Watanzania tuna maswali ya kujiuliza kuelekea 2015 kama kweli tunaitakia mema nchi yetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania tuna maswali ya kujiuliza kuelekea 2015 kama kweli tunaitakia mema nchi yetu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by luckman, Oct 29, 2012.

 1. l

  luckman JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Ni muda sasa umepita nchi ikiwa imevamiwa na wimbi kubwa la majangiri yanayoojiita viongozi, yamebadilisha sheria za nchi na kuziweka chini yao, yamebadilisha mifumo yote na kuifanya fursa za biashara zao, yameuza mali zetu kwa manufaa yao na familia zao, nchi imebaki na ukiwa, nchi inayumba, nchi imekosa mtetezi, hata wale tunaowaita wasomi nao wamekuwa mbayuwayu, wana sura za uelevu ila ndani mioyo yao na matumbo yao vinaonekana kukosa mizizi kitu kinachoashiria elimu ya nchi imehasiwa kwa kiasi kikubwa.

  Naomba nimuongelee kidogo tu huyu jamaa anayejii Edward Lowassa,

  Huyu jamaa nadhan walio wengi watakuwa hawamjui vizuri, bali wanamfahamu tena juujuu,

  Huyu ndo mtu aliyechangia kwa kiasi kikubwa sana kufirisi hii nchi, ni mtu ambaye ni mwenye tamaa za hali ya juu na mroho wa mali na madaraka, amefanikisha mipango mengi sana ya kuibia nchi Tangu akiwa mkurugenzi wa AICC HADI HAPA LEO alipo, akiwa anaitwa waziri mkuu mstaafu wakati alijiuzulu na hii imefanywa makusudi ili aendelee kulipwa 80% ya mshahara wake wakati anajua fika hastahili kulipwa, huruma yake iko wapi? hiyo sio issue hali ni tabia yake lakini naomba tujiulize.

  Nchi hii inateswa na viongozi walioingia kwenye madaraka kwa ghalama kubwa sana na mwisho wanashindwa kuleta maendeleo katika nafasi zao kwani muda mwingi wanakuwa wanashughulika na mambo yao na jinsi ya kurudisha capital zao kwani siasa siku hizi imekuwa na biashara,

  Huyu mzee Lowasa mmiliki wa makampuni ya ALFA-( SHULE, KAMPUNI ZA UJENZI, MWANAHISA WA VODA,...........) Tumemuona akiwa katika harakati za kuingia ilkulu,amehusishwa sana na rushwa nyingi sana kwenye chaguzi zote ndani ya ccm, amehusishwa sana na rushwa kwenye taasisi za dini lakini tujiulize.

  #haya yote na ghalama zote anazotumia kupata upenyo wa kuingia ikulu je anachokitafuta ni nini?#

  Tusipoangalia, tutalangua hii nchi, tutamtafuta nabii tumpate hitler, tutauziwa hadi mama zetu na wazee wetu, tumkumbuke nyerere na tuwe karibu nae, hakika atatusaidia kwa mawazo yake.

  mUngu ibariki Tanzania.
   
Loading...