Watanzania tunajua taifa letu halina mpasuko wa kisiasa, hakuna haja CCM kukaa meza moja na wapinzani wasio na uzalendo

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Wembe ni uleule, CCM ipo kutatua kero za wananchi na kuwaletea maendeleo wananchi.

Habari kuwa kuna wanasiasa walibaguliwa na kutengwa wakati wa utawala wa Hayati Magufuli ni kuleta porojo ambazo hazina mashiko.

Ni Mtanzania gani anataka umoja na wanasiasa ambao hawalitaki mema taifa lao kwa kila namna . Wapo tayari kuomba taifa lisipate msaada au litengwe bila sababu kisa tu maslahi yao yapatikane.

Taifa letu lipo madhubuti, kila mtanzania anajua Ccm ipo imara,japokuwa kuna changamoto. Habari za kutaka kukaa meza moja na Act wazalendo au Chademe ni kupoteza muda na rasilimali za watanzania.
 
Hilo nikwa mujibu wa ile gang ya ukanda pendwa wenye chatu wengi na Igudunde.
 
Wewe ni mbinafsi,usijiangalie wewe binafsi angalia pia kesho ya familia yako.
 
Dharau na kiburi na jeuri ndivyo vilipelekea mauaji ya kimbari ya Rwanda na Burundi.
Usijiulize, polisi, jeshi na vyombo vya ulinzi vilikuwa wapi?
Majira na wakati ukifika, hakuna atakayeweza kuuzuia muda
Acha mkwara mbuzi.
 
Acha mkwara mbuzi, Ccm inawafanyia makubwa watanzania.
 
Naunga mkono hoja, wapinzani wanachotaka ni kutupiwa makombo ili watulie. Kwenye serikali ya wanyonge tuliona wakipinga maendeleo. Huyu zito huwaga mtu wa kutafuta sana maslahi. Tunawajua wote walioshangilia kifo cha mzee, kamwe hamtapa unafuu wowote.
 
Makombora ya ugaidi,uchochezi, uhujumu uchumi na utakatishaji fedha sio, kwa mujibu wa wanakijani.
 
anajua Ccm ipo imara,japokuwa kuna changamoto.
Hizo changamoto ndio mpasuko wenyewe na unahitaji kuuponya kabla haujakua! Unasahau kuwa usipoziba ufa utaujenga ukuta?
Hii ccm mpya imeharibu kabisa misingi iliyoianzisha na ukiichunguza Sana utagundua kuwa lengo lake siyo kuujenga umoja na mshikamano aliouasisi Baba wa taifa Bali ukanda na ukabila aliouasisi mwendake!

Kila kabila na Kila Kanda inajipigania kisiasa na kiuchumi badala ya kupigania taifa!
 
Back
Top Bottom