Watanzania, tumpongeze Yusuf Manji kwa kuwa mzalendo na kurudi nyumbani. Rais Samia asichelewe, amuite Ikulu wazungumze

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Feb 26, 2018
2,490
3,534
Habari wadau!

Kuna siku nilishawai ku comment humu kwamba uwepo wa mfanyabiashara Yusuf Manji una umuhimu mkubwa sana katika Taifa hili, hivyo nikashauri Mama Rais Samia Hassan amuombe Manji arudi, hatimaye sasa Manji amerejea nyumbani.

Hakika Manji ni Mtanzania mzalendo. Yaani licha ya yote yaliyomkuta na kukaa ughaibuni miaka mingi bado hakusahau nyumbani na sasa amerudi kuwekeza nyumbani.

Kwa wasiomjua Manji watabeza lakini huyu mtu ni muhimu sana katika kipindi kama hichi ambacho Rais Samia anataka kuboresha ueekezaji, kukuza uchumi na kutekeleza ilani ya chama kwa kutoa ajira million nane.

Sasa ni muda wa mama Rais Samia Hassan kumuita Manji Ikulu na kumsikiliza ana changamoto zipi ili serikali imsaidie aweze kuwekeza tena nchini.

Manji pia ni mpenzi mzuri wa mpira wa miguu ila kwa pande huu sitaki kumsemea.

Karibu sana nyumbani Mtanzania mzalendo Yusuf Manji.
 
Ukiahidiwa usalama wako na waziri au rais utakua na amani na ahadi ya yupi?
Usalama?

Ngoja tutafakari haya yafuatayo:

kwani yeye ana shida gani na vyombo vyetu vya ulinzi na usalama? Je wafanya biashara wote walipiga hodi ikulu ili kutamkiwa na kuhakikishiwa usalama na rais? Yeye ana upekee upi ambao inalazimu rais amhakikishie usalama?
 
In fact Manji sio muwekezaji, ni mwizi.

Magufuli made a lot of terrible decisions lakini kwa Manji Magufuli was right, he did the good thing.

Kama ingekua inaruhusiwa ku disclose facts kama court cases and disputes za taasisi za serikali ambazo Manji alilipwa hela na akagoma kutoa huduma, billions of Money humu, mtampiga mawe Manji.

Ndio maana Manji alikua na team ya wanasheria zaidi ya 50 kutoka nchi mbalimbali ili kujilinda na kumlinda dhidi ya wizi wote aliokua anafanyia taasisi za serikali.

Manji sio muwekezaji, ni mwizi.
 
Mimi naona hata asipolipa kodi sawa ,kama akiweza kutoa ajira million 8 ,ambazo hizi takataka ccm zimekuwa zikitoa ahadi hewa ,basi apewe na ulinzi kabisa ...


Miaka mitano tunateseka tuu ,no ajira ,hakuna kuongeza mishahara ,biashara ngumu ,yale magenge ya dodoma ni kusisituza tu watu wajiajiri bila mazingira wezeshi...

Apewe na aridhi bure kabisa ...

Nasema uongo ndugu zangu
 
Nikiwa mfanyibiashara Japo sio mkubwa, ila mwenye upeo naunga hoja zako kwa asilimia 100%.

Pia, nikiwa kama mshabiki wa Simba lakini mwenye mapenzi na Mpira wa miguu, namkaribisha Manji nyumbani. Naamini atawasaidia Sana watani wangu Yanga.

Karibu sana Manji, karibu nyumbani.

WANANCHI haswa wafanyabiashara wa kada za chini mnatakiwa muwapende hawa wafanyabiashara wakubwa kwa sababu hawa wakifanya BIASHARA zao vizuri zikikua na wewe wa chini kama una akili timamu utapanda tuu. Kuwachkua hawa no ushamba wa kiwaangi cha juu sana, na wivu wa kijinga. Hawa ndo wanaleta mzunguko wa fedha, hivyo tuwapende na tuwaombee kwa MUNGU, wasiondoke tena hapa nchini.
 
Back
Top Bottom