Awaite wawekezaji wote wakubwa wazalendo aongee nao mf. Bakhresa,Manji,Dewji, zully Nanji, Gachuma,Ndagote, Rostam, Abood. Twiga ciment, nk kisha kikao kingine awaite wawekezaji wa kati kwa makundi mf viwanda, mahoteli, madini, ujenzi,mahospitali, mashule, kilimo, uvuvi, na mifugo. Baadaye awaite wafanya biashara wadogo. Hii itasaidia sana kurudisha imani.Habari wadau!
Kuna siku nilishawai ku comment humu kwamba uwepo wa mfanyabiashara Yusuf Manji una umuhimu mkubwa sana katika Taifa hili, hivyo nikashauri Mama Rais Samia Hassan amuombe Manji arudi, hatimaye sasa Manji amerejea nyumbani.
Hakika Manji ni Mtanzania mzalendo. Yaani licha ya yote yaliyomkuta na kukaa ughaibuni miaka mingi bado hakusahau nyumbani na sasa amerudi kuwekeza nyumbani.
Kwa wasiomjua Manji watabeza lakini huyu mtu ni muhimu sana katika kipindi kama hichi ambacho Rais Samia anataka kuboresha ueekezaji, kukuza uchumi na kutekeleza ilani ya chama kwa kutoa ajira million nane.
Sasa ni muda wa mama Rais Samia Hassan kumuita Manji Ikulu na kumsikiliza ana changamoto zipi ili serikali imsaidie aweze kuwekeza tena nchini.
Manji pia ni mpenzi mzuri wa mpira wa miguu ila kwa pande huu sitaki kumsemea.
Karibu sana nyumbani Mtanzania mzalendo Yusuf Manji.