Watanzania tunajifunza nini na mabadiliko yaliyotokea UK? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania tunajifunza nini na mabadiliko yaliyotokea UK?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mpenda Kwao, May 14, 2010.

 1. Mpenda Kwao

  Mpenda Kwao Senior Member

  #1
  May 14, 2010
  Joined: Apr 29, 2008
  Messages: 175
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hivi kweli Gordon Brown kachemsha zaidi kuliko JK hadi kufikia hatua ya kufanya uchaguzi? Nadhani inabidi watanzania tujifunze kutoka kwa wenzetu badala ya kuwa na desturi ya kusubiri hadi miaka mitano na mbaya zaidi tunampa miaka mingine mitano ya kuendeleza haya yanayotokea.
   
 2. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #2
  May 14, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,944
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Kwanza amewaambia wafanyakazi kuwa hawatapata kima cha chini kufikia 315,000.00 mpaka miaka 8 ipite, sasa huyu bwana si kesha chemsha n a kumwajiri tena ni kumpa nafasi ya kuchemsha zaidi.
   
 3. MANI

  MANI Platinum Member

  #3
  May 14, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,410
  Likes Received: 1,863
  Trophy Points: 280
  Ni wakati wa mabadiliko kwani madudu ya kwetu ni makubwa kuliko ya huko na wamebadili serikali.
   
 4. Mwita Matteo

  Mwita Matteo JF-Expert Member

  #4
  May 16, 2010
  Joined: May 16, 2010
  Messages: 216
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  tungkuwa nawatu wanaotazama mbele hata mwezi October usingefika.. tunanjia ndefu bado yakuwaelimisha ndugu zetu wajue kuwa kiongozi ni uchumi na sii madudu
   
 5. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #5
  May 16, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Wakuu kwanza mna takiwa kujua mfumo wa Uingereza ni tofauti na mfumo wetu sisi. Uingereza siyo kwamba hawa kusubiria waziri mkuu amalize miaka mitano ni kwamba Gordon Brown wakati wa kujiuzulu Blair hakuitisha uchaguzi kwa hiyo yeye alikua ana malizia term ya Blair kama kiongozi mpya wa chama cha Labor. Iwapo Brown angeitisha uchaguzi mwaka 2007 ange kuwa na haki ya kubaki waziri mkuu na kuitisha uchaguzi 2012 meaning ingekua 5 years. Pia tutambue kwamba Uingereza siyo mara ya kwanza chama cha upinzani kupata madaraka. Ni desturi yao tokea zamani na kwa wenzetu chama kuongoza miaka 13 kama livyo fanya Labor ni mingi sana.

  kwa hiyo ndugu wa Tanzania kila nchi ina sheria, katiba na tamaduni zake. Mambo mengine yanayo tokea nchi zingine hayawezi kuwa na uhalisia kwetu. Tuna bidi tuangalie sheria na mazingira ya kwetu yata kayo saidia kuleta mabadiliko. Hii mada ina jaribu kulinganisha mifumo miwili tofauti, watu tofauri wenye tamaduni tofauti. Yes we can make changes lakini siyo kwa mfano wa Uingereza. Mjadala ungekua na maana zaidi tunge angalia hali yetu sisi wenyewe na jinsi tunavyo weza kuitumia kwa faida yetu otherwise tutaendelea kuota ndoto za nchi zingine kila siku.
   
 6. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #6
  May 17, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,063
  Trophy Points: 280
  Ni vigumu kupata somo lolote lile kwa hivi sasa kwani hata waingereza wenyewe haijawahi kutokea hali kama hii. Muungano wa liberals na conservatives ni mgumu sana. Wakati Conservative ni mabwanyeye sana wakati liberals ni mrengo wa kati. Tuangalia mambo yatakavyo kwenda lakini nina uhakika serikali hii ya mseto haitadumu zaidi ya mwaka mmoja na uchaguzi mwingine kuitishwa.
   
 7. k

  kisikichampingo Senior Member

  #7
  May 17, 2010
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 129
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mabadiliko Tanzania yatakuja kwa mtindo wake. Inawezekana isiwe kama Uk, lakini Sisiem lazima watang'oka! Tunachojifunza ni kwamba, masultani hawatakiwi. Kwa mfano, 10 years kuwa rais ni miaka mingi sana. Tungefanya 7
   
 8. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #8
  May 18, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,063
  Trophy Points: 280
  Jee hao ccm wakibaki itakuwaje??????
   
 9. e

  echonza Senior Member

  #9
  May 18, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 163
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi unamaanisha hatuna la kujifunza kutoka uchaguzi wa UK? Si kweli, yapo mengi tu. Kwanza linatupa matumaini kwamba watu wakijitokeza kujiandikisha na kupiga kura kwa mjibu wa matakwa yao, siku ipo watapata viongozi wanaowahitaji kwa masilihi yao na ya nchi pia. Zaidi ni namna demokrasia inavyoweza kupewa nafasi bila kujali itikadi ya chama. Maana kwa uchaguzi huo wa UK Brown pia alikuwa na nafasi ya kutafuta vyama vingine ili aweze kufikisha idadi ya viti vilivyotakiwa kuwa majority (326). Lakini haikuingia akilini mwake kufanya hivyo, na kwa sababu ya uzalendo ndani ya kichwa na moyo wake ndiyo maana aliona hailipi kwake na nchi kwa ujumla na akachagua bora kujiuzuru uwaziri mkuu. Hivyo watanzania hapo tunajifunza uzaleno pia. Lingine ni Jinsi David (waziri mkuu mpya wa UK) alivyoingia madarakani na kwa kuona hali mbaya ya uchumi ilivyo, kaweza kujipunguzia mshahara ili kuokoa kiasi kiende kufanya shughuli za waUK.

  Tumeona mjadala ulivyopelekwa katika makubaliano katika kugawana madaraka kati ya Conservative na Social Democratic. Waoondoa tofauti zao kiilani za uchaguzi na kukubaliana kufanya kwa pamoja yaliyo na masilahi kwa taifa. Hivyo si kweli hatuna la kujifunza kutoka uchaguzi wa UK. Maana tukikaa na mawazo hayo aliyotoa mdau hapo juu itakuwa ni uvivu wa kufikilia na kulinganisha mambo. Ni kweli kwamba UK iko mbali sana nasi ukilinganisha kiuchumi na mfumo. Lakini yapo mengi tu ya kujifunza kutoka kwao. Kufanya maamuzi kisanyansi zaidi, nalo ni moja ya masuala muhimu sisi watanzania tunatakiwa kujifunza. Siyo maamuzi kama tunayoyasoma na kuyasikia mara nyingi yakifanya na viongozi wetu. Kesho anasimama huyu anaongelea kitu fulani, na kesho yake mwingine anaongelea hicho hicho lakini takwimu tofauti na aliyemtangulia kuliongelea suala fulani.

  Naimba uzalendo ni muhimu sana ikiwa ni pamoja na kuheshimu taaluma za watu waliopo kwenye mfumo pindi wanapotoa ushauri wao kuhusiana na kitu fulani kwa masilahi ya nchi.
   
Loading...