Watanzania tuna kila sababu kumshukuru Mungu kwa kutuletea Rais Mkali

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,367
Kikwete alikuwa kiongozi bora lakini aliponzwa na upole wake.

Magufuli ni Rais Bora zaidi na ana kitu cha ziada ambacho ni ukali, busara, hekima, utulivu, uvumilivu, ujasiri, uwajibikaji, ubunifu na umakini.

Hizi ni ni sifa muhimu sana kwa mustakabali wa taifa letu ambalo lilijaa wazembe wengi, majizi, majambazi, mafisadi na kila aina ya ufedhuli.

Sasa Rais anainyoosha nchi na inanyoosheka japo mikunnjo kwenye baadhi ya maeneo hazikosekani.

Watanzania Tumshukuru Mungu kutuletea Rais wa aina hii na tuna kila sababu kumuombea usiku na mchana ili atimize ndoto zake za kuifanya Tanzania kuwa Donor Country na nchi ya viwanda.

Sio siri kwa sasa watu wanawajibika.

Leo hii wananchi wanakuwa na ujasiri wa kueleza kero zao hadharani bila ya kuogopa kushughulikiwa na viongozi na watendaji wa Serikali.

Leo hii viongozi wanajiuliza mara mbili mbili na kutafakari kwa kina kabla ya kufanya maamuzi.

Taifa linanyooka. Linaenda kwenye mwelekeo mzuri. Hii yote sababu ya ukali wa Rais.

Ukali unasaidia na unalipa
 
Nabii Suleimani aliomba Mungu ampatie Busara na Hekima , na si ukali..
Uwe unatafakari kile utakacho kuja kutype.. Good Leader create Leaders, Bad Leader create Followerz
 
Kikwete alikuwa kiongozi bora lakini aliponzwa na upole wake.

Magufuli ni Rais Bora zaidi na ana kitu cha ziada ambacho ni ukali, busara, hekima, utulivu, uvumilivu, ujasiri, uwajibikaji, ubunifu na umakini.

Hizi ni ni sifa muhimu sana kwa mustakabali wa taifa letu ambalo lilijaa wazembe wengi, majizi, majambazi, mafisadi na kila aina ya ufedhuli.

Sasa Rais anainyoosha nchi na inanyoosheka japo mikunnjo kwenye baadhi ya maeneo hazikosekani.

Watanzania Tumshukuru Mungu kutuletea Rais wa aina hii na tuna kila sababu kumuombea usiku na mchana ili atimize ndoto zake za kuifanya Tanzania kuwa Donor Country na nchi ya viwanda.

Sio siri kwa sasa watu wanawajibika.

Leo hii wananchi wanakuwa na ujasiri wa kueleza kero zao hadharani bila ya kuogopa kushughulikiwa na viongozi na watendaji wa Serikali.

Leo hii viongozi wanajiuliza mara mbili mbili na kutafakari kwa kina kabla ya kufanya maamuzi.

Taifa linanyooka. Linaenda kwenye mwelekeo mzuri. Hii yote sababu ya ukali wa Rais.

Ukali unasaidia na unalipa
Rais gani asiyeee itiii katiba. Anasigina katiba halafu unamfagilia. Mmmmmh
 
Ogopa rafiki mnafiki anaye kukumbatia, kukusifia na kukuchekea huku anakumwagia sumu Kali , wewe Eliza ni mnafiki tena mkubwa , unamsifia rais wako hiari unaona uchumi unayumba, hali inazidi kuwa mbaya kila kukicha. Sisi tunahitaji rais anayeongozwa na kuilinda katiba sio hisia.
 
Ndo maana mnaitwa ma.sh.oga maana hata ujinga mtatetea tu.Jaribu kutumia akili wakati mwingine,bwana uyo mpaka sasa kafanya nini cha kusifia kama siyo upuuzi mtupu.Nataman na mimi nipewe ndo.to kama ya Lema juu ya mtu uyo uyo.
 
Ukali sio sifa ya kiongozi, ukali ni hasara kubwa kwa kiongozi. Kiongozi bora hatakiwi kuwa mkali, anatakiwa kuwa na busara na hekima. Ukali ndio uliofanya mfalme akashonewa nguo isiyoonekana. Fundi aliogopa kumwambia ukweli kwamba hakuna nguo isiyoonekana kwa sababu ya ukali wake. Mfalme akavaa nguo isiyoonekana na akatembea akiwa uchi kabisa. Hakuna aliyethubutu kumwambia yuko uchi mpaka mwendawazumu alipopiga kelele kwamba mfalme anatembea uchi. Hizo ndizo hasara za ukali. Hapa kwetu tuna uhakika wa kumpata mwendawazimu atakayemwambia mfalme uko uchi atakapotembea uchiìi??
 
Watu humu wana Stress za maisha magumu, hawana pesa mfukoni, sasa ukiwaambia hizi habari hawawezi kukuelewa.

Rais ongeza Ukali, naona umepunguza sana Ukali.
 
Watanzania gani unazungumzia wewe!!Acha kugeuka msemaji wa wengine bhana..Me binafsi mpaka sasa najiuliza ameletwa na nani?Na aliyemleta hakika alaaniwe...
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom