Watanzania tumeahidiwa kila mmojawetu atapata chandarua kufikia Agosti ijayo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania tumeahidiwa kila mmojawetu atapata chandarua kufikia Agosti ijayo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mtoboasiri, Jun 4, 2011.

 1. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #1
  Jun 4, 2011
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  JK: Kila Mtanzania kulala kwenye chandarua Agosti
  BY MWANDISHI WETU
  3rd June 2011
  Email
  Print
  Comments

  Rais Jakaya Kikwete akizungumza katika mkutano wa wadau wanaotafiti upatikanaji wa dawa bora za kutibu ugonjwa wa malaria uliofanyika jijini Dar es Salaam jana.

  Rais Jakaya Kikwete ametangaza kuwa kila Mtanzania atakuwa analala ndani ya chandarua katika miezi miwili ijayo kuanzia sasa katika jitihada za serikali za kupambana na ugonjwa wa malaria unaoendelea kuua watu wengi kuliko mwingine wowote nchini.
  Alitangaza habari hizo kwa Watanzania jana usiku alipohutubia Mkutano wa 12 wa Wadau wa Watafiti wa Dawa za Malaria (MMV).
  Mkutano huo wa siku mbili wa mabingwa wa kupambana na ugonjwa wa malaria kutoka kote duniani unafanyika kwenye Hoteli ya Double Tree, jijini Dar es Salaam.
  Rais Kikwete alisema ugonjwa wa malaria unabakia kama ambavyo imekuwa kwa muda mrefu, tishio kubwa kwa afya, ustawi, uzalishaji na maendeleo ya Watanzania na Waafrika kwa jumla.
  Pia alisema serikali yake imedhamiria kutokomeza ugonjwa huo kwa kutumia njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kugawa bure vyandarua za kuwalinda wananchi dhidi ya mbu wanaosababisha ugonjwa huo.
  Alisema malaria siyo matokeo ya umaskini wa Waafrika bali ni chanzo na sababu kuu ya umaskini ugonjwa huo ukizigharimu chumi za Afrika kiasi cha dola za Marekani bilioni 12 kwa mwaka katika kuhudumia wagonjwa na kiasi cha asilimia 1.3 ya mapato ya taifa ya nchi hizo kwa upotevu wa mapato.
  “Malaria pia ni mchangiaji na chanzo kikuu cha kiwango cha juu cha vifo vya akinamama na watoto katika Afrika, na hivyo kuwa kikwazo kikubwa katika kuchelewesha ufikiwaji wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDG),” alisema.
  Hata hivyo, Rais Kikwete alielezea mafanikio makubwa ambayo yamepatikana katika kupambana na ugonjwa wa malaria barani Afrika.
  Alisema: “Katika miaka mitano iliyopita matumizi ya vyandarua, unyunyiziaji wa dawa na matumizi ya dawa zenye kufanya kazi vizuri zaidi umepunguza kiwango cha ugonjwa wa malaria kwa asilimia 50 katika nchi 11 za Afrika. Sasa malaria imepoteza nafasi yake kama mwuuaji wa kwanza wa watoto wadogo wenye umri wa miaka mitano na kushikilia nafasi ya tatu.”
  Akikariri takwimu za Ripoti ya Malaria ya Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa mwaka jana, 2010, Rais Kikwete alisema kuwa kiasi cha vyandarua milioni 289 vimegawanywa katika nchi za Afrika kati ya mwaka 2008 na 2010, idadi inayotosha kuwalinda asilimia 76 ya wakazi wa bara hilo wanaokabiliwa na hatari ya kupata malaria. “Idadi hii ni kubwa sana kwa kutilia maanani kuwa mwaka 2000 idadi hiyo ilikuwa ni asilimia tano tu.”
  Kuhusu unyunyiziaji wa dawa, Rais Kikwete alisema kuwa mwaka 2009 kiasi cha watu milioni 73 katika nchi za Afrika waliepukana na malaria kutokana na dawa hiyo kulinganisha na milioni 13 mwaka 2005 na dawa mseto kiasi cha milioni 229 zilinunuliwa duniani pote mwaka 2009 ikilinganishwa na milioni 2.1 mwaka 2003.
  Hata hivyo, Rais Kikwete alisema pamoja na mafanikio hayo yote, vita dhidi ya malaria bado mbichi kabisa na akawashuruku wote; watu, taasisi na mashirika, ambao wamekuwa wanachangia raslimali zilizochangia mafanikio hayo yaliyopatikana katika kupambana na ugonjwa huo.
  Naye Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Haji Mponda, alisema kiasi cha watu kati ya 60,000 hadi 80,000 hupoteza maisha yao kila mwaka kwa ugonjwa wa malaria.
  Kwenye shughuli hiyo, Rais Kikwete pia alishuhudia aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya MMV kwa miaka sita iliyopita, Baroness Lynda Chalker kutoka Uingereza akikabidhi uenyekiti kwa Raymond Chambers wa Marekani ambaye pia ni Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika kupambana na malaria.
  SOURCE: NIPASHE
   
 2. Omuregi Wasu

  Omuregi Wasu JF-Expert Member

  #2
  Jun 4, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 753
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kawaida yake kuahidi ila kutekeleza ndo hadithi nyinginezo hapo
   
 3. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #3
  Jun 4, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Wapo watanzania bilioni ngapi sasa? Sensa ya mwisho tulielezwa tupo 32 bilioni. Hivi karibuni tukaambiwa tumefikia zaidi ya 40bilion. Kila mtanzania akiwa ana chandarua chake inahitajika vyandarua zaidi ya 40 bilioni, hii haijalishi familia ambazo watu zaidi ya wawili wanalala kitanda kimoja, haitajali iwapo unalala kitanda cha miti na kamba ambacho mbu waweza kupenya, haijalishi unaishi nyumba ya udongo yenye madirisha na milango ya matete au inayozuiwa kwa khanga kuukuu, haijalishi kma unashinda baa au kwenye majukumu yanayokufanya utoke usiku kila siku, haieleweki iwapo mgao wa chandarua utaendelea kwa wale ambao vyandarua vyao vitachanika nk. Hii staili ya malaria haikubariki ni mradi wa wajanja. How possible to control experienced mosquitos using trapping nets? Mbu wengi wameshakuwa sugu na mazingira yetu. Chandarua za mradi wa malaria mostly ni mbovu, hazina uhimara wa kudumu zaidi ya wiki moja kabla hazijachanika. Achilia mbali wale wazitumiao kuvulia samaki na kutegea ndege, tutawadhibitije!?
   
Loading...