commited
JF-Expert Member
- Feb 27, 2012
- 1,626
- 870
Ndugu zangu tumelalamika sana juu ya mustakabali wa maisha yetu sisi watanzania hasa sisiwenye kipato kidogo, tumelalamika kwa zaidi ya mika 15 juu ya
1. Kuuzwa kwa viwanda vyetu nchi nzima, na kusababisha watanzania zaidi ya 500,000 kukosa ajira kwa sera mbovu za kina Mkapa, Ngasongwa, Kigoda..... Viongozi wa ccm
2. Tumelalamika sana juu ya serikali kufikiria vyanzo vingine vya mapato, siyo kila siku kutegemea pombe (bia) wakati nchi ina madini, mbuga, msitu , mabonde,milima.... mfano mdogo du haijulikani mpaka leo MLIMA KILIMANJARO UNACHANGIA TSH katika uchumi wa nchi???
3. Tumepiga kelele za kutosha juu ya upatikanaji wa kazi, kazi zinatolewa kwa vimemo, kwa kujuana , kwa kufata majina makubwa makubwa, kama mzazi wako hayuko katika systemu ajira imekuwa ndoto, na huku wimbi la vijana likiongezeka kwa kukosa ajira, lakini serikali inacheza na masha katika jukwaa eti ajira milioni 1 kwa mwaka zimepatikana
4. Tumepiga kelele sana juu ya matumizi mabaya ya nguvu za polisi kwa wananchi wasiona hatia, watu wamevunjiwa majumba yao, watu wamehamishwa bila kulipwa fidia, watu wanaua wakiwa mikoni mwa polisi, vyama pinzani vinawekewa vikwazo na mapolisi katika kufanya kazi zao kwa uhuru
5. Tumepiga kelele juu ya mfumo huru wa uchaguzi, lakini kila uchaguzi lazima vurugu zitokee, serikali kushindwa kutofautisha shughuli za kichama na serikali, Serikali ya chama tawala kuiba kura waziwazi, tume ya uchaguzi kutokuwa huru nakadhalika..
6. Tumepiga kelele sana juu ya uuzwaji wa wanyama pori wetu, na migodi (kama barrick) kwa wawekezaji wasio na tija huku mikataba yao ikiwekwa siri hata wabunge wetu ambao ndio wawakilishi wa wananchi hawaioni
7. Tumepiga kelele sana juu ya rushwa inayokua anzaia sekta muhimu za serikali, kama wizarani (Afya, Nishati, Mambo ya ndani-Polisi, usalama wa taifa, Ikulu), rushwa bungeni, rushwa katika chaguzi, rushwa ndani ya chama tawala , lakini hakuna anayekamatwa hasa wale mapapa... wapo mitaani
8. Tumeona wizi uliokithiri kwenye huduma za mawasiliano kama, mitandao, ya simu na mamlaka TCRA ipo lakini hatuoni kianacho endelea, makampuni ya simu hayalipi kodi, lakini serikali imetulia
9. Tumeona serikali inaleta usanii kwenye swala nyeti la kilimo, mkulima hana say katika soko, anapangiwa mahali pa kuuza mazao yake aliyoyazalisha kwa ghrama zake, mkulima anachakachuliwa mbole, Ruvuma mwaka jana kwa mfano watu walipiga mbolea ya ruzuku zaidi ya tani 200 lakini hakuna kinachoendea
10. Tumepiga kelele juu ya serikali kuboresha huduma za jamii kama elimu bora kwa watoto maskini,kuboresha mishahara ya walimu, na madaktari, na wafanyakzi kwa ujumla, kuboresha huduma za afya na kuondoa matabaka katika sekta muhimu, lakini mambo ni yaleyale, watu leo wanakufa kwa kukosa dawa, mashine mbovu mahospitalini nakadhalika, Wanafunzi wanamaliza darasa la saba zaidi ya 5000 hawajui kusoma na kuandika, elimu yetu haimuandai mtu kujitegemea. lakini serikali inaleta poroja mpaka katika sekta muhimu zinazoigusa maisha ya mlala hoi.
SASA NDUGU ZANGU TUMELALAMIKA SANAA.. NA MAMBO NI YALE YALE, JE NINI KIFANYIKE
kARIBUNI