Watanzania Tujitambue...

GHIBUU

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
4,432
3,006
Watanzania Na Wazanzibar kwa ujumla tunashindwa kujielewa.

Matatizo ya nchi ambayo inakabiliwa hasa katika suala la utumiaji wa madaraka vibaya pamoja na utumiaji wa rasilimali za umma kutumiwa vibaya inatokana na mambo haya kwa kutayachamua zaidi basi mutapata ukweli.

Kwanza Katiba - Katiba inatoa madaraka makubwa kwa viongozi akianzia rais mpaka mawaziri,kiasi ambacho hutumia vibaya madaraka yao,katiba haitoi fursa wananchi kuwashitaki viongozi waliko madarakani wakati wanapofanya maovu yao.

Pili Mahakama haziko na uhuru wa kisimama wenyewe, ispokuwa zinatumika kisiasa zaidi , rais anakuwa na nguvu zaidi ya mahakama,anaweza kutoa hukumu kabla haya hujafika mahakamani ,unapofika mahakamani unaweza kukumbana na vikwazo vikubwa kama vile kupata wadhamana, mfano tuangalie wiongozi wa dini tanzania bara na Zanzibar.

Tatu vyombo vya usalama- Vyombo hivi vipo chini ya Rais, rais anao uwezo wa kufanya chochote kile hata kama hakikubaliki,ana uwezo wa kutumia vyombo hivi kiubinafsi au kisiasa hata mawaziri pia vile vile.

Kwa mfano- wakati wa uchaguzi mkuu, Rais anaingia katika uchaguzi mkuu akiwa bado ni amiri jeshi mkuu,paanapotokea rais huyo kushindwa na chama cha upinzani,hutumia nguvu yake kuhakikisha anaendelea na madaraka yake,na kuhakikisha uchaguzi unachakachuliwa.

Mfano wa pili, pale vyama vya siasa hasa vya upinzani au jumuiya yoyote inataka kuomba kibali kwa police kwa mfano kutaka kufanya maandano ya kupinga jambo lolote linapingwa na wananchi kutoakana na uwendeshaji wa serikali, rais ana uwezo wa kukishawishi jeshi la police kuliingia maamuzi yao,hata kama maandamano yatakuwa yaa amani basi watanyimwa haki hiyo yaa maandamano.

Haya ni machache tu.
 
Back
Top Bottom