Watanzania tunahitaji kuondokana na zaidi ya mapacha watatu........ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania tunahitaji kuondokana na zaidi ya mapacha watatu........

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Vancomycin, Jun 3, 2011.

 1. V

  Vancomycin Senior Member

  #1
  Jun 3, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nimekuwa nikifuatilia vyombo vya habari,chama chao CCM na watu wengi wamekuwa wakiwazungumzia watu watatu ambao sasa wanajulikana kwa jina la mapacha watatu, wafukuzwe nafasi zao za uongozi na katika chama chao.

  Imekuwa ikizungumzwa kana kwamba hawa pekee ndiyo mafisadi,nakubali kabisa hawa ni mafisadi pengine wakuu lakini tunahitaji kuondokana na mafisadi wote.

  Ndugu zangu 'TUNAHITAJI TUONDOKANE NA CHAMA CHA MAPINDUZI"

  Mawazo yetu na malengo yetu isiwe mapacha watatu pekee tunahitaji kuondoa CCM kwa sababu wamefika mwisho hawana mawazo mbadala tena walichofanya kinatosha........

  CCM ni mti mzee umechoka matunda ni machache,si matamu tena ni wa kukata na kutupa........
   
Loading...