Ni ngumu kuingia akilini, mjumbe aliyepigania kufutwa kwa nafasi fulani ameteuliwa kushika nafasi hiyo hiyo akapiga goti na kushukuru kwa kupata nafasi adhimu!. Huu ni utumwa wa fikra sio njaa. Uhuru ni zaidi ya kutanua mdomo unavyotaka, kuamini unachofikiria, kuona unavyotaka, kwenda unakopenda. Uhuru ni pamoja na kuhoji na kutambua kwanini unasema, kwanini unafikiri na kwanini unaamini.
Watanzania bado ni watumwa wa fikra, hatuko huru hivyo itakuwa ngumu sana kuunda katiba huru na nzuri. Kama hata wale waliotuaminisha walisimama kwa miguu sio mioyo, walisema kwa midomo sio mioyo, waliona kwa macho yao sio mioyo yao.
Lini itatokea Tanzania mtu akateuliwa kushika nafasi fulani akakata kwa sababu nafasi hiyo inapingana na kile anachokiamini?