Watanzania tujikite kuzalisha na kuuza nje kuliko kuagiza zaidi kutoka nje (china)

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,077
21,929
Leo nilikaa na kufikiria kidogo juu ya biashara ... nilijikumbusha baadhi ya miaka ya mapema ya 2000 wakati biashara kati ya Dubai na Tanzania ilistawi. Niliona watu wengi wakienda Dubai kununua vitu halafu wanakuja kuuza Tanzania. Biashara ya vifaa vya umeme na magari iliwavutia wengi. Hivi sasa tuko katika zama za China na Tanzania ingawaje Dubai bado inaendelea kimyakimya.

Tofauti na Waarabu, nahisi kuna changamoto kubwa kwa Wachina. Viumbe hawa wamevuka mipaka na kuanza kuwa washindani wa wateja wao yaani sisi wanunuzi. Kivipi? Wachina wameamua kuja kufungua maduka yao Afrika. Kwa mfano, ukienda nchi jirani ya Zambia utapata maduka makubwa yaliyojengwa katika miji midogo kama Nzega, Katesh au Iramba kwa hapa nchini Tanzania. Na ndani ya Duka kubwa utakuta Wachina wanaweka karibu kila kitu raia anachohitaji kwa mahitaji yake ya kimsingi. Hii imefanya wenyeji washindwe kutoa ushindani na kuishia kupoteza mitaji. Ikiwa unafikiria kawaida bila hata digrii ya chuo kikuu ni kwamba China inachofanya ni kuvuna pesa zetu.

Je, na sisi pia twende huko kwao China tukafungue Malls zetu? Jibu ni kwamba haiwezekani na wachina sio wajinga kuruhusu kitu kama hicho. Nchi makini itaruhusu mwekezaji kuja kuwekeza vitu vikubwa kama viwanda, mahoteli na mengine kama hayo. Sisi tunaowaruhusu wageni kuja kushindana na Mangi tuna matatizo. Pia hatujipendi. Ila ndo imeshatokea na bado serikali inaendelea kuwaalika "wawekezaji"....

Vijana wa kiafrika tunachotakiwa kufanya ni kujikita kwenye biashara ambazo tutauza bidhaa na huduma kutoka hapa kwetu kwenda nje ya mipaka yetu. Kilimo na ufugaji ni kipaumbele kikuu. Pia vipaji ni chanzo kizuri cha fedha za kigeni. Nchi iendelee kuzalisha kina Diamond na Samatta wengi. Vijana wasomi nao wauze utaalamu wao hadi nje ya mipaka. Tuwe na ndoto ya kuona kijana wa kitanzania akiwauzia wageni utaalamu au bidhaa kutoka hapahapa nchini tofauti na sasa hivi vijana wengi tunafanya biashara ya kuagiza kutoka China na kuuza hapa. Kwangu mimi huu ni upotevu wa fedha za kigeni na uuaji wa vipaji na utaalamu mwingi uliogharamiwa na taifa. Kimsingi tutakachouza nje lazima kiwe kingi kuliko tukachoagiza kutoka nje.

Serikali kupitia bunge itunge sheria za kusapoti haya mambo badala sheria za kukandamizana. Lakini hawa wabunge ambao wengi wao wanasapoti miswada ya kisheria bila kufikiria mara mbili ndiyo wataleta mabadiliko? Hawa ambao wakiitwa kwenye Party caucus wanaishia kupatwa na uoga na kuishia kukubaliana na kila kitu? Muhimu zaidi ni katiba kubadilishwa hasa kile kifungu kinachoruhusu sifa ya mtu kuwa mbunge ni kujua tu kuandika na kusoma. Elimu ni muhimu sana ili binadamu kuweza kujitambua na kujiamini. Mungu ibariki Afrika.
 
Bandiko hili wengi hawatoelewa.
Mwaka 2006 niliacha kazi ya kuprint nguo na kwennda chuo.
Mwaka 2009 narudi pale nilipokuwa nafanya kazi naambiwa biashara imekuwa ngumu kwa vile wamekuja wachina keko halali masaa 24 anafanya kazi na ana mitambo yake.
Nikaambiwa analala juu ya kamba na ukimgongea anapokea kazi na alfajiri unarudi unapokea kazi yako.Nikawaonea huruma.

Baadae nikasikia kuna wachina wanapaka rangi mwenge inakuwa kama imetoka kiwandani.
Nimefika mikoani samaki wa maji chumvi walikuwa wanaletwa kupitia wavuvi wa kichina kilo moja Tshs 5000 na samaki wapo kimo kimoja wote.sisi wabongo kilo moja ilikuwa 6000.baada ya muda nikasikia wamepigwa ban samaki wabkichina nikashukuru watanzania tutauziana wenyewe kwa wenyewe he bei ikapanda ikaanza Tshs 6500 sasa hivi 8000-10,000 kwa kilo.
Tunapaswa tujenge mifumo imara nabtujielewe vyema kulinda biashara zetu na wateja wetu.
Ukuangalia wapemba hununulizana mtaani,ukiangalia wahindi nao ni hivyo hivyo sisi waswahili hatujali.
 
Ofisa ni kwamba yajayo hayafurahishi kama viongozi wetu hawatakuwa na msimamo
 
Ishakuwa to late, sisi tuliojaribu kutengeneza bidhaa tumeshajifunza maana vitendea au mashine hazipo mpaka ununue kwao na mafundi wa kuzitengeza hawapo Sasa uzalishaji unakuwa ni washidashida tu cha muhimu serikali itafute njia ya kuwaita waje wawekeze kutengeneza mashine na waajili watu wetu Ili wajifunze kutengeneza mashine kwa ajili ya kizazi cha baadaye ila sisi tuendelee tu kununua bidhaa zilizotengenezwa twende sambamba na teknolojia maana mpaka mashine zipatikane kwa wingi na bidhaa na ujuzi upatikane kwa wingi tayari tutakuwa nyuma kwenye teknolojia na maendeleo ya Leo.
 
Bro umenipiga na kitu kizito mno... ukweli mchungu
 
Back
Top Bottom