Watanzania tunapaswa kuambiwa na kujua ukweli kwamba Gesi inayochimbwa Mtwara si yetu

Mbona mambo yapo wazi siku nyingi tu,yule Profesa Muhongo akiwa waziri wa madini na nishati,alipokuwa anauza vitalo vya gesi kwa wageni ulitegemea nini?
Alipouza vitalo alitamba sana kuwa wazungu ndio wenye fedha.Badala ya TPDC kuwezeshwa gesi ikageuka laana.
Labda jambo muhimu ni kujua Huyo Professor aliuza vitalo vingapi na kwa makubaliano yapi.
Pili je mchango wa wamiliki hao kama hawaendelezi vitalo ni hatua gani za kisheria zinaweza kuchukuliwa?
Tatu,kama kweli wameuza gesi yote kwa wazungu mbona miaka yote ya utawala wa Mjomba Magufuli walikimbia ?
Tanzania imelaanika au tubadiri jina?
Prof Muhongo kwa uwaziri wake tu asingekuwa na mamlaka ya kuuza hivyo vitalu unavyovisema !! Labda kama alitumwa kufanya hivyo !!
 
Kuna mambo bado hayajawekwa sawa na yakaeleweka vyema.

Gesi inayochimbwa Mtwara sio ya watanzania, ile gesi ni ya makampuni ya kigeni na sio ya Watanzania.

Ieleweke pia kwamba Gesi ile iko 18% nchi kavu na 82% majini ama baharini kwenye kina kirefu.

Ieleweke zaidi kwamba shirika la mafuta na petroli la Taifa ama TPDC wao ni watu wa kati kati ama middle man wa gesi inayozalisha umeme Tanzania.

TPDC wao wananunua gesi kutoka kwa makampuni ya kigeni yanayochimba gesi na kisha kuiuzia TANESCO, yaani makampuni yanachimba, yanapiga gharama za uchimbaji na faida yake, yanaiuzia TPDC, kisha TPDC anaweka cha juu na yeye anaiuzia TANESCO halafu TANESCO anazalisha umeme anauzia wananchi.

Kwa kiswahili chepesi ni kwamba, kwenye gesi ya mtwara TPDC ni dalali ama machinga wa gesi, yeye mwenyewe hana gesi ila kutokana na sheria za nchi, ana umiliki kidogo wa hisa kwenye hayo makampuni yanayochimba gesi. Serikali ama TPDC hawana kisima hata kimoja cha gesi, wao pia wananunua.

Hivyo basi ifahamike kwamba umeme wa gesi hautakuja kua bei Rahisi Tanzania kwa sababu gesi ina madalali ama inapitia mikono mingi na kila wakala ama dalali anaweka cha juu hadi kumfikia TANESCO na tanesco kuwafikishia walaji ambao ni wanachi.

Hivyo ifahamike zaidi kwamba gesi iliyoko kusini 90% ilishauzwa na wamakonde wakae wakijua hawana gesi pale, sio yao ni ya makampuni ya kigeni.

Na hao unaosikia wanasema uanzishwaji wa kiwanda cha kuchakata gesi utabadili maisha ya watanzania ama wanaita game changer huo ni uongo wa wazi kwani kiwanda hicho faida pekee ambayo tutaipata kwa Tanzania ni ajira, kodi na vitu vidogo vidogo lakini sio hasa keki ama nyama yenyewe ya gesi kwani gesi sio yetu.

Ukitaka kujua kitakachotokea kwenye gesi kwa kujenga mtambo wa LNG ni kuangalia faida tunayopata kwenye viwanda vya sukari, je tunafaidi uwepo wa bei ndogo ya sukari ama tunafaidi vitu vidogo vidogo kama ajira ya watu wachache, kodi na vitu vingine vidogo vidogo ila bei ya sukari iko juu.

Tunapeana matumaini ila ukweli ni kwamba we are fucked up.

Habari ndio hiyo.
Ukweli upi tena? Kwani huwajui wenye gesi yao? Endelea kupiga jalamba
 
86 Reactions
Reply
Back
Top Bottom