Watanzania tunakubali mitambo ya dowans iwashwe?!!!!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania tunakubali mitambo ya dowans iwashwe?!!!!!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kabindi, Feb 15, 2011.

 1. k

  kabindi JF-Expert Member

  #1
  Feb 15, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 334
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Niambieni! Mnakubali kuwapa matapeli ushindi?!! ina maana ukiishiwa pesa yakubidi uende kubomoa Bank ukaibe? matumizi yako hayakukuashiria kwamba unaelekea kuishiwa ili ukajenga mikakati halari ya kujipatia pesa?! Kwani matatizo ya Umeme yamekuja Ghafla?!! Mbona hii mitambo ina takribani Mwaka na Kitu na iliingia wakati wa tuna matatizo makubwa! in maana hakuna mikakati ya dharula ambayo ilikwisha chukuliwa?! INAAMANISHA SERIKALI ILIKUWA IMELALA KIASI HIKI!? au IMEFANYA MAKUSUDI KUHARALISHA MITAMBO YA DOWANS?! wanataka kutufanya Watanzania WAPUMBAVU?! MAWAZO YA KITOTO YA JANUARY MAKAMBA YANA NAFASI KWA WATANZANIA WENGI WENYE AKILI?! MNYIKA, INABIDI ISSUE UICHUKULIE SERIOUS usije aibika! Jadiliana na wenzako kabla hujaamua kuzungumza kitu!
  BORA TUKAE GIZA KULIKO KUTUFANYA WAPUMBAVU!! SERIKALI MAKAE NA UJINGA WA KUTUFIKISHA HAPA TULIPO MAANA INAONEKANA MMEFIKIA HATUA HAMUWEZI KUFIKIRI TENA!!
  JARIBUNI KUWASHA MITAMBO YA DOWANS MUONE!!!!!!!
   
 2. M

  Mgalatia JF-Expert Member

  #2
  Feb 15, 2011
  Joined: Nov 28, 2007
  Messages: 297
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nadhani kwa sababu za kishabik tu itafika mahali tukose uelekeo kwa kupinga tu kila kitu kwa sababu kuna neno DOWANS. Hiyo ni kampuni iliyokuwa inafanya biashara na serikali yetu au wizara au baadhi ya watu waliokuwa serikalini wakitumia upenyo au opportunity iliyojitokeza. Mtu yeyote aloes mfanyabiashara mwerevu atafanya hivyo. Sasa tuangalie kosa au ujinga au uzembe uko kwa nani. Nadhani kosa liko kwa walioamua mkataba Wa dowans uvunjwe bila kupitia vipengele vya mkataba uliokuwepo au waliupitia Ila wakapuuza au walishauriwa na wataalam au wanasheria lakini wakaweka maslahi binafsi mbele. Hawa ndio Wa kufuatiliwa na kushughulikiwa. Watafutwe na kushitakiwa .Ila kwa sababu nchi imekuwa Kama shamba la bibi tumefika mahali busara zaidi zitumike na ndipo ninapoona ni vema kukaa meza moja na hawa Dowans ili waiuzie Tanesco Mitambo baadala ya kulipa fidia ya mabilioni bila mitambo.
  Kelele za kupinga ni za kisiasa zaidi ambazo zinakuwa Kama Chura ndani ya kisima ambazo hazimzui ng'ombe kunywa maji. Nadhani mwanasheria mkuu aliyepashwa
  kuishauri serikali kutovunja mkataba kukwepa consequences za kulitia aibu taifa ndiye awe Wa kwanza kujibu.
   
 3. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #3
  Feb 15, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,567
  Likes Received: 1,930
  Trophy Points: 280
  Msaidie president maana hawajui.
   
 4. M

  Mwera JF-Expert Member

  #4
  Feb 15, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hongera mkuu kwahakika umenena yale yaliyo moyoni mwangu,kwa hakika wewe unafaa kuwa mshauri wa rais ktk mambo ya maendeleo ya taifa hili,nakupa 100
  thanks,una mawazo makinisana.
   
 5. Avatar

  Avatar JF Gold Member

  #5
  Feb 16, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 676
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 35
  All in all... Mwisho wa siku ni kwamba hii mitambo Tanzania inaihitaji... Co kwaajili ya kumaliza tatizo lililopo sasa bali kwaajili ya mustakabali wa maendeleo ya taifa letu!... Hoja ya kusema NI BORA KUKAA GIZA KULIKO KUWASHA HII MITAMBO sikubaliani nayo kabisa!... Hadi leo hii kuna baadhi ya viwanda vimefungwa kwa ajili ya mgao, watu hawafanyi kazi Kwasababu ya mgao... Uchumi wa nchi hii unashuka sio suala la kukaa na kutoa hoja za kisiasa zisizoangalia uchumi wa nchi!...
   
 6. KICHAKA

  KICHAKA Member

  #6
  Feb 17, 2011
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 58
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ni Kichaa asiyekuwa na utambuzi anayeshabikia giza kwa kuwa tu baadhi ya watu wanataka kufurahi! Sisi ni kama wagonjwa na mgonjwa hachagui dawa, nadhani wenzetu hapa mnafurahia giza kwa kuwa hamna fedha za luku lakini kama mngalikuwa mnafukuzwa kazi kwa kuwa viwanda havizalishi na mkakosa mkate wa kulisha watoto wenu msingekuja hapa na kusema bora tukae gizani. Sijali umeme unazalishwa na nani lakini ni upuuzi kuacha kuwasha umeme uliopo etu kwa kuwa ni wa Dowans ambayo watu fulani humu wakiiona wanaona malengo yao kisiasa yanapata giza.
   
 7. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #7
  Feb 17, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,567
  Likes Received: 1,930
  Trophy Points: 280
  Who is DOWANS? Kweli waTZ wepesi wa kusahau.
   
 8. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #8
  Feb 17, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,201
  Likes Received: 1,005
  Trophy Points: 280
  Tunaihitaji sana hiyo mitambo tuiwashe ikiwa mali yetu kwa maana kwamba tuwe tumeitaifisha tayari.
  Halafu hii kitu inayoitwa dharura kwenye nchi yetu mimi siielewi inamaanisha nini kwa sababu toka 2002 inazungumziwa dharura mpaka leo ni 2011.
  Ina maana taifa letu ni la emergency.
  Kingine cha kujiuliza ni kwa nini wanaotaka mitambo ya dowans iwashwe wanataka kukaa na watu ambao muda wote wa sakata la richmond hadi dowans hawajawahi kujitokeza hadharani? Leo hii watawapata wapi ili wajadiliane?
  Hii ndio inayotia mashaka kuwa dawans ni mradi wa ccm wa kulipa fadhila za pesa ya uchaguzi 2005. Maana haiingii akilini kuwa megawatt 120 zimeshindikana kupatiwa ufumbuzi wa mpango wa kudumu toka 2002 hadi 2011.
  Serikali isitake kutuaminisha kwamba inaendeshwa kwa mashinikizo kana kwamba nchi haina kiongozi mkuu pale wanaposema ati kuna waliotaka mkataba uvunjwe ndio wa kulaumiwa. Kwani washikikizaji wanatoka chama gani?
  Kama mashinikizo yana nafasi katika uongozi wa nchi, nashauri kuwe na shinikizo la kuzuia mfumuko wa bei na kupunguza ukali wa maisha ili tuwezekufurahia shinikizo kwa mara nyingine tena.
  .
   
Loading...