Watanzania tunajifunza nini kwa wenzetu wa Kenya? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania tunajifunza nini kwa wenzetu wa Kenya?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pax, Aug 27, 2010.

 1. P

  Pax JF-Expert Member

  #1
  Aug 27, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Kenya hatimaye imeandika ukurasa mpya katika historia yake, wenyewe wanasema new republic imezaliwa. Pamoja na mambo mengine wameondoa mikoa na kuleta majimbo ambayo yana madaraka ya kujiamulia mambo yake. Zaidi ni kuwa katiba yao imegusa mambo mengi ya msingi. Jambo kubwa nililojifunza ni kuwa wenzetu wa Kenya wanajua katiba yao. Je ni watanzania wangapi angalao wamewahi kuiona katiba yetu? Nimeshaisoma mara kadhaa katiba yetu na hakika pamoja na kwamba haikidhi mahitaji, ni kuwa haifuatwi. Inafuatwa pale tu viongozi wapotumia madaraka yao lakini yale wanayotakiwa kuwafanyia wananchi wao hawafanyi. Na kwa kuwa wananchi hawaijui katiba na hawajui hata haki zao basi ndio maana viongozi wetu wanawekaga viraka tu wakitaka.

  Wakenya wametuonyesha nini maana ya katiba kuwa ndio kioo cha kuleta maendeleo, bila katiba nzuri kuendelea ni ndoto.
   
 2. e

  ezechuku Member

  #2
  Aug 27, 2010
  Joined: Feb 2, 2010
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tunatakiwa kujifunza kenya ni kwamba wenzetu wakenya wanajua maana ya kupiga kura na umuhimu wa kura so watanzania tujaribu kubadilika
   
 3. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #3
  Aug 27, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Watanzania wengi ni sikio la kufa, halisikii dawa.
   
 4. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #4
  Aug 27, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Haki haijileti lazima idaiwe. Na kufanya hivyo kuna gharama.
   
 5. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #5
  Aug 27, 2010
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Afadhali tumesema wenyewe, wao wakituambia hivyo tunahamaki eti wametutukana!
   
 6. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #6
  Aug 27, 2010
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,858
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  kama tunataka katiba mpya Tanzania cha kwanza ni kuing'oa CCM itoke. Kenya wamefanikiwa kwa sababu hatua ya kwanza waliing'oa KANU, lakini chini ya utawala kandamizi wa CCM katiba mpya tusahau hadi kiama.
   
Loading...