Watanzania tumtumieni Rais Magufuli vizuri, Akiondoka tutamkumbuka sana

Kwa kweli moja kati ya vitu ambavyo hatutakuja kumsahau ni

Bomoa bomoa kwa wakazi wa kimara na mbezi watu wengi wamekufa kwa presha
Ni kweli kupoteza makazi kunatia Presha ila watu walifuata barabara kulikuwa hakuna namna zaidi ya kuwatoa wapishe maendeleo.Kama wanahisi hawakutendewa haki wanaweza kufungua kesi mahakamni kudai haki yao.Au hamkupenda barabara itengenezwe ipendeze?
 
Najua kuna watu ambao hawataelewa ninachotaka kusema ila wacha niseme tu.

Tangu wamau ya kwanza watu wamekuwa wakisubiri tu siku watakapopata kiongozi bora atakayeleta neema.Enzi za baba wa taifa watu hawakumtumia vizuri alipoondoka akaja Mzee ruksa akafanya yake naye watu hawakumtumia vizuri akapita akaja Mzee Mkapa,kisha Kikwete na sasa Magufuli.

Viongozi wote hao walikuwa na mazuri na mapungufu yao ila sasa wengi wetu badala ya kutumia yale mazuri yao vizuri ila kuhakikisha tunapiga hatua kati a maisha yetu na taifa letu tulifanya makosa tunayofanya sasa ya kubeza bila kutumia fursa zilizopo

Niseme tena jamani watanzania,Rais wa sasa ndo huyu, changamoto zake tumezijua na fursa zake tumeziona kwa hio basi ili tusonge mbele ni vyema tukamtumia ipasavyo.Kama tuna mambo tunataka yanyooke katika biashara, sheria, haki, uchumi n.k. na ambayo hayana majungua majungu na kejeli basi ni wakati wa kuyafikisha kwake kwa njia yoyote ile ili ayafanyie kazi.

Kama ni suala la elimu basi tujenge hoja ya kile tunataka kifanyike kuboresha elimu yetu na kwa hakika atachukua hatua.Kama ni huduma za afya, ulinzi na usalama,mawasiliano,biashara,uchumi n.k..tuseme kwa nguvu kubwa na sauti kubwa kile tunachotaka ambacho kitafanya maisha yako,ya watoto wako na taifa kwa ujumla wake liwe bora zaidi tuseme.

Kama kuna kero ya barabara mtaani kwenu simameni kwa pamoja mseme,jengeni hoja tumieni mitandao ya kijamii kuonesha tatizo na kushauri nini kifanyike na Rais wetu atafanya.kama ni tatizo la ajira jiungeni pamoja,ibueni miradi semeni changamoto zenu na rais wenu atafanya.Narudia tena kusema kwamba MTUMIENI HUYU MZEE KABLA HAJAONDOKA KWANI MTAMKUMBUKA SANA.

Msikae tu ksema kuhusu madhaifu yake na kumfrustarte kwa sababu ana ngozi laini kwa sababu hiyo haitaleta maendeleo yoyote.Narudia tena ibukeni semeni kila mnachotaka na mpendwa wetu JPM atafanya. Akiondoka Mtamkumbuka kwani hamjui ataekuja baada yake atakuwa na wajihi gani.

Mimi nimesema tu kwa atakenielewa anajua nini cha kufanya kwa wale ambao wanafikiri kila kitu ni siasa au mapenzi piteni kimya wala msisome huu uzi wa la kuchangi ila kwa wale mnaojua maana chukueni hatu mapema kwani akiondoka ni vigumu kumpata mwingine kama yeye na kwa hakika mtatamani arudishwe ila ndo basi tena awamu yake itakuwa imepita.

Wenu

SM
Wamau.....ndio mnyama gani?
 
Mkuu swala la Tundu Lisu bado halijathibitika kwa hakika ni nani waliohusika.Binafsi nafikiri inawezekana kabisa waliofanya hivyo walitaka ionekane kwamba ni serikali ilifanya tukio hilo.Kulikuwa na njia nyingi za kumnyamazisha bila kutumia nguvu kubwa ila kwa sababu lengo lilikuwa kuleta taharuki waliamua kutumia mbinu hio chafu.Ni namna moja ya kulitazama hilo

Mbona hawataki uchunguzi huru?
 
Mbona hawataki uchunguzi huru?
Uchunguzi huru wa kuchunguza nini?Unafikiri polisi hawajafanya uchunguzi?Tatizo hawajafanya arrests kwa sababu hakukuwa na taarifa za kuwawezesha kuanza uchunguzi zaidi ya hisia tu kwamba ni serikali.Iwapo Lisu atarejea nchini naamni kabisa kwamba atatoa mwanga wa yaliyojiri siku ya tukio na wahusika watatiwa nguvuni
 
Alikuwa Nairobi hapo na akasema polisi anayetaka ushirikiano wake aende, hakuna aliyekwenda. Hata huko Ubelgiji kama nia ipo yuko tayari na ni nchi ambayo tuna balozi wetu. Kwenye hili bora ukae kimya tu boss.
 
Wafanyabishara gani ambao hawajalipwa na serikali?Wale ambao wanato rushwa ili wapate tender kisha wanatoa huduma ambazo ni substandard kwa sababu wana wau wao kwenye system na kisha wanpobanwa ndo wanaanza kudai kwamba serikali inataka kuwadhulumu?

Kutoa na kupokea rushwa ni kosa kisheria. Kwa nini wasikamatwe na kushtakiwa? Sasa hivi nawafahamu wafanyabiashara wanne ambao wanaidai serikali na wamebambikiwa madai ya kodi kukata malipo yao ili kufidia madeni hewa ya kodi (hazina ilitoa waraka namba 4 wa mwaka 2019 unaozitaka taasisi za serikali kutomlipa mfanyabiashara bila kuwasiliana na TRA).
 
Mkuu mbona watu wanapewa increments za performance na kupandishwa madaraja kama kawaida?Ambacho ameondoa ni ilie ya kupandiha kima cha chini cha mshahara ambayo ilikuwa inasukuma sana inflation.Kama kuna uongo kwenye hili naomba mfanyakazi yeyote wa serikali aseme hapa kama watu hawapandishiwi mishahara kwa kutumia madaraja na utendaji kazi.

Unajua maana ya salary increments?
 
Ndio rais wako utafanyeje umpende usi mpende ndio rais wako lete fyokofyoko hadharani kama kweli una rais mwengine
Nimesoma kichwa cha habari tu,utumbo wa ndani wa tumbo la kuhara sijausoma ila nikujibu tu kwamba HATUMTAKI MAGUFULI.
Ieleweke tu kwamba si kiongozi sahihi wa taifa hili hana maono,jana anazungumza eti world bank watatupa mkopo kwa sababu anazozijua na anaongea kwa vijembe baada ya masaa kadhaa world bank wanamjibu na kumwambia kuwa mkopo wamesitisha kwa sababu ya sera zake.
Harafu mtawazaji wake unakuja na kuleta uhalo hapa kwendaaaaaaaa.
2020 No Magufuli.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Najua kuna watu ambao hawataelewa ninachotaka kusema ila wacha niseme tu.

Tangu wamau ya kwanza watu wamekuwa wakisubiri tu siku watakapopata kiongozi bora atakayeleta neema.Enzi za baba wa taifa watu hawakumtumia vizuri alipoondoka akaja Mzee ruksa akafanya yake naye watu hawakumtumia vizuri akapita akaja Mzee Mkapa,kisha Kikwete na sasa Magufuli.

Viongozi wote hao walikuwa na mazuri na mapungufu yao ila sasa wengi wetu badala ya kutumia yale mazuri yao vizuri ila kuhakikisha tunapiga hatua kati a maisha yetu na taifa letu tulifanya makosa tunayofanya sasa ya kubeza bila kutumia fursa zilizopo

Niseme tena jamani watanzania,Rais wa sasa ndo huyu, changamoto zake tumezijua na fursa zake tumeziona kwa hio basi ili tusonge mbele ni vyema tukamtumia ipasavyo.Kama tuna mambo tunataka yanyooke katika biashara, sheria, haki, uchumi n.k. na ambayo hayana majungua majungu na kejeli basi ni wakati wa kuyafikisha kwake kwa njia yoyote ile ili ayafanyie kazi.

Kama ni suala la elimu basi tujenge hoja ya kile tunataka kifanyike kuboresha elimu yetu na kwa hakika atachukua hatua.Kama ni huduma za afya, ulinzi na usalama,mawasiliano,biashara,uchumi n.k..tuseme kwa nguvu kubwa na sauti kubwa kile tunachotaka ambacho kitafanya maisha yako,ya watoto wako na taifa kwa ujumla wake liwe bora zaidi tuseme.

Kama kuna kero ya barabara mtaani kwenu simameni kwa pamoja mseme,jengeni hoja tumieni mitandao ya kijamii kuonesha tatizo na kushauri nini kifanyike na Rais wetu atafanya.kama ni tatizo la ajira jiungeni pamoja,ibueni miradi semeni changamoto zenu na rais wenu atafanya.Narudia tena kusema kwamba MTUMIENI HUYU MZEE KABLA HAJAONDOKA KWANI MTAMKUMBUKA SANA.

Msikae tu ksema kuhusu madhaifu yake na kumfrustarte kwa sababu ana ngozi laini kwa sababu hiyo haitaleta maendeleo yoyote.Narudia tena ibukeni semeni kila mnachotaka na mpendwa wetu JPM atafanya. Akiondoka Mtamkumbuka kwani hamjui ataekuja baada yake atakuwa na wajihi gani.

Mimi nimesema tu kwa atakenielewa anajua nini cha kufanya kwa wale ambao wanafikiri kila kitu ni siasa au mapenzi piteni kimya wala msisome huu uzi wa la kuchangi ila kwa wale mnaojua maana chukueni hatu mapema kwani akiondoka ni vigumu kumpata mwingine kama yeye na kwa hakika mtatamani arudishwe ila ndo basi tena awamu yake itakuwa imepita.

Wenu

SM
Mambo mengi sana yanayo isambaratisha Tanzania kutoka utawala wa Magufuri, ila nitataja 12 tu;
1. Ni mropokaji kwa kuwa anapoongea hajali kadamnasi imayomsikia. Matusi ya nguoni ndiyo lugha yake ya kawaida.

2. Hapendi upinzani kwa kuwa akiruhusu atashindwa asubuhi. Ndiyo maana katumia hela ya Serikali kuwanunua wabunge wa Kinondoni, Siha na Bahati.

3. Anapenda rushwa na ufisadi ndiyo maana hataki kufanya kazi na CAG aliye nyooka.

4. Ni mwizi wa mali ya umma ndiyo maana kamuweka Katibu Mkuu Hazina ambaye ni mpwa wake. Kwa miaka 4 tayari Tsh 2.4 Trillion hazijulikani zilipo

5. Ni mpenda ukabila kwa kuwa sehemu nyeti zote amejaza ndugu na watu wa Kanda ya ziwa Angalia IGP, DPP, AG, KM-KM-Hazina, RC DSM, Waziri Nishati, CAG mpya, Waziri Viwanda, Jaji Mkuu nk

6. Ni mtu wa kufuja mali ya umma. Angalia ujenzi wa uwanja wa ndege wa Chato na uanzishaji wa mbuga ya Burigi -Chato

7. Amezuia shughuli za vyama vya siasa wakati CCM inafanya mkutano kila mahali. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 toleo la mwaka 2000 na Sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992 zinatambua shughuli za vyama vingi.

8. Hataki watu wajieleze kwa uhuru kadri ya katiba, na amevibana vyombo vya habari. Kwa mfano Eric Kabendera ameanzishiwa shitaka la kutakatisha fedha wakati kiukweli ni maoni yake kwenye gazeti la The Economist

9. Anachukia wenye vyeti feki lakini kamuacha Bashite aendelee kuwa RC DSM wakati naye ana cheti feki. Hata PhD yake yasadikiwa amekopi kwa supervisor wake ambaye kamteua kuwa Katibu Mkuu wa Wizara mojawapo.

10. Ameruhusu kikundi cha wasiojulikana kiteke watu, kuwatesa na wengine kuwaua kama Ben Saanane, Azory Gwanda. Na majeruhi kwa Tundu Lissu

11. Analitawala Bunge kwa remote control. Bunge haiwezi kuhoji chochote kilichofanywa na Serikali.

12. Mahakama nayo iko mfukoni mwake. Yeye ni Polisi, kuendesha mashtaka na Hakimu
 
Mkuu kwenye kodi,watu walikuwa hawalipi kodi,wanafanya biashara kwa ujanja ujanja na kukwepa kulipa kodi kubwa huku wakihonga watumishi wa TRA.Yeye kaamua kwamba kila mtu alipe kodi ili nchi ipate mapato halali sidhani kama unaelewa hilo mkuu.

Serikali zilizopita zilikuwa zinapata wapi fedha kuendeshea shughuli zake kama wafanyabiashara walikuwa hawalipi kodi? Mgodi mmoja tu wa Nyamongo (ambao wakiwa kwenye peak ya uzalishaji kabla ya kuzuiliwa kusafirisha mchanga nje) walikuwa wanalipa PAYE zaidi ya billion 30 kwa mwezi. Sasa hivi hata billion 3 hazifiki, umakini wa Magufuli upo wapi?
 
Back
Top Bottom