Elections 2010 Watanzania tujitokeze kwa wingi tukapige kura oktoba 31

Thuraya

Member
Mar 24, 2009
24
0
Mengi yamesemwa wakati huu wa kampeni.Mengi yatasemwa wakati uliobakia kabla ya Oktoba 31..siku ya kupiga kura.

Kila jitihada zimefanyika kwa ajili ya kushawishi wapiga kura wakatae mabadiliko..lakini hamna kilicho na nguvu kuliko nguvu ya umma.Nguvu ya umma ni kubwa kuliko nguvu ya fedha...kuliko mabango ya kampeni...kuliko vitisho vya vyombo vya usalama...kuliko SMS za vitisho...kuliko matokeo ya REDET.

Kumbukeni Keneth Kaunda aliitawala Zambia kwa miaka 27 na akaondolewa kwa nguvu ya umma kwenye uchaguzi....KANU ya Daniel Arap Moi iliondolewa baada ya miaka mingi ya utawala wa mabavu....Kamuzu Banda wa Malawi aliyekuwa rais wa maisha aliondoka madarakani kwa nguvu ya umma...Surhato wa Indonesia naye aling'oka...na wengine wengi wameondolewa kwa nguv ya umma.....

Mwaka 1991 wakati wa uchaguzi huko Zambia,kura za maoni zilionyesha kuwa Keneth Kaunda wa UNIP alikuwa anaongoza kwa 90% na mgombea wa upinzani MMD Fredrick Chiluba alikuwa anafuata akiwa chini ya 10%.

Kura zilipopigwa ,Kaunda alishindwa pamoja na chama chake kupoteza viti vingi vya uwakilishi bungeni.Ilionekana kuwa Kaunda alikuwa akidanganywa na wanaomzunguka kuwa angeshinda lakini hali halisi ilikuwa tofauti.

Hivyo watanzania wasibabaishwe na propaganda za akina Dk.Bana na REDET .Tujitokeze kwa wingi kupiga kura na kulinda kura zetu ili siku ya uchaguzi.Washawishi wale wanaotaka mabadiliko wakamchague Dr.Slaa na wagombea wengine wa upinzani ili nchii iweze kujikwamua kutoka kwenye makucha ya CCM.

Dr.Slaa ameshaonyesha njiana sasa ni wajibu wetu wapiga kura kumpa ushirikiano .

AMKENI WATANZANIA
 
Back
Top Bottom