"Watanzania Tunaishi Kwa Kudra Za Mwenyezi Mungu Tuu!"-Mhe. Dr. Faustine Ndungulile. Jee ni Kweli?.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,442
113,452
Wanabodi,

Asubuhi ya leo, nimepata fursa kuangalia TBC.

Naibu Waziri wa Afya, Mhe. Dr. Faustine Ndugulile yuko live TBC kwenye kipindi cha Jambo Tanzania.

Amesema "Watanzania hatuna utamaduni wa kupima afya zetu, mtu kwenda hospitali ni mpaka aumwe na kuandikiwa vipimo na daktari, hivyo tunaishi kwa kudra tuu za Mwenyezi Mungu!"- Dr. Ndugulile. Jee hii ni kweli?.

Dr. Ndugulile amesema kutokea kwa vifo vya ghafla kwa baadhi ya watu, kunachangiwa na watu wengi kuishi na magonjwa hatari yanayotibika bila wao kujijua, na kusema kunapofanyika upimaji wa jumla kwenye matukio mbalimbali, kuna mtu amekutwa na presha juu ya 200 na anadunda tuu bila yeye kujijua!.

Dr Ndugulile ametoa wito kwa Watanzania tujenge utamaduni wa kupima afya zetu kwa hiari mara kwa mara, na sio kusubiri hadi tuumwe, ndipo twende hospitali kupimwa na kutibiwa.

Dr. Ndugulile, pia alizungumzia mambo mengi makubwa mazuri ambayo serikali ya awamu ya 5 imeyafanya na inaendelea kuyafanya kuboresha sekta ya afya nchini.

Pia alizungumzia hali ya ugonjwa wa ukimwi na maendeleo ya vita dhidi ya ukimwi, amewasisitiza Watanzania kujitokeza kwa wingi na kupima afya zao kwa hiari na haswa wanaume. Wizara yake na taasisi za upimaji wa hiari, zimelenga kila mikusanyiko, na hata juzi kati kwenye mechi ya watani wa jadi, kulikuwepo na kambi ya upimaji wa hiari.

Pia Waziri Ndugulile aliwahakikishia Watanzania kuhusu ubora wa condoms za bure ni ubora ule ule sawa na condoms za kulipia, condoms zote zinazoingizwa nchini, zinapimwa kiwango cha ubora, hizo condoms za bure, zinatolewa bure kwa sababu kuna watu wamezilipia ruzuku, na sio za bure kwa sababu zina ubora hafifu hivyo hazina thamani, na zile condoms za gharama, zina gharama sio kwa sababu ya ubora, bali ni sababu za kibiashara tuu kwa kuongeza ladha, vikorombwezo na rangi mbalimbali ili tuu kuvutia mtumiaji lakini ubora wa condoms zote ni ule ule.

Pia Dr. Ndugulile alizungumzia baadhi ya changamoto za sekta ya afya na namna ya kuzikabili, changamoto kuu ni nguvu kazi, tuna wafanyakazi wachache kuliko mahitaji, na kutolea mfano wataalamu wa X-Ray ni wachache, hivyo sasa serikali imeanzisha Digital X-Ray machines ambazo, sasa X-Ray zitapigwa hospitali zote nchini na kutumwa kwenye a reading centre ambayo kutakuwa na wataalamu, na hapo hapo wanarudisha majibu kule ilikopigwa. Huu sasa ndio mwanzo wa Tanzania kufanya telemedicine.

My Take
Kwa maoni yangu, Dr. Ndugulile is good kwenye kujieleza, anafaa sasa awe awe waziri kamili, na waziri wake atafutiwe pengine pa kwenda. Ingekuwa na waziri wake ana uwezo kama huu, Watanzania wangeilewa vizuri zaidi awamu hii ya tano na mambo mazuri inayowatendea Watanzania kwenye sekta ya afya, such that come 2020, they will do the right thing.

Tufike mahali serikali yetu iendeshwe kwa proffesionalism, Waziri wa Afya awe MD, anamchukua mwanasheria na kumpa wizara ya Afya!, halafu naibu ndio MD, matokeo naibu ndio the right person wa kuelezea masuala la kiafya kuliko Waziri wake, a lawyer!.

Kama ilivyo kwenye wizara ya sheria, yuko mwanasheria bingwa, mambo ya ndani yuko polisi, Habari yuko mwanahabari, ulinzi alipaswa awe mjeshi etc. Kuwaweka mawaziri professionals kwenye technical ministries zinazohitaji professionalism kunaongeza productivity hivyo kuleta tija zaidi, kwa sababu sasa tunaelekea kwenye siasa za ukweli, politics of reality na sio politics of propanganda, tunapaswa, tuachane na siasa za propaganda, mabingwa wa kusema sana ndio wanateuliwa mawaziri, tuelekee kwenye politics of reality, ma professionals wenye kuonyesha uwezo wa delivery ndio wapewe vizara zinazohitaji professionals zao, na sio kwenye uwaziri tuu hata makatibu wakuu, mfano Viwanda na Biashara, yupo yule yule mkemia aliyasimamia ile Ph.D ya kemia, kama asante yake kwa kazi nzuri ya ile dissertation wakati tuna ma Ph.D holders kibao wa biashara. Tusiwateua watu kwa shukrani kwenye key technical, ministries na ukombozi wa taifa hili, lets give the key ministries to the key professionals and the best brains that we have halafu zile wizara za blah blah ndio unawaweka watu wa blah blah.

Jumatano njema.

Paskali.
 
naibu waziri kachemka kutoa hiyo kauli. anamaanisha kwamba kwenda hospitali kutatengua hizo kudra za Mwenyezi Mungu? hakuna hospitali yeyote inayotoa uhai duniani ndio maana hata nchi zilizoendelea wagonjwa wanakufa mahospitalini ambapo kuna huduma bora za afya, hivyo ni kudra za Mungu tu kwa mtu kuishi ama laa
 
Wanabodi,

Asubuhi ya leo, nimepata fursa kuangalia TBC.

Naibu Waziri wa Afya, Mhe. Dr. Faustine Ndungulile yuko live TBC kwenye kipindi cha Jambo Tanzania.

Amesema "Watanzania hatuna utamaduni wa kupima afya zetu, mtu kwenda hospitali ni mpaka aumwe na kuandikiwa vipimo na daktari, hivyo Tunaishi Kwa Kudra Za Mwenyezi Mungu Tuu!"-Mhe. Jee hii ni Kweli?.

P
Kumuona daktari tu kuna ada yake bado vipimo, madawa n.k., mshahara wenyewe haujapanda miaka mitatu, hiyo hela unaitoa wapi
 
Wanabodi,

Asubuhi ya leo, nimepata fursa kuangalia TBC.

Naibu Waziri wa Afya, Mhe. Dr. Faustine Ndungulile yuko live TBC kwenye kipindi cha Jambo Tanzania.

Amesema "Watanzania hatuna utamaduni wa kupima afya zetu, mtu kwenda hospitali ni mpaka aumwe na kuandikiwa vipimo na daktari, hivyo Tunaishi Kwa Kudra Za Mwenyezi Mungu Tuu!"-Mhe. Jee hii ni Kweli?.

P
Licha ya Sumaye kuwa waziri mkuu kwa miaka 10 lakini alisema hajui ni kwa nini Tanzania ni maskini, ujinga huohuo ndio anauleta huyu Ndugulile

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukweli hatuna tabia ya kucheki afya lkn in kusema hatuzifuatilii afya zetu swala la kudra zake Mola ni la wote hata yeye naudokta wake.
Lkn watu wakiwa na kipato kizuri wanaweza kujali afya na kupata muda was kuzicheki afya,maskini anakimbizana kutafuta chakula sio dawa. Amshauri mkuu wake wananchi wnahitaji kurahisishiwa chakula mavazi malazi kabla ya madege. Nchi watoto washule hawali wanapata vidondatumbo yeye anajisifu kununua ndege!? Tujitafakari jmn
 
Wanabodi,

Asubuhi ya leo, nimepata fursa kuangalia TBC.

Naibu Waziri wa Afya, Mhe. Dr. Faustine Ndungulile yuko live TBC kwenye kipindi cha Jambo Tanzania.

Amesema "Watanzania hatuna utamaduni wa kupima afya zetu, mtu kwenda hospitali ni mpaka aumwe na kuandikiwa vipimo na daktari, hivyo Tunaishi Kwa Kudra Za Mwenyezi Mungu Tuu!"-Mhe. Jee hii ni Kweli?.

P




Ni kawaida sana kukuta mtz wa miaka 60+ hajui hata group lake la damu.

Ni kawaida sana kukuta mtz wa 50+ akiwa hajawahi pima uzito wake since amemaliza clinic ya watoto chini ya miaka 5.

Wengi wa wanaopata Hypertensive strokes unakuta hajawahi katu kupima Blood pressure yake tangu ajitambue.

Tumesikia kuhusu katika umri gani tezi dume uanza ila badala ya kuchukua hatua tumeingia kwenye debates za sitaki kupigwa dole la kati, hamna kipimo kingine?.

Kwenye kupima Kisukari na HIV ndio usiseme.

Hata hivyo nawapongeza wanawake kwani mtazamo wao juu ya kutafuta huduma za afya ni chanya kuliko wanaume.
 
Back
Top Bottom