Ni ukweli usiopingika kuwa Watanzania tunayo hamu kubwa ya kupata katiba mpya. Lkn ni ukweli usiopingika kwamba CCM kama chama na si watu hawako tayari kuliona tamanio hilo likitimia!!
Nimeamua kuna na hoja hii baada ya vilio vya hivi karibuni vya wana wa UKAWA kufuatia kipigo kikali kutoka kwa wana wa CCM japo bado siamini kama katiba ya sasa ndio iliyosababisha kipigo hicho. Lkn mwisho wa siku Watanzania tunahitaji katiba mpya ambayo itakuwa imerekebisha mambo mengi yakiwemo ya uchaguzi n.k.!
Lkn tatizo ninalo liona ni kuwa pamoja na kuwepo matamanio hayo, bado wana hawa Watanzania wanakosa mtu kwenye nia ya dhati ya kuwaongoza kuhakikisha tamanio hili linatimia! Kwanini?
Mwaka 2010 Mara baada ya uchaguzi CDM walibeba jukumu hhili, mapingamizi yalianza mapema kabisa akianza waziri wa sheria wa wkt huo mama Cellina Kombani( mungu amrehemu) yeye alisema hatuhitaji katiba mpya Bali iliyokuwepo ilikidhi mahitaji na kama ingetokea bac ingepigwa vilaka tu!
Cellina kombani alikuwa waziri wa sheria tamko lake lilimanisha tamko la serikali, yaani huo ndo ulikuwa msimamo wa JK na serikali yake. Lkn CDM wakiungwa mkono na makundi mabalimbali ya kijamii hawakukata tamaa, nakumbuka nkwenye moja ya vyuo vikuu pale Dodoma kwenye moja Gobless Lema ktk tukio moja alituongoza kufanya maandamano kabla ya kukutana na kipigo cha Police. Hatukuwa tumejali uwezekano wa kupigwa na Police kwa sababu tuliona katiba mpya kama jambo lenye maslahi kwa taifa, hatukuangalia nani aliyekuwa anatuongoza bali tuliangalia nia thabiti ya huyo!
Baada ya pressure kuzidi hatimaye Jakaya Kikwete alimgeuka Waziri wake na wanaCCM wengine wengi, akatangaza mchakato wa katiba mpya. Nimeanza na utangulizi huu mrefu kuonyesha kuwa jambo hili halikuja kirahisi na hatuwezi kufika hapo tunapotamani kirahisi.
Tofauti na mwanzoni ambapo tatzo lilikuwa kwa wahafidhina wa CCM safari hii limeongezeka tatzo lingine, ni kwamba hatuna mtu wa kusimama na kutuongoza katika mapambano hayo ambayo kama nilivosema so mepesi! Kwanini!?
Wote tunajua jinsi uchaguzi wa mwaka Jana ulivoacha vurugu katk vyama vyetu, kuanzia CCM hadi CUF, vurugu hizo zimesababisha watu kujikuta wakiwa ktk maeneo wasiyositahili huku wengine wakiondoka ktk maeneo wanayostahili.
Uchaguzi umetupa raisi ambaye ameweka wazi kuwa kwake katiba mpya si kipaumbele, ikumbikwe Rais aliyepita aliunga mkono hoja ya katiba mpya kabla ya kutugeuka dakika za mwisho baada ya kuwekwa kikaangoni!!
Wote tunajua nguvu za rais chini ya katiba ya sasa hvo kulazimisha kupata jambo asilolitaka linahitaji kuwa na viongozi kwenye nia thabiti, je tunao hao?
Lkn pia uchaguzi huo umewaingiza baadhi ya watu waliokuwa wakitegemewa ktk upatikanji wa katiba mpya ndani ya serikali, serikali ambayo katiba mpya si kipaumbele, hawa hawawezi tena kuthubutu kuwa mstari wa mbele!!!
Lkn upande wa pili nako hali si shwari, CDM ile, CUF ile sasa hazionekani, hawa simu hizi wanaweza kupigwa mkwara na Paul Makonda na wakanywea.
Kibaya zaidi watu walioikata hadharani katiba ya Warioba, watu ambao ushahidi wa wazi unaonyesha dhahili walishiliki kikamilifu kuhakisha katiba ya Warioba inakwama,sasa ndo vinara wa upande huu, bahati mbaya yangu tuwakaribishe hawajawahi kutuomba msamaha juu ya Yale waliyotenda wakiwa Kyle, hawajawahi kutoka hadharani na kusema sasa wana msimamo gani juu ya katiba mpya!
Hawa wanaonekana wakitumia nguvu nyingi sana kuelekea uchaguzi wa 2020, hawataki kuangalia mstakabali wa nchi kwa mda mrefu kama ss tunavyoangalia, hawa wakija na kelele za katiba mpya hawezi tena kuaminiwa, rekodi zao zipo wazi na hata tukiacha rekodi zao matendo yao yanatuonesha wanangalia 2020 hivyo hata wakipiga kelele za katiba mpya wengi tutashindwa kuwaamini, kwa sababu ukweli ni kuwa watakuwa wanazitumia kama mwavuli tu wa 2020, HAWA HATUWEZI KUWAAMINI HATA KIDOGO na hawana legitimacy tena ya kubeba jukumu hilo, uchu wa kuingia magogoni 2015 umewaondolea uhalali huo!
Kule CUF ndo usiseme wanashinda mitandaoni wakiitana majina ya ajabu ajabu kweli.
Zitto anaoeneka anaweza kulibeba jukumu hilo, tatzo hawa wengine watakubali ajipatie ujiko huo?, chama chake kina watu na rasilimali za kulisimamia hilo!?
Hebu ona NGOS nazo ziko hoi, hawa nao kama wanachungulia kwanza wenzao waanze wao ndo wanajifanya kupiga kelele, labda TLHRC wangeweza kutusimamia, lkn Yule mama namuona mwepesi mno, akipigwa mkwara mdogo ananywea, lkn sioni kama kuna Manpower yanye weledi na moyo wa uzalendo pale inayoweza kusimama naye hata kama angethubutu!
Deus Kibamba wa jukwa la Katiba anoaonekana mtu strong, lkn NGO yake sioni kama ina nguvu za kutosha( fund na manpower), mmmmhhhh!!!
Nikasema bac vyombo vya habari, thubutuu!!
Huku nako mambo si mambo, baada ya uchaguzi huku wameamua kuchagua pande, ss wametuacha, sasa wanapiga ngoma za wanaowalipa!
Kinachobaki ni sisi Watanzania kubaki na matamanio yetu, huku tukiomba kudura za Allah atokee shujaa wa kujitoa mhanga na kutuongoza ktk kutimiza haja yetu hii mhimu, "KUPATA KATIBA MPYA"