mareeTZ
Senior Member
- Jun 4, 2015
- 171
- 179
Moja kati ya mambo yaliyonihuzunisha ni tukio la kuchaguliwa na kuapishwa kwa mkuu wa tume ya uchaguzi. Yani walikuwa wanacheeeeka, wameshatuweza..... Miezi kadhaa tu iliyopita wakenya walipoteza maisha na kumwaga damu wakidai tume huru ya uchaguzi na wakaipata. Katiba hii iliyopo vifungu vingi vilitungwa na mkoloni kwa ajili ya kumnyonya mwafrika Leo hii mwafrika anatumia vifungu hivi hivi kumnyonya mwafrika mwenzie inauma.
Leo hii tuna viongozi wasiosubutu kunyanyua ndimi zao kuhoji wakihofia kutumbuliwa.wamebaki kusifia tu kila kitu. Inauma.
Leo hii bunge halina nguvu ya kuwajibisha serikali inapokosea kwa kuogopa vitisho vya mtu mmoja inaumwa.
Leo hii kijiji kidogo cha chato kinajengwa moja ya Airport kubwa tanzania ilhali wanafunzi hawana mikopo, wafanyakazi hawajaongezwa vyeo na mishahara, vijana wametoswa kwenye ajira huku wakidaiwa na bodi inauma.
Tunanunua tu ndege hakuna kiwanda walichojenga. Hivi kwanini kwenye kampeni wasingesema Tanzania ya ndege? Mtu unayesema ndege zutakuza utalii kwa taarifa yako asilimia 90 ya abiria watategemea wazawa yani hii ni sinema. Inauma.
Katiba mpya itapunguza madaraka ya Raisi, itaruhusu tume huru ya uchaguzi, inataka serikali tatu... Kamwe hawezi iruhusu.