake, yanaiuzia TPDC, kisha TPDC anaweka cha juu na yeye anaiuzia TANESCO halafu TANESCO anazalisha umeme anauzia wananchi.

Screenshot 2022-05-05 at 15-01-35 Julius Nyerere Interview (1996).png
 
Weusi mmezidi mno gubu na roho mbaya!! Mungu mwenyewe mlimgeuka !! aka watosa sasa leo mnalilia nini?? tena aliwaambia ''mtajiuza kwa adui yenu na hakuna atakae wanunua!! mtakosa thamani mnooo!!'' ndo haya sie twajua tulieni dawa iwaingie!

hao viongozi wanao kimbiza hela nje wanaya jua haya nyie hamna maana kuwageuka ni dakika sifuri tu sasa akae hapo kwa nini??
" KARMA "
 
Kuna mambo bado hayajawekwa sawa na yakaeleweka vyema.

Gesi inayochimbwa Mtwara sio ya watanzania, ile gesi ni ya makampuni ya kigeni na sio ya Watanzania.

Ieleweke pia kwamba Gesi ile iko 18% nchi kavu na 82% majini ama baharini kwenye kina kirefu.

Ieleweke zaidi kwamba shirika la mafuta na petroli la Taifa ama TPDC wao ni watu wa kati kati ama middle man wa gesi inayozalisha umeme Tanzania.

TPDC wao wananunua gesi kutoka kwa makampuni ya kigeni yanayochimba gesi na kisha kuiuzia TANESCO, yaani makampuni yanachimba, yanapiga gharama za uchimbaji na faida yake, yanaiuzia TPDC, kisha TPDC anaweka cha juu na yeye anaiuzia TANESCO halafu TANESCO anazalisha umeme anauzia wananchi.

Kwa kiswahili chepesi ni kwamba, kwenye gesi ya mtwara TPDC ni dalali ama machinga wa gesi, yeye mwenyewe hana gesi ila kutokana na sheria za nchi, ana umiliki kidogo wa hisa kwenye hayo makampuni yanayochimba gesi. Serikali ama TPDC hawana kisima hata kimoja cha gesi, wao pia wananunua.

Hivyo basi ifahamike kwamba umeme wa gesi hautakuja kua bei Rahisi Tanzania kwa sababu gesi ina madalali ama inapitia mikono mingi na kila wakala ama dalali anaweka cha juu hadi kumfikia TANESCO na tanesco kuwafikishia walaji ambao ni wanachi.

Hivyo ifahamike zaidi kwamba gesi iliyoko kusini 90% ilishauzwa na wamakonde wakae wakijua hawana gesi pale, sio yao ni ya makampuni ya kigeni.

Na hao unaosikia wanasema uanzishwaji wa kiwanda cha kuchakata gesi utabadili maisha ya watanzania ama wanaita game changer huo ni uongo wa wazi kwani kiwanda hicho faida pekee ambayo tutaipata kwa Tanzania ni ajira, kodi na vitu vidogo vidogo lakini sio hasa keki ama nyama yenyewe ya gesi kwani gesi sio yetu.

Ukitaka kujua kitakachotokea kwenye gesi kwa kujenga mtambo wa LNG ni kuangalia faida tunayopata kwenye viwanda vya sukari, je tunafaidi uwepo wa bei ndogo ya sukari ama tunafaidi vitu vidogo vidogo kama ajira ya watu wachache, kodi na vitu vingine vidogo vidogo ila bei ya sukari iko juu.

Tunapeana matumaini ila ukweli ni kwamba we are fucked up.

Habari ndio hiyo.
Mbona mambo yapo wazi siku nyingi tu,yule Profesa Muhongo akiwa waziri wa madini na nishati,alipokuwa anauza vitalo vya gesi kwa wageni ulitegemea nini?
Alipouza vitalo alitamba sana kuwa wazungu ndio wenye fedha.Badala ya TPDC kuwezeshwa gesi ikageuka laana.
Labda jambo muhimu ni kujua Huyo Professor aliuza vitalo vingapi na kwa makubaliano yapi.
Pili je mchango wa wamiliki hao kama hawaendelezi vitalo ni hatua gani za kisheria zinaweza kuchukuliwa?
Tatu,kama kweli wameuza gesi yote kwa wazungu mbona miaka yote ya utawala wa Mjomba Magufuli walikimbia ?
Tanzania imelaanika au tubadiri jina?
 
86 Reactions
Reply
Back
Top Bottom