Watanzania tumekula Tunda tukaujua ukweli kwamba tupo Uchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania tumekula Tunda tukaujua ukweli kwamba tupo Uchi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by rennychiwa, Oct 28, 2010.

 1. rennychiwa

  rennychiwa Member

  #1
  Oct 28, 2010
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Ndugu zangu wanajamiiforum, naomba mnikaribishe rasmi kuwa mwanachama mpya. Nimeamua kujiunga nanyi katika kutoa michango ya kimawazo kwa Taifa letu. Na ninawapongeza sana wale wote walioanzisha tovuti hii.

  Ni kwa muda mrefu sana tumeishi kwa upofu, bila ya kujitambua na wakati mwingine tulifanywa vipofu kwa manufaa ya wachache. CCM imetuziba macho kwa muda mrefu, huku hali ya maisha ya mtu wa chini ikiendelea kudidimia. Chama tawala kimeshindwa kujipanga katika kuinua uchumi wa Taifa letu, wamejipanga kulinda maslai yao binafsi wakasahau umoja wetu wa kitaifa. Wameua viwanda walivyoachiwa na Baba wa Taifa, Kilimo kimebaki kuwa siasa majukwaani, madini leo hii hata mtoto mdogo amegundua kwamba si ya kwetu tena, huduma za afya kwa mtu maskini imekuwa ndoto.

  Leo hii watanzania waliokuwa wanaitwa wadanganyika wamekula tunda wamegundua miaka yote ya utawala wa CCM walikuwa wanatembezwa uchi sasa wanakimbilia nguo, CCM haitaki wavae nguo wanafunika nyeti zao kujisitiri na aibu. Sasa wanadai kuvalishwa nguo. Wanataka kujua nchi yao inakwenda imetoka wapi, inakwenda wapi na kwa nini?

  Tunaitaji uwiano wa wabunge, tunaitaji katiba mpya tunaitaji Rais mpya mwenye fikra mbadala na tunaitaji chama kipya. Tunataka tuwe na udhubuti wa kusema HAPANA miaka yako mitano uliaidi A,B na C hujatekeleza hata moja, Nenda zako. Ndani ya miaka mitano tuwapime, ndani ya miaka mitano tuwaangushe kama hakuna walilofanya kwa maslai ya Taifa letu.

  Nina kila sababu ya kukiunga mkono CHADEMA.
  Tujitokeze kwa wengi, tuwapigie kura. Huu ndio wakati wetu wa kufanya maamuzi sahihi.
  Kura yako ina nguvu zaidi ya Risasi.
   
 2. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  tena mimi nilikula koma manga baada ya kuuma tu hivi nikajicheki nikagundua niko uchi


  chadema oyeeeeeeeeeeee!!!
   
 3. Tatu

  Tatu JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2010
  Joined: Oct 6, 2006
  Messages: 1,081
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Inabidi niungane na wewe. Kwanza karibu sana katika jamii yetu.

  Pili, ni kweli sasa tumekula tunda tena la katikati ya bustani kwenye rutuba nyingi na ustawi mzuri. Muda wote huu tumekuwa tunaambulia maganda tu (ma-panki). Inabidi tusirudi nyuma hata hatua moja.

  Kabla ya kujiunga na jamii forums, Chama Cha Masikini kilikuwa baba, mama, kaka, dada, ............. and the list goes on. Naweza kukubaliana na mtu mmoja tu katika CCM ambaye bado namuheshimu na NITAMUENZI milele, JULIUS KAMBARAGE NYERERE. The guy will live with me forever. Manyang'au wengine sitaki hata kuwasikia. They need to go to HELL.
   
Loading...