Watanzania tumelalamika sana kwa zaidi ya miaka 15, sasa nini kifanyike?????

commited

commited

JF-Expert Member
1,615
1,195
Ndugu zangu tumelalamika sana juu ya mustakabali wa maisha yetu sisi watanzania hasa sisiwenye kipato kidogo, tumelalamika kwa zaidi ya mika 15 juu ya
1. Kuuzwa kwa viwanda vyetu nchi nzima, na kusababisha watanzania zaidi ya 500,000 kukosa ajira kwa sera mbovu za kina Mkapa, Ngasongwa, Kigoda..... Viongozi wa ccm

2. Tumelalamika sana juu ya serikali kufikiria vyanzo vingine vya mapato, siyo kila siku kutegemea pombe (bia) wakati nchi ina madini, mbuga, msitu , mabonde,milima.... mfano mdogo du haijulikani mpaka leo MLIMA KILIMANJARO UNACHANGIA TSH katika uchumi wa nchi???

3. Tumepiga kelele za kutosha juu ya upatikanaji wa kazi, kazi zinatolewa kwa vimemo, kwa kujuana , kwa kufata majina makubwa makubwa, kama mzazi wako hayuko katika systemu ajira imekuwa ndoto, na huku wimbi la vijana likiongezeka kwa kukosa ajira, lakini serikali inacheza na masha katika jukwaa eti ajira milioni 1 kwa mwaka zimepatikana

4. Tumepiga kelele sana juu ya matumizi mabaya ya nguvu za polisi kwa wananchi wasiona hatia, watu wamevunjiwa majumba yao, watu wamehamishwa bila kulipwa fidia, watu wanaua wakiwa mikoni mwa polisi, vyama pinzani vinawekewa vikwazo na mapolisi katika kufanya kazi zao kwa uhuru

5. Tumepiga kelele juu ya mfumo huru wa uchaguzi, lakini kila uchaguzi lazima vurugu zitokee, serikali kushindwa kutofautisha shughuli za kichama na serikali, Serikali ya chama tawala kuiba kura waziwazi, tume ya uchaguzi kutokuwa huru nakadhalika..

6. Tumepiga kelele sana juu ya uuzwaji wa wanyama pori wetu, na migodi (kama barrick) kwa wawekezaji wasio na tija huku mikataba yao ikiwekwa siri hata wabunge wetu ambao ndio wawakilishi wa wananchi hawaioni

7. Tumepiga kelele sana juu ya rushwa inayokua anzaia sekta muhimu za serikali, kama wizarani (Afya, Nishati, Mambo ya ndani-Polisi, usalama wa taifa, Ikulu), rushwa bungeni, rushwa katika chaguzi, rushwa ndani ya chama tawala , lakini hakuna anayekamatwa hasa wale mapapa... wapo mitaani

8. Tumeona wizi uliokithiri kwenye huduma za mawasiliano kama, mitandao, ya simu na mamlaka TCRA ipo lakini hatuoni kianacho endelea, makampuni ya simu hayalipi kodi, lakini serikali imetulia

9. Tumeona serikali inaleta usanii kwenye swala nyeti la kilimo, mkulima hana say katika soko, anapangiwa mahali pa kuuza mazao yake aliyoyazalisha kwa ghrama zake, mkulima anachakachuliwa mbole, Ruvuma mwaka jana kwa mfano watu walipiga mbolea ya ruzuku zaidi ya tani 200 lakini hakuna kinachoendea

10. Tumepiga kelele juu ya serikali kuboresha huduma za jamii kama elimu bora kwa watoto maskini,kuboresha mishahara ya walimu, na madaktari, na wafanyakzi kwa ujumla, kuboresha huduma za afya na kuondoa matabaka katika sekta muhimu, lakini mambo ni yaleyale, watu leo wanakufa kwa kukosa dawa, mashine mbovu mahospitalini nakadhalika, Wanafunzi wanamaliza darasa la saba zaidi ya 5000 hawajui kusoma na kuandika, elimu yetu haimuandai mtu kujitegemea. lakini serikali inaleta poroja mpaka katika sekta muhimu zinazoigusa maisha ya mlala hoi.


SASA NDUGU ZANGU TUMELALAMIKA SANAA.. NA MAMBO NI YALE YALE, JE NINI KIFANYIKE
kARIBUNI
 
F

Froida

JF-Expert Member
8,663
2,000
Tuchukue hatua sasa wakati wa kulalama umeshapita ,ili kuiweka nchi kwenye dereva wa usukani aliye bora ni sisi wananchi kuamua sasa manake kila baya tunalijua lakini tumeshindwa kuamua
 
Azipa

Azipa

JF-Expert Member
1,071
1,225
Maandamano utasikia nenda kaandamane mwenyewe, basi tuanze ni migomo sekta zote.
 
Filipo

Filipo

JF-Expert Member
9,338
1,500
Ni kutoa elimu ya uraia kwa wenzetu ambao bado hawajatambua, kuhamasisha watu kujiandikisha kupiga kura na mwisho ni kukipigia kura chama mbadala ili tupate serikali mbadala kuanzia serikali za mitaa/vitongoji mwaka 2014 na serikali za wilaya na serikali kuu mwaka 2015. Lengo ni kupata serikali za wananchi, zitakazosikiliza na kutekeleza matakwa ya wananchi.
Na nina amini kwa sasa hakuna chama kingine mbadala zaidi ya cdm.
 
V

vutakamba

Senior Member
199
225
Haki haipatikani kwenye sahani ya shaba. Inapiganiwa na anaeendelea kuing'ang'ania wakati mwingine hubidi kumnyang'anya kwa nguvu. Hakuna atakayesema haki yako hii hapa chukua.
Changamoto kwa watanzania. La sivyo tutaendelea kulalamika miaka nenda rudi.
 
Evelyn Salt

Evelyn Salt

JF-Expert Member
48,839
2,000
kulalama ndo kipaji tulichojaliwa watz...Ndo tulivyo yani!!!!
 
CHASHA FARMING

CHASHA FARMING

Verified Member
6,804
2,000
Kuna Mtu aliwahi Kuniambia kwamba Tanzania na India ndo kuna Wanachi waoga kuliko mahali popote pale Duniani, na hili lina ukweli ndani yake,

Wabongo ni waoga asikuambie mtu, hatuko siriasi, Cheki mfano wa Ishu ya Mafao ya Kujitoa, Walikuwa wanalalamika watu wa Migodi pekee, wengine wote kimya, na Walikuwa wanalalamikia humu janvini, Facebook, kwenye vijiwe vya kahawa na kwingineko,

Jaribu kutembelea Vijiwe vya Kahawa, Draft na kazalika uone watu wanavyo lalamikia hii serikali, ila waambie sasa tuchuku hatua, hutamuona hata mmoja.

Kule Kagera Wanywaranda wameingia hadi Bongo na Wamefanya koloni lao kabisa, wanainchi wa huko wamebakia kulalamika tu bila wao kuchukua hatua,

KWA SASA INDIA KIDOGO WANACHI WAMEAMKA SO TUMEBAKIA TANZANIA PEKEE AMBAPO NDO KUNA WATU WAOGA
 
CHASHA FARMING

CHASHA FARMING

Verified Member
6,804
2,000
Ni kutoa elimu ya uraia kwa wenzetu ambao bado hawajatambua, kuhamasisha watu kujiandikisha kupiga kura na mwisho ni kukipigia kura chama mbadala ili tupate serikali mbadala kuanzia serikali za mitaa/vitongoji mwaka 2014 na serikali za wilaya na serikali kuu mwaka 2015. Lengo ni kupata serikali za wananchi, zitakazosikiliza na kutekeleza matakwa ya wananchi.
Na nina amini kwa sasa hakuna chama kingine mbadala zaidi ya cdm.
Ishu si Kubadili Serikali, Ishu ni Wabongo waache Uoga, Mkuu tunaweza badili serikali ukashangaa serikali mpya inakuja na Mambo ya Ajabu sana,
Cheki kule Misiri, Maandamano hayaishi pamoja na kwamba kuna Mabadiliko
 
S

Savannah

JF-Expert Member
239
0
CCM imetufikiswa hapa tulipo na hakifai kuendelea kushika dola. Mabadiliko ni lazima. Mambo ya misri ni kutikana na udikteta (negative dictatorship) wa muda mrefu amabayo ni sawa na wa CCM.
 
Azipa

Azipa

JF-Expert Member
1,071
1,225
Suala la mgomo au maandamano ni zuri sana. It'll help to make a political statement. Balozi zote zitapeleka ripoti kwenye nchi zao
 
commited

commited

JF-Expert Member
1,615
1,195
suala la mgomo au maandamano ni zuri sana. It'll help to make a political statement. Balozi zote zitapeleka ripoti kwenye nchi zao
unadhani maandamano yataleta uwajibiakaji tunaoutaka mkuu???
Karibu ufunguke zaidi
 
commited

commited

JF-Expert Member
1,615
1,195
Suala la mgomo au maandamano ni zuri sana. It'll help to make a political statement. Balozi zote zitapeleka ripoti kwenye nchi zao
Unadhani migomo na maandamano ndio njia sahihi ya kutuletea uwajibikaji tunaoutaka??
 
commited

commited

JF-Expert Member
1,615
1,195
ishu si kubadili serikali, ishu ni wabongo waache uoga, mkuu tunaweza badili serikali ukashangaa serikali mpya inakuja na mambo ya ajabu sana,
cheki kule misiri, maandamano hayaishi pamoja na kwamba kuna mabadiliko


sasa tufanyeje mkuu ili wabongo waache uoga?/
 
Azipa

Azipa

JF-Expert Member
1,071
1,225
unadhani maandamano yataleta uwajibiakaji tunaoutaka mkuu???
Karibu ufunguke zaidi
Njia ya haraka na yenye uhakika ndiyo hiyo, mkuu! Kumbuka uchumi wa nchi yetu upo mikononi mwa watu wachache. Maandamano siyo uhaini au uhalifu ni haki yetu ya kikatiba. How else is the outside world supposed to hear of our grievances?
 

Forum statistics


Threads
1,424,540

Messages
35,066,495

Members
538,014
Top Bottom