Watanzania tukatae serikali Moja, Mbili au Tatu. Tupiganie REFERENDUM.

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
6,808
6,500
Tanzania hatutapata tena "GOLDEN CHANCE" kama hii iliyotokea ya kupata katiba mpya na kuachana na hili "DUDU" linaloitwa MUUNGANO.

Kudai muungano usiwepo kwenye katiba ijayo 2014 kwa sasa siyo kosa. Lingehesabika ni kosa kisheria kama tungekuwa tunaweka viraka tena katika katiba hii mbovu ya mwaka 1977, kama ilivyo katika ibara ya 1 na 2(i).
1. Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano.
2.-(1) Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar, na ni pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania inapakana nayo.

Sijasikia hata chama kimoja cha siasa, Asasi za kisiasa na Wanasiasa mmoja mmoja wakija na hoja ya REFERENDUM ili kujisimika kwa wapiga kura kwa vile kwa sasa kuna OMBWE la hoja ya msingi kuhusu muungano.

Kama kitatokea chama kwenye uchaguzi mkuu ujao 2015 kikaja na hoja yenye ABSOLUTE PROMISE ya referendum sina pasi shaka kitapata kura maelfu kwa mamilioni kwa wananchi wa pande zote za muungano.

Huhitaji kufanya research kujua wananchi wa pande zote mbili za muungano wamechoka na hili 'ZIGO' la muungano ambalo liko UNBALANCED kwa pande zote. Kila pande zinalalamika lakini kwa sababu ambazo haziko wazi na hazieleweki huku wanasiasa wetu wakiwa wameziba midomo na masikio.

Tarehe 30 Aprili, 1992, Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais wa wakati ule, John Samuel Malecela alibainisha katika bunge la Muungano matatizo ya muungano ambayo alisema mwarobaini wake ni UTEKELEZI.

John Samuel Malecela alisema, ninanukuu,
Na bila ya kuyaficha baadhi ya matatizo hayo ni mambo yanayohusu suala la uraia, milki ya fedha za kigeni, ukusanyaji na mgawanyo wa mapato kutokana na kodi na ushuru wa forodha,tatizo la formula ya kuchangia gharama za Muungano. Hakuna shaka kwamba haya ni matatizo na mara nyingine yanakera:

Hata hivyo, kwa heshima zote kwa Tume Waheshimiwa Wabunge watakubaliana nami kuwa utatuzi au ufumbuzi wa matatizo hayo, hautapatikana kwa kuanzishwa Shirikisho la Serikali tatu. Kinyume chake hiyo itakuwa ni chanzo cha kufifia umoja wa mshikamano wa Tanzania uliojengeka tango mwaka 1964. Inatoa mwanya kwa wasiopenda umoja huo hatimaye kuuvunja. Hiyo siyo kwa manufaa ya wananchi wa Tanzania nzima. (Makofi) Mheshimiwa Spika, matatizo ni
lazima yatatuliwe. Hivyo ni azma ya Chama Cha Mapinduzi na Serikali kueleza nguvu zake zote katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo hayo. Serikali na Chama zitaendelea kutafuta ufumbuzi wa matatizo bayo halisi na kuyaondoa kwa manufaa ya wananchi wote wa Tanzania chini ya mfumo wa sasa. Hivyo kwa sasa Serikali inayafanyia kazi maeneo Yanayohusika. Uhusiano wa Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na hasa katika maeneo yanayohusu matatizo niliyoyaainisha.
Mwisho wa kunukuu.

Miaka 49 kwa sasa, matatizo siyo kwamba bado ni yale yale bali pia yameongezeka. Repoti zaidi ya 39 kuhusiana na muungano zimeandikwa na viraka zaidi ya 10 vimewekwa bila kupata mwarobaini wa matatizo achilia mbali utekelezaji. Kwa jinsi hali inavyoonekana, things will only get worse before getting more worse. Ikumbukwe kuwa mfumo wa muungano wa Ireland ya Kaskazini uliotumika kama BENCHMARK kuandika Hati ya Muungano wetu lakini imegundulika mfumo huu una matatizo ambayo hata nchi za Ireland Kaskazini mpaka ninaandika hii mada bado zina matatizo makubwa na Mwingereza kwa maana kuwa, hii hati ya muungano ina matatizo ya msingi ambayo hayawezi kumalizwa na vikao vya bunge na repoti mbali mbali, bali yatamalizwa na REFERENDUM kama UK walivyonyosha mikono juu na kuamua baada ya uchaguzi mkuu ujao kuwepo na referendum kuhusu uhuru wa Waskotishi na uanachama wa muungano wa nchi za ulaya.

Wakati wa vuguvugu la G55, Rais Mwinyi aliwahi kutamka kuwa mwerekeo wa CCM na sera zake ni kutoka serikali mbili kuelekea serikali MOJA. Kwa sasa jinsi matatizo yalivyokuwa makubwa, hata hiyo sera ya CCM ya serikali moja haiwezekani tena.

Kwa sasa tumefikia sehemu ambayo hata Jaji Mkuu na Waziri Mkuu hawana uhakika kama Zanzibar ni nchi au Mkoa. Matatizo ni makubwa yamefikia kiwango cha nchi kutokuaminiana kutokana na matatizo ya hati ya muungano, maslahi kiuchumi na tofauti la ongezeko la watu kati ya nchi mbili ukilinganisha na eneo la nchi. We can't sit in here and keep on fooling ourself. It'll NEVER work.

Swali linalokosa majibu ni DOGO lakini limebeba mabadiliko ya kitaifa kwa manufaa ya wananchi kitaifa kwa leo na kwa kizazi kijacho katika nyanja zote (kisiasa, kiuchumi na kijamii).

Kwa nini swala la muungano linakuwa ni SIRI?. Kwa nini wananchi wasipewe REFERENDUM wakajiamulia mwerekeo wao?.

Wananchi wana haki ya kuambiwa na kujua mwelekeo wa nchi zao kwa matakwa yao na kwa manufaa yao na kizazi kijacho. Hizi ni zama za UWAZI na UKWELI kama Rais Mkapa alivyochagiza baada ya kuingia madarakani mwaka 1995. LAZIMA TUAMBIZANE.

Kama wanasiasa wetu wanahubiri kuwa nchi ina DEMOKRASIA, huku wakijua demokrasia maana yake ni utawala wa watu au madaraka kwa manufaa ya watu. Kwa nini wanashindwa kuishi kwenye maneno yao?.

Kwa sasa inavyoonekana wananchi wanataka mwerekeo mwingine kisiasa, kiuchumi na kijamii, kwa hiyo lazima wasikilizwe. Njia mbadala kwa sasa ni kura kwa njia ya REFERENDUM.

GIVE US A REFERENDUM to vote YES MUUNGANO or NO MUUNGANO.

Hatuwezi kuukimbia UKWELI. Kufanya hivyo ni kuwa kama ngamia anayezika kichwa kwenye mchanga.
 
Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    49.4 KB · Views: 150
Hii hoja naiunga mkono sana. Tufike mahali sasa wananchi wapewe nafasi ya kuamua kama wanautaka muungano or not. Nina uhakika kabisa kwamba katika kura zitakazopigwa, asilimia themanini wataukataa. Akina Warioba wanajaribu kutuchagulia aina ya muungano bila kutupa nafasi ya sisi kuamua kama tunautaka au hatuutaki? Nafikiri ni wakati mzuri sasa, kuitaka katiba iache kipengele cha muungano kuamuliwa kutokana na kura za maoni.
 
tatizo sio kuvunja muungano. bali ni namna ya kuuvunja tuna madeni ya taifa, tuna mipango ya maendeleo ya muda mrefu na sasa ina zaidi ya miaka 20 na inaendelea, kutakuwa na mabadiliko ya majengo ya mabalozi nchi zote m kiti cha umoja wa mataifa vitatakiwa viwili, kuna fungu benki kuu la kugawana na kugawana majeshi na polisi walioko kwenye ajira moja ya muungano yenye pension namafao tofauti. NADHANI KINACHOWATESA NI NAMNA YA KUUVUNJA SIO KUSEMA TU NENO TUVUNJE AU KURA ZA WANANCHI SIO TATIZO. pia na suala la kiusalama hawa wenzetu znz wanaweza kugeuka somalia tukapata maumivu kama wanayoyapata kenya.
 
Umelinena vema sana hili mkuu. Lakini huu ni kama mwiba ulioingia kwenye mguu? Kuuchomoa ni lazima upate maumivu mara dufu ya yale ya mwiba wenyewe unapokuwa bado upo humo ndani. Lakini je tusiutoa mwiba kwa kuogopa maumivu halafu tuje tukumbane na adha ya kukata mguu? Tutafakari hili. Haya matatizo tunayoyaogopa tutayalea hadi lini? Maana ni wazi kwamba hayatibiki kwa kuendelea kuyapolishi kwa federation. Vinginevyo kama hatutaki kuuvunja muungano tuunde serikali moja. Zanzibar iwe mkoa wa Tanzania.
 
Hoja zilizoletwa kwenye Rasimu ya katiba na tume ya Jaji Warioba hazina tofauti na kile ambacho kimekuwa kikifanyika kwenye katiba hii ya 1977. Wanajaribu kuzipa viraka kwenye nguo badala ya kununua nguo mpya.

Tutapata katiba mpya lakini tatizo la muungano halitaondoka na kitakachotokea ni kuwa na matatizo mengi na makubwa.

Mabunge matatu, marais watatu bila kusahau mabaraza ya mawaziri matatu yanayojaribu kutatua matatizo ya wananchi millioni 44,928,923 ambayo bajeti yake 40% kutoka kwa wahisani.

Hiki ni kichekesho.
 
Kijana haujatafakari vizuri bali umekalili nani aliwahi kusema nini. tunachotaka wewe utushawishi nacho ni hoja yako ya referendum ina faida gani ukilinganisha na hoja iliyoletwa mbele yetu. Maana naamini muungano wa wazazi wako uliukuta hata kama baba na mama wanagombana kila siku huwezi kuja mtoto kuitisha referendum ya kujadili muungano wa wazazi wako. hii ni kwa sababu muungano unafaida kuliko matatizo yanayojitokeza ndani yake ambayo yanaweza kujadiliwa na kutatuliwa. naamini watanzania wote tutasapoti maboresho ya muungano labda anayetaka kutushawishi aje na hoja za kutuambia tunapata hasara gani ndani ya muungano ambazo tunaweza kuzieupuka nje ya muungano na alinganishe na faida tunazozipata ndani ya muungano ili tuangalie uzito mkubwa uko wapi. muungano si wa mtu au kundi Fulani bali muungano ni wa watanzania hivyo tushawishiwe kwa hoja zinazochambua watanzania sio kundi Fulani lilikuwa hivi au mtu Fulani alisema hivi.
 
Hizi gharama kubwa za serikali ya Muungano zitalipwa na nani?

Kama bara watotoa 97% ya gharama na Visiawni 03%... je kuna manufaa gani ya Muungano huu haswa kwa bara?

Je bara wataendelea kubeba gharama hizi hadi lini??
 
Binafsi tangu mwanzo nilishahuri kwanza mfumo wa utawala tuujadili kama taifa na kukubaliana kisha ndiyo itungwe Katiba. Huwezi kuandika Katiba ya Muungano bila kwanza kukubaliana ni muundo gani wa muungano unautaka. Matokeo yake ni kuwaachia hakina Warioba na Tume yake kutuamlia muundo wa muungano. Ikumbukwe kuwa awali walijaribu kutunga sheria ambayo ilitaka kuzuia watu kuongelea suala la muungano! Nguvu za watu tu ndiyo zilishinda, sasa tunaona tatizo lilivyo kubwa. Katiba ya muungano haiwezi kukamilika bila kuwa na makubaliano ama tuwe na muungano au la, au muafaka wa aina ya muungano huo.

Pia aina ya utawala (hasa kwa Tanganyika) tutakao kuwa nao tunapaswa kukubaliana kwanza, siyo Tume inakuja tu na kauli ya "tumefikiria mufumo huu tukaona ni wa gharama au utaleta ukanda, ukabila au udini kwahiyo hatukuuchukua". Umoja utajengwa kwa kujadili mambo haya na kufikia mwafaka ili yakiingia kwenye sheria mama yanaungwa makono na waliowengi.

Pendekezo la Referendum ni la kujenga lakini lifanyike tu baada ya mjadala wa kitaifa.
 
Hii hoja naiunga mkono sana. Tufike mahali sasa wananchi wapewe nafasi ya kuamua kama wanautaka muungano or not. Nina uhakika kabisa kwamba katika kura zitakazopigwa, asilimia themanini wataukataa. Akina Warioba wanajaribu kutuchagulia aina ya muungano bila kutupa nafasi ya sisi kuamua kama tunautaka au hatuutaki? Nafikiri ni wakati mzuri sasa, kuitaka katiba iache kipengele cha muungano kuamuliwa kutokana na kura za maoni.
Ninaamini hata Kikwete hautaki Muungano ila anaogopa kuingia kwenye vitabu vya kumbukumbu kwamba wakati wa utawala wake ndipo muungano ulivunjwa, sijui kwanini watu wanauogopa mzimu wa nyerere hata kwa mambo ambayo hata Nyerere mwenyewe angekuwepo angeona kwamba yamepitwa na wakati.
 
tatizo sio kuvunja muungano. bali ni namna ya kuuvunja tuna madeni ya taifa, tuna mipango ya maendeleo ya muda mrefu na sasa ina zaidi ya miaka 20 na inaendelea, kutakuwa na mabadiliko ya majengo ya mabalozi nchi zote m kiti cha umoja wa mataifa vitatakiwa viwili, kuna fungu benki kuu la kugawana na kugawana majeshi na polisi walioko kwenye ajira moja ya muungano yenye pension namafao tofauti. NADHANI KINACHOWATESA NI NAMNA YA KUUVUNJA SIO KUSEMA TU NENO TUVUNJE AU KURA ZA WANANCHI SIO TATIZO. pia na suala la kiusalama hawa wenzetu znz wanaweza kugeuka somalia tukapata maumivu kama wanayoyapata kenya.

Hili nalo neno maana hawa jamaa waliowengi ni wa hivi hivi
 
Ninaamini hata Kikwete hautaki Muungano ila anaogopa kuingia kwenye vitabu vya kumbukumbu kwamba wakati wa utawala wake ndipo muungano ulivunjwa, sijui kwanini watu wanauogopa mzimu wa nyerere hata kwa mambo ambayo hata Nyerere mwenyewe angekuwepo angeona kwamba yamepitwa na wakati.
Walivunja azimio la Arusha ambalo lilikuwa na impact kubwa kwa mstakabali wa taifa letu, wanashindwaje kuvunja muungano ambao hata faida yake haionekani. Nchi zilizokuwa nchi moja hapo zamani kama Ethiopia na Eritrea, Sudan na Sudan kusini, zinatengana, iwe ajabu kwetu ambaye unaunganishwa na nchi mbili huru?
 
Kijana haujatafakari vizuri bali umekalili nani aliwahi kusema nini. tunachotaka wewe utushawishi nacho ni hoja yako ya referendum ina faida gani ukilinganisha na hoja iliyoletwa mbele yetu. Maana naamini muungano wa wazazi wako uliukuta hata kama baba na mama wanagombana kila siku huwezi kuja mtoto kuitisha referendum ya kujadili muungano wa wazazi wako. ni kwa sababu muungano unafaida kuliko matatizo yanayojitokeza ndani yake ambayo yanaweza kujadiliwa na kutatuliwa.
Hii unayoleta hapa ni dhana potofu kwa sababu Muungano haukuwa wa kuwanufaisha wazazi peke yake.

Muungano ulikuwa pia wa kuninufaisha mimi kama mtoto na vizazi vijavyo lakini kadri siku zinavyokwenda, hayo manufaa siyaoni na kosa langu linakuwa ni kuhoji manufaa yake kwa sababu kama kusingekuwa na matatizo hata Rais Abdul Jumbe asingelazimishwa kwa mabavu kujiuzuru na wala kundi la G55 lisingetokea hata kitabu cha Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania kisingeandikwa achilia mbali mwasisi wake kutoa machozi. Kibaya zaidi Zanzibar pamoja na vilaka 11 lakini mpaka sasa hatujaweza kuziondoa kero zake zaidi ya kuongezeka.

Hayo matatizo yataondolewa lini ukichukulia toka mwaka 1992, wanasiasa wanadai matatizo yataondelewa.

naamini watanzania wote tutasapoti maboresho ya muungano labda anayetaka kutushawishi aje na hoja za kutuambia tunapata hasara gani ndani ya muungano ambazo tunaweza kuzieupuka nje ya muungano na alinganishe na faida tunazozipata ndani ya muungano ili tuangalie uzito mkubwa uko wapi. muungano si wa mtu au kundi Fulani bali muungano ni wa watanzania hivyo tushawishiwe kwa hoja zinazochambua watanzania sio kundi Fulani lilikuwa hivi au mtu Fulani alisema hivi.

Huwezi kuwawekea mwanvuli Watanzania wote kwa vile hakuna hoja ya kusapoti mwanvuli wako.

Kitu kitakachotuwezesha kufahamu kama Watanzania wengi wana sapoti Muungano ni kwa njia ya referendum ambapo swali la ndiyo au hapana litatoa jibu lisilo na ukakasi kuhusiana na mwelekeo wa muungano.
 
tatizo sio kuvunja muungano. bali ni namna ya kuuvunja tuna madeni ya taifa, tuna mipango ya maendeleo ya muda mrefu na sasa ina zaidi ya miaka 20 na inaendelea, kutakuwa na mabadiliko ya majengo ya mabalozi nchi zote m kiti cha umoja wa mataifa vitatakiwa viwili, kuna fungu benki kuu la kugawana na kugawana majeshi na polisi walioko kwenye ajira moja ya muungano yenye pension namafao tofauti. NADHANI KINACHOWATESA NI NAMNA YA KUUVUNJA SIO KUSEMA TU NENO TUVUNJE AU KURA ZA WANANCHI SIO TATIZO. pia na suala la kiusalama hawa wenzetu znz wanaweza kugeuka somalia tukapata maumivu kama wanayoyapata kenya.
Muamerika aitwaye H.P. Lovecraft aliwahi kusema, The oldest and strongest emotions of humankind is fear, and the oldest and strongest kind of fear is fear of the unknow.

Sisi hatutakuwa wa kwanza katika dunia hii na kuna mifano ambayo pamoja na muungano kuvunjika, nchi zimeweza kupiga hatua mbele za kimaendeleo. Nchi nyingi za ulaya ya mashariki ziliweza kuachana na zimeweza kusonga mbele.

Kibaya zaidi, muungano umekuwa kama ni siri ambaye wananchi wa kawaida hawatakiwi kuuchimba ili kuufahamu kwa undani zaidi ya kupata dodoso za hapa na pale kutoka kwa wanazuoni mbali mbali.

Kwa nini sisi tuwe tofauti na nchi zilizofanikiwa baada ya kuachana na muungano.
 
Hizi gharama kubwa za serikali ya Muungano zitalipwa na nani?

Kama bara watotoa 97% ya gharama na Visiawni 03%... je kuna manufaa gani ya Muungano huu haswa kwa bara?

Je bara wataendelea kubeba gharama hizi hadi lini??
Haya ndiyo maswali ambayo wanasiasa wetu hawataki kuyajibu badala yake wanatuletea dummy la muungano ili tuendelee kunyonya kana kwamba nchi bado ni changa na wananchi hawafahamu kilichoko nyuma ya pazia.

Muungano wa serikali tatu hauwezi kutatua matatizo yaliyopo ambayo yana miaka karibia 50, kitakachofanyika ni kuyapoza kwa muda kabla hayajalipuka kwa kishindo.
 
Hakika ninayo furaha kuiona Tanganyika ikitajwa kwenye rasimu ya katiba mpya,ni ishara kubwa Tanganyika itarejea na kurejea kwake kutarejesha TANU maana Afro shiraz itarejea kwao za Zanzibar na CCM kufa kimiakimia.ooh karibu TANU uturejeshee utu wetu,uzalendo wetu,upendo wetu,aridhi yetu,madini yetu,elimu yetu na maendeleo yetu na utuondolee wanasiasa wanafiki waliosajili vyama kwa ajili ya matumbo yao na ndg zao huku wakijiita wakombozi,kumbe ni wezi wa mchana.karibu TANU,Karibu Tanganyika Uliyetuletea Uhuru wetu.
 
Hoja zilizoletwa kwenye Rasimu ya katiba na tume ya Jaji Warioba hazina tofauti na kile ambacho kimekuwa kikifanyika kwenye katiba hii ya 1977. Wanajaribu kuzipa viraka kwenye nguo badala ya kununua nguo mpya.

Tutapata katiba mpya lakini tatizo la muungano halitaondoka na kitakachotokea ni kuwa na matatizo mengi na makubwa.

Mabunge matatu, marais watatu bila kusahau mabaraza ya mawaziri matatu yanayojaribu kutatua matatizo ya wananchi millioni 44,928,923 ambayo bajeti yake 40% kutoka kwa wahisani.

Hiki ni kichekesho.

Yaani hapa tumeshachanganywa na kukorogwa, hatujui hata kusini au kaskazini ni wapi! Mara wengine wanaikubali, mara wengine sio yote, mara wengine sijui nini... I don't see how we are going to get organized in this f***n business...

Kwa vyovyote vile, kama wataendelea kung'ang'ania hili limuungano lao, 2014 rasimu inapigwa chini kwenye kura ya maoni... wakilirudisha tena, tunaipiga chini tena... eeh, tuone watafanya nini. Sijui wataamua kutagaza kuwa mchakato wa katiba umeahirishwa hadi tutakapotangaziwa tena?!!!

Maana watu wanajitia kuwasemea watanzania kuwa tunapenda muungano!!! Nani kasema?
 
Umelinena vema sana hili mkuu. Lakini huu ni kama mwiba ulioingia kwenye mguu? Kuuchomoa ni lazima upate maumivu mara dufu ya yale ya mwiba wenyewe unapokuwa bado upo humo ndani. Lakini je tusiutoa mwiba kwa kuogopa maumivu halafu tuje tukumbane na adha ya kukata mguu? Tutafakari hili. Haya matatizo tunayoyaogopa tutayalea hadi lini? Maana ni wazi kwamba hayatibiki kwa kuendelea kuyapolishi kwa federation. Vinginevyo kama hatutaki kuuvunja muungano tuunde serikali moja. Zanzibar iwe mkoa wa Tanzania.
Wandugu mchana mwema; Mfano mwingine TALAKA... Mke akingangania talaka na kumburuza Mumewe kwa wahusika, itabidi mume atoe talaka na asiulize we mama watoto wangu utaenda wapi na kuiishi na nani? talaka ikitolewa tu hapo hayamhusu mume tena. huyo ex-mke atajua lake na maisha yake (kumradhi/hashakum awe kahaba au jambazi au gaidi au Barmedi nk,) Kwa hiyo haijalishi awe kama Somaliya au Iraki au Afghanistan !! Sasa hapo ndo tatizo letu Vile Mume atabeba tija na matokeo yote ya mustakabali ( yaani kutunza watoto na kulipia madeni yote) Wakuu Jambo hili ni la kujikamua na kulitafakari kiutu uzima. siyo kufuata mahanjamu na presha la viongozi njaa na wasiyo na misimamo. tukubali
kupoteza machache ili tuokoe shehena kubwa la jahazi. LONG LIVE TANZANIA.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom