Watanzania tunamuhitaji Musa kutupeleka nchi ya ahadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania tunamuhitaji Musa kutupeleka nchi ya ahadi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KXY, Jan 12, 2012.

 1. KXY

  KXY JF-Expert Member

  #1
  Jan 12, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 876
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 60
  ​Wengi wetu nataraji tutakuwa waumini wa dini na bila kuzitaja dini hizo naamini asilimia kubwa ya sisi waumini tumeshasikia hadithi za Musa/Moses. Katika hadithi hizi sehemu kubwa inaelezea safari ya kuwatoa utumwani Waisraeli na kuwaongoza katika nchi ya ahadi.

  Kuna mambo mengi sana ya kujifunza katika safari hiyo ya kuelekea nchi ya ahadi, nitaorodhesha machache hapa chini.
  1. Haikuwa rahisi kutoka kwenye mikono ya Farao
  Japokuwa Mungu aliwaadhibu Wamisri kwa mapigo kadhaa watu hawa hawakukubali kirahisi kuwaachia watumwa wao, hii inaonesha ni kiasi gani Farao alinogewa na kula vya bure kiasi cha kuvumilia mapigo na hata alipowaruhusu alituma majeshi yake kuwafuatilia.

  2. Manung’uniko ya Waisraeli safarini
  Japo watu hawa walifahamu kuwa wanaenda kwenye nchi ya ahadi, nchi yenye neema za kila aina na hawatakuwa watumwa bali wenye nchi lawama na manung’uniko yalikuwa hayaishi. Kitu cha kusikitisha ni kwamba ilifika wakati wapo waliosema ni bora wangelikuwa Misri utumwani kuliko mateso wanayoyapata huko jangwani.

  3. Musa hakufika katika nchi ya ahadi
  Safari ambayo Musa aliwaongoza Waisraeli iliyojaa changamoto za kila aina toka kwa adui na watu aliowaongoza, kwa kiongozi huyo iliishia mpakani na aliishia kuiona kwa mbali tu. Kazi kubwa ilifanywa na Musa lakina Yoshua ndio aliyeimalizia na kuwavusha mto jordan kuingia nchi ya ahadi.

  Nimejitahidi kuelezea kwa kifupi bila kuingia kwa kina sana ili kujenga tu taswira ya ninachotaka kukielezea.

  Watanzania ili tufike nchi ya ahadi tunahitaji tumpate Musa wa kutuongoza lakini aelewe yafuatayo.
  1. Imani na uthubutu
  Kama nilivyoelezea hapo juu kwenye namba moja, kazi ya kuwatoa Waisraeli Misri haikuwa rahisi vivyo hivyo kazi ya kuwatoa Watanzania walipo haitakuwa rahisi. Farao(wanao nufaika na hali duni yetu) hatokubali kirahisi kuachia watumwa wake, Musa anatakiwa aamini anaweza na athubutu kutuongoza.

  2. Uvumilivu na hekima
  Katika safari hii lazima Musa aelewe kwamba yeye ndio kiongozi na ndio mwenye maono lakini anaowaongoza wanaweza wasimuelewe wakati mwingine. Aelewa kwamba tunakoelekea ni kwenye neema na yupo tayari kuwaongoza watu wake katika nyakati za maatabiko akiamini tukifika mambo yatakuwa mazuri kwa kila mmoja.

  3. Kujitoa mhanga
  Sio rahisi kukubali kufanya yote aliyoyafanya Musa kama utatambua kuwa mwisho wa safari hutakuwepo kula mema ya nchi. Lazima Musa aelewe kwamba akienda kinyume au kwa sababu nyingine yoyote kuna uwezekano wa yeye kutofika. Baada ya kutambua hilo anatakiwa kuwaandaa kina Yoshua kupokea kijiti na kuhakikisha tunafika katika nchi ya ahadi.

  Sijui safari hii itachukua miaka 40 au minne, sijui kama Musa ameshazaliwa, yupo kwenye kikapu kuepushwa na mauaji ya Farao, analelewa kwenye familia ya kifalme ya Farao au yupo mlima Sinai.

  Nawasilisha,

  KXY.
   
 2. Mchaga 25

  Mchaga 25 JF-Expert Member

  #2
  Jan 12, 2012
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 463
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hatumitaji musa wala bakari tunaenda wenyewe, ngojea mgomo wa madaktari na maaskari ufanikiwe
   
 3. KXY

  KXY JF-Expert Member

  #3
  Jan 12, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 876
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 60
  madaktari wakienda njia yao, askari, walimu na wengineo, kila mmoja akienda njia yake tutafika??
   
 4. Mchaga 25

  Mchaga 25 JF-Expert Member

  #4
  Jan 12, 2012
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 463
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hapo ndipo umuhimu wa Musa utakapoonekana ndio maana kuna mambo yanatakiwa yatimie ile mengine yaanza. Kikombe cha hukumu ya ccm hakija jaa. Huu ni mwanzo wa mwisho
   
 5. KXY

  KXY JF-Expert Member

  #5
  Jan 13, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 876
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 60
  Mi nasubiri, with the right mindset
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Jan 13, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,537
  Trophy Points: 280
  KXY, Musa wetu yupo!. Kama kawaida nabii huwa hakubaliki nyumbani kama jiwe walilolikataa waashi, litafanywa kuwa jiwe kuu la pembeni!.
   
 7. KXY

  KXY JF-Expert Member

  #7
  Jan 13, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 876
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 60
  kama yupo tutamuona ukifika mda wa kuvuka bahari ya shamu..
   
 8. N

  Ndanshau New Member

  #8
  Jan 13, 2012
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Musa wetu naona bado asubiri kidogo kwenye utulivu kule mlima wa Sinai kwani Farao na jeshi lake wanafanya kila hila humdhuru.
  Kwa vile Mungu amesha muandaa, tunaammini ataongoza kutuvusha .
  HAKUNA sililokuwa na mwisho.
  Ndanshau
   
 9. KXY

  KXY JF-Expert Member

  #9
  Jan 13, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 876
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 60
  Sawasawa Mkuu.
   
 10. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #10
  Jan 13, 2012
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Tamthilia nzuri. Musa wako ni wewe mwenyewe. Kama huthubutu usitarajie wengine ndio wakutendee. Musa wako ni elimu na maarifa uliyonayo. Kama huwezi kuyatumia utabaki na ndoto tu.
   
 11. KXY

  KXY JF-Expert Member

  #11
  Jan 13, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 876
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 60
  Advice taken.
  Kuna wengi wanaohitaji kushikwa mkono, kama kila mtu ataitetea nafsi yake sijui mwisho utakuwa vp. Kila mmoja kwa nafasi yake anatakiwa ku-act lakini kwa manufaa ya wote na sio binafsi
   
 12. D

  Dawa ya Mjinga JF-Expert Member

  #12
  Jan 13, 2012
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 382
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Wakuu, mimi naamini kuwa Musa tayari tulikuwa naye. Bahati mbaya kama Musa wa Waisraeli katuacha jangwani. Kwa bahati mbaya zaidi hatujampata Joshua wa kutufikisha Kaanani. Huyo ndiye tunayemhitaji. Kwa kweli kama ingejulikana kuwa Musa hafikishi watu Kaanani ni bora safari ingeanza chini ya Joshua kabisa. Tunamuhitaji Joshua si Musa.
   
 13. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #13
  Jan 13, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,189
  Trophy Points: 280
  Tatizo letu ndilo hili, badala ya kila mmoja kufanya kazi, tunamtegemea "Musa".

  Mwishowe unasikia "Kikwete chaguo la mungu", miaka miwili baadaye hao hao wanataka kumpiga kwa mayai viza.

  Kwa nini utegemee Musa?

  Zaidi ya Musa, Watanzania wanahitaji muamko katika jamii nzima. Musa ni mtu mmoja tu na hata kama ana nia ya kweli kufanya mabadiliko, kama system ya nchi na muamko wa watu hautabadilika, atashindwa tu. Maana siku hizi hata kufikia uongozi wa juu lazima mtu awe mchafu na ajue kutafuta hela chafu kwa kampeni.

  Kwa hiyo, watu safi na wenye nia ya kusaidia by virtue of their ethics hawawezi kupanda the national ladder of visibility.

  Watu wanaoweza kupanda ladder of visibility ndio hao tulionao, wote scandals na hawawezi kuleta mabadiliko yoyote.

  Ngoma yetu inahitaji wote tucheze, Musa peke yake hawezi kitu.
   
 14. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #14
  Jan 13, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,189
  Trophy Points: 280
  Exactly my sentiments.
   
 15. KXY

  KXY JF-Expert Member

  #15
  Jan 13, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 876
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 60
  Hata uwe na shoka lenye makali kiasi gani bila mpini ufanisi wake hautaonekana, na mpini bila shoka ni gongo tu haliwezi kata mti
   
 16. kiroba

  kiroba JF-Expert Member

  #16
  Jan 13, 2012
  Joined: Sep 10, 2011
  Messages: 324
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ni mada nzuri sana,mtoa mada kwa kweli ametumia akili sana kuiwakilisha.

  Kwa upande wangu, musa wetu alikuwa ni mwalimu nyerere. Ametutoa enzi za ukoni na akatufikisha hapo alipotuacha tunajitawala wenyewe.

  Sasa Joshua wetu ndio hapo sasa kwenye kasheshe. Hapa wamepita watu wengi tukadhani ndio majoshua wa kutufikisha pale musa wetu alipotuach,kumbe hapakuwa na joshua yeyote bali ni mifano tu ya Joshua.

  Kwa mtazamo wangu, sasa hivi yatubidi kwanza tuache unafiki wa kushabikia vyama na kutukana mtu mmoja mmoja au kundi fulani. Yatubidi kweli tumtazame mtu sahihi anayeweza kutufikisha huko tuendako. Kiukweli kama tukiachilia mbali chuki tulizonazo kwenye mioyo yetu basi mtakubaliana nami Joshua wetu atakuwa ni Edward Ngoyai Lowassa. Mwenye swali aniulize nimjibu kwa hoja na wala si matusi kwa sababu hapa ni mahali pa wasomi na wastaarabu.
   
 17. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #17
  Jan 13, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,189
  Trophy Points: 280
  Mentality nzima kwamba kiongozi ndiye atakayetuwezesha kubadili mambo ina mapungufu makubwa sana katika miaka hii.
   
 18. KXY

  KXY JF-Expert Member

  #18
  Jan 13, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 876
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 60
  Mkuu Kiranga nakuelewa unachoongelea, hoja yangu ni kwamba kila mtu ana manung'uniko yake, wamachinga wanaonewa, walimu wana madai yao, madaktari wanafukuzwa, watumishi hawapandishwi vyeo n.k. Kama hakuna wa kutuunganisha kila moja akiwa peke yake hakuna atayefanikiwa, itakuwa rahisi kujenga taswira kwamba kundi flani sio wazelendo au hawa wauni, mara wale wanatumiwa na watu flani ili mradi tu kututenganisha. Sijui kama unanipata vizuri
   
 19. KXY

  KXY JF-Expert Member

  #19
  Jan 15, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 876
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 60
  Moment of silence! R.I.P Regia
   
 20. mose

  mose Senior Member

  #20
  Jan 18, 2012
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 110
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Pendo lililobarikiwa KXY,


  Umetaja kuhusu 'Nchi ya Ahadi'; sasa sina budi kuzungumza neno juu ya hili.


  Mshairi Khalil Gibran kutoka Lebanoni alikuwa sahihi aliposema 'Vitu vyote tuvionavyo kuja na kazi za mwanadamu vilianza kama Fikra ndani ya kichwa cha fulani'(Kitabu, Wisdom of Khalil Gibran)... Fikra kupitia kazi za mikono ya mwanadamu huumba na kudhahirisha lililotangulia 'kuonekana' katika jicho la akilini. Mchakato huu wa utungikaji neno/fikara na mfuatio wa uumbwaji wa mfano wake katika ulimwengu wa nje wa mtu ni finomena ya uumbaji. Na hivi unaweza kudadavua ukweli wa kwamba kionekanacho kudhahirika katika mazingira ya mwanadamu ni kwa sehemu mchakato wa Asili na pia pilika za mwanadamu anayetafuta kumudu mazingira yake, ustawi wake na basi mustakabari wake.


  Uwepo wa mwanadamu katika hii dunia unakirimiwa mahitaji yake ya lazima na kimsingi kwa Neema ya vitu viwili--Ardhi na Nguvu za Jua. Uhai na uzima wa vyote vilivyomo duniani ni kudra na karama za ardhi na Jua kwa namna iliyo ni numononi--tuliache hili kwa kuanza kwa kuwa linapelekea hitaji kwa uchanganuzi wa kimetafizikia pia; japo si kuwa halina umuhimu... Kimsingi vyote juu ya ardhi vimefanyika kwa vumbi, pumzi na maneno yashikiliyo maumbo na ipo namna hili kuanzia sasa linaweza kusanisiwa katika sayansi na kuleta maarifa mapya yenye kuzaa mawezekano zaidi ya ilivyo kwa sayansi ya leo inayobainisha visomo vya fizikia kwa minajili ya vipimo na ukadirishaji wa mahusiano kati ya maada na kinatachotajwa leo ni 'Nishati'... Lakini maumbo yote yenye hadhi ya uhai na yasiyo hai hufungamana mazingara mengine ya kiwezekano ilivyo ni jinsi ya kiokalti(toka kilatini, kilicho katika upande uliofichika) na hata tukitajacho hapa kama 'Metafizikia'(Kiyunani, 'Zaidi kupitiliza nguvu za kimaumbo').


  Ninalazimika kutambulisha muktadha wa visomo anuai kwa kuwa sasa ndiyo wakati hivi vyote vyapasa kuwa ni sehemu ya visomo vya watu wote wenye kutafuta maana katika 'Uzima' na maumbile... Kuanzia kufikirika kwa tonadari(Kng, atom) hadi muonekano wa Kosmosi(Mkusanyiko wa nyota, mpangilio na mienendo yake katika Mbingu isiyokuwa na mwanzo wala mwisho).


  Pia niyatambulisha haya kwa kuwa ni visomo vyake vinaweza kumeza kasumba na usadikifu pofu wa kimakundi unaoathiri ustaarabu na maendeleo ya wanadamu katika vipindi vya nyuma hadi sasa. Ikiwa kuna Agano la Kale kwa mujibu vya vitabu vya watu na Historia ya Waisraeli, halafu ambapo ustaarabu wao ulizingatia namna ya utaasisi wa Kiongozi wao aliyefahamika kwa jina la Musa; alikuja mtu kwa jina la Yesu ambaye hao walio nduguze hawakumpokea kama 'Musa' mwingine aliyekuja 'kutia maana' juu ya mapokeo yao yaliyojengeka kwa msingi ya taasisi mbili mashuhuri za Ukuhani na Uongozi wa jamii za kiyahudi--yumkini Yesu alikuwa akijitahidi na kujaribu kuleta muktadha mpya wa elimu na mwangaza wa jinsi ya kuibadili hadhi na ustaarabu wa Wayahudi ili kuchukua fahari bora zaidi... Ndivyo hivi Yesu alifundisha juu ya mambo kama 'Ufalme wa Mbingu', Kuishi katika hali ya Neema ili kustahili Ujazi, siri zenye kuleta furaha na ule Ukweli wenye kuweka mtu huru...


  Mafundisho ya Yesu peke yake yanahitaji uwanja wake kwa kuwa alichofundisha, kwa wenye hekima, ni zaidi ya 'Mwongozo wa Agano Jipya kwa Wayahudi' na ni mafundo ya kugema mawezekano ya siri za Uzima na neema ya ulimwengu wote mzima--jambo ambalo hadi leo hii walimwengu wamekosa kung'amua kwa kuwa wangeling'amua ustawi, ustaarabu wa mataifa mengi ungekuwa tofauti na ilivyo leo kote duniani. Ingelikuwa mapenzi yangu sana nizungumze kilichokoswa kueleweka kuhusu Yesu na shughuli yake kama mtu miongoni mwa watu wa taifa lake lakini itoshe kudodosa bado nafasi ipo kuweka mambo sawa na hili sasa litatimia...


  Mimi nikiwa kama mtu, niliyezaliwa katika ardhi ya bara la Afrika nitalipenda nizungumze na kudhihirisha mengi katika upeo na akili yangu kama mwana wa Afrika--kwa hivyo si mapenzi yangu kabisa kuona watu wa Afrika wanatumia historia ya watu wa mataifa mengine kusimamisha nguzo za imani zao... Roho inashuhudia nafsi yangu kuwa mwanadamu yeyote katika sura ya dunia anaweza kuinuka na kustawi kwa mwongozo na nuru ya dhamira yake njema katika kusudio jema la kuishi hapa duniani. Imani lazima kuwa ni njia kumpeleka mtu katika Hakika kwa ile kweli yenye kutunza na kutawala yote... Na haijalishi ninaweza kukutana na watu kutoka pande zipi za dunia, maarifa na hekima yao kuhusu siri za mbingu na nchi--ilivyo ndiyo kiini cha ushawishi mkuu wa yote katika dini; zitapata hakiki katika kioo cha roho iliyo ndani yangu. Na hivi nina uhuru kamili kwa mfano; wa kutofungamana na dini yeyote ya mapokeo... Lakini kwa Neema ijayo kwa Nuru na Saburi, ninaweza kutambua yote yenye kheri kutoka dini ya kimapokeo yeyote ya hapa duniani... Kwa nidhamu hii ninakiri yeyote aliyezaliwa hapa Afrika kama mimi pia uwezo upo kwake kuchagua njia ya uhuru na nidhamu katika kutafuta kweli ama kuridhi yale ya kufikia bila utashi.


  Chaguo langu la muktadha wa utu-anadamu vile kugusia kwa mfano shauri la Uafrika na Afrika ni kwa kuwa ninatambua katika kudra zifanyikazo na makundi ya viumbe hai katika kutia hadhi ya upekee wa kudhahirika na neema iliyofungamana na mawezekano ya ustawi wake. Kwa neema na kheri, nina mapenzi yaliyotukuka kwa bara la Afrika na watu wake--wale waishio na kustawi katika mapana ya nchi yake. Japo binadamu yeyote anaweza kuwa na hadhi ya utu na fahari zake zenye kuweza kupitiliza kawaida; lakini kushtukia kudra zijazo na makabila ya watu na hata mabara kwa ujumla kuna weza kuleta mchanuo wenye uzuri wa kipekee ikiwa yeyote mwenye kuzaliwa upya katika fahari yenye kupitiliza kawaida ya kiutambuzi. Kwa misingi hii miye ninayomakusidio kwa kuja kuona Afrika iliyofanyika katika fahari mpya... Kwangu mimi hiyo ndiyo inakidhi hadhi na sifa ya kuwa 'Nchi Mpya'--na hii ni ndoto yangu ninayoshiriki na wote wenye kutafuta mahala pa kimbilio; njooni tuote 'Ndoto Afrika'.


  Ndoto izungumziwavyo hapa ni Ndoto kwa mujibu wa hisia za matamanio na kuhuisha picha ya mapendezo; lakini pia ni Maono kwa sura ya Hakika kuweza kudhahirika. Kuzungumza mazuri yenye kupendeza na kuweza kutamaniwa ni moja ya shughuli ninayofanya katika kualika wengi katika kalamu ya wateule... Lakini upande mwingine mahiri ni Maono na njia za msingi kufikia Fahari yenye kuonekana kwa ubora wangu katika fahamu za akili zangu. Kwangu mimi yabidi kutambua kudra zinazoweza kusukia fahari mpya na hii yaweza kufanyika kwa mtu yeyote akiwa atakuwa na mapenzi ya dhati kwa fahari ya msingi ya utu-anadamu wote--kujipenda na kujikubali kwa yote; kushukuru na kutukuza kwa neema ya fahari yako kama mtu wa kabila fulani ama utu-anadamu fulani; na hii kuakisika katika matendo yako ya kila siku na hisia na mawazo.


  Kudra huja na miili lakini karama huja na nuru ya roho... Yeyote anayetaka ufunuo wa mambo ya mbele kiwakati; wenye kheri katika roho; kwa kukidhi kwake kuishi katika hali ya kushukuru na kushirikiana kudra za kufanyika kwa mwili wake atajaliwa karama bora ili vipawa vya akili vipate kuongozeka na basi ili kuelekea kutosheleza hamu/tamanio lake lililosafi kama roho ilivyo ni safi kutunza 'maneno' yanayoshikilia maumbo yote katika fahari iliyofichika na basi hata hakuna kazi ya mikono ya mwanadamu inayoweza kuchafua hadhi ya uwezo wake ila tu mwanadamu hujipoteza njia kwa kutoamka kiroho ili kukirimiwa kheri yenye kuwezekana kwa kuzidishwa kwa talanta ya usafi wa nia na makusudio yake kwa wakati.


  Muktadha wa Roho si lazima kuwa kama watu wengi wamepata kuzoea kusikia katika dini za mapokeo japo ukweli wake unaweza kukaribia yale yalipata kuzungumzwa labda hapa ama pale katika hizo hizo dini... Roho haigusiki lakini yaweza kuhuisha vile vilivyo katika mpangilio fulani na hivi kuongoza njia zake zaUzima--mizunguko ya kuzaliwa, kukua, kufa na kuongezeka idadi pia ama pia kufufukia katika fahari ya miili mingine. Azma yangu ni kuweka bayana baadhi ya vile ambavyo vinavyoweza kutajwa ni siri za uzima kusudi maarifa haya yapate kusanisiwa katika miundo-kazi ya mwanadamu na basi kuleta namna ya Uzima wa vyombo vya shughuli/kazi.


  Kama vile Kahlil Gibran alivyopata kusema katika kitabu cha 'Nabii/The Prophet': Kwa uwakilishio wa kauli ya Almustafa; yeye alisema hivi juu ya kazi:


  “Mwafanya kazi ili muende hatua sambamba na dunia na roho ya uzima wa Nchi ya Dunia. Kwa kuwa kukaa bure ni kuwa mgeni katika majira na misimu, na kukaa kando na msongo wa maisha, wenye kupiga kwata katika heshima kuu na kujivunia kujikabidhi kuelekea kule Kusikompaka. Utendapo kazi wewe ni filimbi kupitia moyo wake minong’ono ya mida hugeuka muziki”.

  Kazi ni utu; kichangamshaji chenye kutusaidia kujifahamu sisi na mazingira yetu tulimo twaishi na wakati wake.


  Na msingi huu ninatambua--kwa mtu yeyote na kwa wakati wowote uliosahihi, mshughuliko wake ni sehemu ya kule kufunuka kwa fahari ya ustawi wake ijayo pia kwa neema ya majira ya nchi. Wakati na Majira ndiyo nguzo mbili ambazo zinashuhudia nafasi ya mizunguko ya asili kama vile usiku na mchana ama majira ya mwaka/kalenda kuwa sehemu muhimu ustaarabu na ustawi wa watu. Ama kwa hakika hata katika visomo vyote vya ustawi na ustaarabu wa watu kati ya mambo ya msingi kutizama ni 'namna za kalenda' na shughuli zinazoambatana na hiyo... Iwe ni katika kuchunguza Ustaarabu kama ule wa Babiloni, Mexico ya kale, India ya kale ama hata himaya zilizopata kustawi Afrika magharibi ya Zamani.


  Katika Hisia na Utambuzi wa kiMaono ya kuelekea' Afrika Mpya' ninaona mtiririko wa shughuli na kazi kama mchakato wa msingi katika ufikiaji wa Fahari yake Mpya. Ni kupitia hamu ya hili hadhi ya Ujazi, Fanaka, Liberiti(uhuru wa kiutu) na furaha kwa watu wote wa Afrika hata kupitiliza mipaka ya Afrika; imetungika ndani yangu namna ya uelewa wa namna ya muktadha wa Uchumi Mpya. Ndani yangu kuna ndoto ya ajabu kukubalika kwa mtu wa kawaida lakini imani yangu haisitishi nia ya kushuhudia na kuwaambia bayana ndugu zangu wote--Afrika ndiyo itakuwa Bara Mama la ustaarabu na ustawi wa dunia yote kwa takriban miaka 2000 ijayo... Kuwa Bara Mama haina maana Afrika ndiyo inakuwa 'Taifa lenye Nguvu/Mabavu'--la hasha; Afrika ina kudra ya kuwa mlezi kwa mchanuo na ustawi mpya. Afrika itakuwa nchi moja yenye kufanywa na jumuiya nyingi zenye ushirika wenye utangamano fulani wa mshughuliko, bidii na fahari--ushirika huu ni Harambee Halisi; Na Afrika ina fahari ya Simba... Nitazungumza hili zaidi kwa sura yake itarajikayo panapo kheri na majaliwa.


  Katikati ya Afrika ya Zamani na Afrika Mpya kuna daraja la mauti. Watu wa Afrika hawana budi kufa ili kuzaliwa upya katika nuru na 'mwongozo mpya' kutoka ndani na ndani ya nafsi zao na ili kumalizana na ulimwengu hadaa wa leo wa ufikirifu pofu wa kimakundi. Sehemu ya jitihada ya kushiriki haya yote ni katika kule kuchochea mawezekano ya fikra za mtu mmoja mmoja katika kule kujaribu kunasua mtu na ukundiko wake wa kiimani ama dini--hakuna jinsi, kila mtu hana budi kubeba mzigo wake katika wakati hu muhimu. Yeyote anayeona 'hajiwezi' ila kubakia na makundi yake ya usadikifu hata kwa mambo ambayo ingelimpasa sana kujimulika mwangaza--kwake huyo hakuna jinsi ila Wakati kuwa muamuzi wa mavuno ya ustahili wa wale wenye kufaulu kujinasibu katika kule kuzaliwa upya ajili ya fahari mpya.


  Ni mtu mmoja mmoja aliyejikwamua kiakili ataungana na mwenzake katika shauri lenye kheri zaidi na kuzaa ushirika na taasisi zenye Nguvu Mpya, Ari Mpya na Hadhi Mpya. Mtu wa zamani ni kimeo taslim na wala hata nusa wala kuonja harafu ya marashi ya ustawi mpya wenye mawezekano; lake itakuwa ni kusakamwa na maradhi na kule kutokomea katika migogoro isiyo na suluhu na pia maangamizi ya taasisi na mifumo isiyofaa tena.


  Na hivi Afrika Mpya itafanyika kwa Uhandisi wa Kijamii ilivyo ni muktadha mpya wa kuchochea miundo rasmi ya kujengeka na kubomoka kwa jumuiya za watu katika taratibu zenye kuwa na kheri na kuridhiwa na jamii yote nzima. Mengi hayatakuwa kama ilivyo leo kwa kuwa hata taasisi ya ndoa kwa mfano itatoweka. Lakini watoto watazaliwa kwa shangwe na watatunzwa vema mbali kupita malezi tuliyoyajua wengi leo... Uhuru wa mwanamke utawezekana kwa kufanikiwa kwa Usanisi wa Ujasiriamali wa Kijamii na hivi wanawake watakomboka na mifumo dume... Wanawake watakuwa na uhuru wa kuchagua na kupanga uzazi wapendavyo. Siku za mbele itakuwa ni kawaida mwanamke kuzaa na mwanaume zaidi ya mmoja bila kuonekana ni ubaya... Siku za mbele familia nyingi itakuwa ni vikundi vya wake kwa waume na watoto na si familia ya mama na baba mmoja. Wake kwa waume watakaa pamoja kwa kuongozwa na vipaji, uwezo na umahiri katika mapana fulani ya ustawi na ustaarabu... Mambo kama wivu wa kimahusiano/mapenzi hayatawekupo na upendo, nidhamu na heshima vitatawala--kwa kuwa wivu huu ni udhaifu wa hisia za kimwili kuchangamana na mawazo hafifu ya mtu--iwe mwanaume ama mwanamke.


  Watoto wa siku za mbele watakuwa na uwezo wa mkubwa zaidi kuliko leo kadri wakuavyo kwa kuwa itakuwa ni kawaida watoto kulelewa na zaidi ya 'mama' mmoja katika kaya... Mtoto anayelelewa kwa upendo na zaidi ya mwanamke mmoja anajijengea hazina kubwa kitabia na mwenendo kuliko mtoto wa kulelewa na mama mmoja... Wanawake watachukua nafasi muhimu sana katika utunzaji na malezi ya jumuiya za watu--wanawake ndiyo wakaotawala vyombo vya serikali na utumishi kwa uwiano wa 2:1 dhidi ya wanawaume. Wanaume watatawala vyombo vya elimu, ufundi na uhandisi kwa uwiano wa 2:1... Na elimu ya kesho itakuwa na hadhi tofauti na elimu tuijuavyo leo.


  Siku za mbele--katika kukadirisha msuko endelevu wa ustaarabu na ustawi mpya ninapendekeza mtoto wa kwanza wa mwanamke yeyote kuwa ni kutoka kwa kabila lake, utaifa wake, ubara wake ama utu-anadamu wa jinsi yake. Na hivi itakuwa ni kawaida mtoto wa kwanza wa mwanamke kuwa hivyo; kutoka hapo kwenda mbele mwanamke anao uhuru wa kuchagua azae vipi kwa kuchanganya vipi... Kwa jinsi hata yeyote mwenye kuweza kufungua jicho hata miaka 200 ijayo upo uwezekano wa kumuona Muafrika kama Muafrika, Mgogo kama Mgogo na labda vile vile Mjaluo kama Mjaluo. Kwa kuwa wanawake wanashikilia fungua wa uwezekano huu na wengi watatii wito huu.


  Siku zijazo, watoto wakwanza kuzaliwa watakuwa wajibu muhimu wa kutunza mapokeo ya asili zao; na wao watafanya hivyo hivyo kwa watoto wao. Kwa namna hii uhandisi utakuwa umekamilika na mengine ya ndani sitazungumza hapa na kwa leo kuhusu ufundi wa kuandaa watu kuzaliwa wapi na kwa nani ambao siku za mbele itakuwa ni sehemu ya ujuzi kamili wa watu utakaokuja na kuongezeka kwa maarifa zaidi.


  Haya yote yatakuja kwa kuwa baadhi ya yale mambo yaliyopata hata kuongelewa na watu wa siku za nyuma kuhusu 'Mtu Mpya na Nchi' Ni Roho yenye kuweza kunasibisha yote hata nje ya wakati kwa namna tunavyoufahamu... Na hakika katika Roho hata mtu wa mbele ya wakati aweza kushughulika na aliyenyuma ya wakati; lakini hili ndilo litakuwa fahari la siku za mbele kupita zama hii ya Usanisi. Kwa kuwa katika usanisi tunajifunza kufanikisha 'mapenzi yawe hapa chini' kama ilivyo 'juu'--siri za ufalme wa Mbingu ulio ndani ya mtu sehemu ya msingi wa maelekezo ya Yesu kuhusu siri za Uzima na njia zake--pamoja hufanya Kweli ya yote; yaliyodhahiri na hata yasiyodhahiri.


  Kwa hiyo nifupishe mmuliko wa leo wa haya yote kwa kusema hitaji kuu kwa sasa 'Mtu wa Usanisi' ama pia kwa muktadha wa kiingereza 'Men Of Social Entrepreneurship Synthesis'... Kwa kuwa huyu/hawa pekee ndiyo njia nyembamba ilekeayo Uzimani. Njia ya Upotofu wengi wajazana na kuangamia kupotea bila kusogelea ufalme mbingu--lo, na uko hapa. Una macho? Una Masikio? ama wapotea kwa kudhania miujiza ya ajabu zaidi ndiyo utambue kweli ya uzima wa yote?

  Ahadi ipo kwenye kufanikisha fahari ya Afrika Mpya.


  Wewe ni Musa na wewe ni Moses--tafuta mhimili wa imani yako katika kuielekea Kweli; hiyo itakuweka huru.


  Upendo
   
Loading...