Watanzania tumwombe Mungu sana maana inaonekana tunakoelekea siko

ZEE LA HEKIMA

JF-Expert Member
Aug 10, 2015
1,417
1,839
Wakati unapotokea ukame Watanzania wa dini zote wanamwomba Mungu na mvua inanyesha. Hali tuliyonayo sasa ni mbaya sana kuliko ukame mkali. Tunaelekea kuwa Tanzania ya kubaguana, chembechembe za ukabila zinaonekana, uonevu umeibuka na utu unaonyesha kutoweka. Kama utu haujatoweka kwa nini watu ambao nyumba zao zinatakiwa zibomolewe wasipewe angalau siku tatu ili waondoe vifaa vyao vya nyumbani? Kwani hata kama tarehe za notisi zimepita siku tatu za ziada kweli zitachelewesha ujenzi wa reli kwa kiasi kikubwa mno? Hebu viongozi wa dini na Watanzania wote, tumwombe Mungu ili matendo yanayozua chuki mioyoni mwa watu yasiwdpo
 
Back
Top Bottom