Watanzania tunalilia bomba la mafuta la Uganda. Hivi gesi ya Mtwara na bomba la gesi vimekufa?

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Mpaka wakimaliza ununuzi wa madiwani na wabunge na wakihakikisha hakuna wa kuwapinga bungeni na uraiani ndio hizi habari itakuwa mwisho kusikia mali za umma zinavyoliwa na ufisadi mkubwa katika awamu hii.

Ivi tunapoamua kushadadia bomba la mafuta kutoka uganda hadi Tanga ivi lile bomba letu la gesi linaingiza kiasi gani?

Ivi ile gesi tunapata kiasi gani kulipa mkopo wa zaidi ya tril 2.5 zilizotumika na ni mkopo toka benki ya Exim China? Na riba yake si itakuwa tunadaiwa zaidi ya tril 3.8?

Sasa hii gesi inasaidia nini zaidi ya mbwembwe za Kinyerezi nini kingine inafanya? Inaingizia taifa pato kiasi gani?

Nani mmiliki wa bomba hilo?
 
Watakwambia mwekezaji bado anarudisha gharama zake tusubiri miaka 20. Wakati huo huo kwa mwananchi wa kawaida TRA wanakukadiria kodi na ulipe kabla hata haujaanza biashara.
 
Watanzania hatujalilia bomba la mafuta la Uganda, Waganda ndo waliona likipita Tz watapata nafuu ya gharama za kulijenga na kuliendesha. Hilo bomba kuna mteremko wa kilomita nyingi sana ambapo mafuta yatashuka yenyewe bila kuhitaji pampu hadi Chongoleani Tanga na sisi watanzania tutanufaika kiuchumi hiyo inaitwa win win situation. Kama unataka tenganisha hizi topic lete ya gesi ya Mtwara peke yake ili wajuzi waupatie ukweli.
 
Hivi mlishawahi kuona Magufuli anapoteza muda kujihusisha na hiyo Gesi!? Inshort ujinga mtupu ulifanyika kule kwa ajili ya kujinufaisha kisiasa...
 
Miradi ya gesi asilia ina walakini kwa kila kona ni shida si tu ujuzi wa kuiendesha bali hata upeo mdogo.Soko la mafuta na gesi asilia haina tofauti na soko la nyanya la Kariakoo au mahakama ya ndinzi Ubungo.Kuna bei inapanda na bei inashuka,lakini serikali imeshindwa kutumia vigezo vya wakati gani wawezeke,kwa mfano gharama ya kuwekeza kwa sasa ipo chini kuliko miaka minee ya nyuma.Lakini watasubiri bei ya mafuta na gesi ipande ndio wawekeze?
Hizi kazi achia weyewe.
 
Hivi mlishawahi kuona Magufuli anapoteza muda kujihusisha na hiyo Gesi!? Inshort ujinga mtupu ulifanyika kule kwa ajili ya kujinufaisha kisiasa...
Mradi uko mikoa ya kusini, kwa awamu hii haina faida wala nguvu
 
Tuliaminishwa gesi ndio mwarobaini wa matatizo yetu, leo SGR ndio tunaambiwa ni MBINGU yetu, mazoba yamejazana DODOMA kushuhudia jiwe la msingi as if TRENI itaanza kupita kwenye hiyo Reli leo leo. Nchi inaongozwa na washamba kweli kweli
 
ACHA UTOTO, NENDA NISHATI KAULIZE NI WAJIBU WAKO, SIO KUKAA MITANDAONI KILA SIKU NA KUIDHARAU NCHI YAKO, MWANA MWENYE LAANA
 
Back
Top Bottom