Watanzania tujiulize hili swali

Ketoka

JF-Expert Member
Sep 23, 2015
1,087
1,913
Lugumi ni kampuni inayotuhumiwa kwa muda mrefu kuwa inahusika katika kuhujumu uchumi na ufisadi wa nchi hii kupitia vyombo vyetu vya usalama hasa jeshi la polisi

Wakati mh Magufuli anaomba kura alisema mahakama kimafisadi itajengwa kwa ajili ya kupambana na wahujumu uchumi na mafisadi,sijui mpaka sasa hivi mapapa wangapi wamefungwa

Sasa la Juzi mh waziri wa mambo ya ndani anampa Lugumi siku 10 wawe wamekutana ofisini kwake Dodoma

Tujiulize hii ,Lugumi hatujaisikia leo kuwa ni wahujumu uchumi,inakuweje mpaka sasa hawajafunguliwa mashtaka ya uhujumu uchumi na ufisadi

Waziri unamuitaje mhujumu uchumi ofisini muongee na munaongea nini,kwamba mkubwa sasa tunaomba urudishe hela ambazo ulichukua au inakaaje hii

Ni Mara ya nyingine nasikia serikali ya Rais Magufuli inayochukia mafisadi wanaitana mezani na fisadi eti waongee, jiulizeni wanaenda kuongea nini Watanzania tujihoji hili swali kwa umakini,je Lugumi akimwambia haya mambo yaishe chukua billion 5 na hii nyingine 8 mpe bwana mkubwa ukaushe tutajuaje

Hivi hao watu wanaenda kuongea nini hasa?
 
Waziri unamuitaje mhujumu uchumi ofisini muongee na munaongea nini,kwamba mkubwa sasa tunaomba urudishe hela ambazo ulichukua au inakaaje hii

Mkuu unashangaa nini, mbona wale WEZI wetu tulizungumza nao na tukawabadilisha jina toka WEZI hadi WANA.........?
 
Back
Top Bottom