Watanzania tujiangalie jamani

Kutenga watoto wa kike under 18 eti kapata mimba wakati kama jamii na serikali hatujamlinda ni ukatili na halikubaliki. Hao ni kundi linalohitaji ulinzi wetu na sio kulitenga.

Hayo ya ushoga tusiwe wanafiki hapa kwani ni faragha ya mtu na hakuna anaye mpima mwenzake kuwa sio shoga.
Jee kama siku mnagundua kumbe huyo apigaye kelele kuwa hataki ushoga yeye mwenyewe anawakung'uta wengine mtasemaje? Au yeye anakung'utwa je?

Yametokea haya nchi tofauti kwa mawaziri kujitangaza ni mashoga na watu hawakujali kwani shida nini kwa wengine unapotumia kiungo chako?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
maiyanga1,
Sasa we unapaswa kujua ajenda ya MABEBERU ni USHOGA yaani wanatuchokonoa tuingie kwenye ajenda yao kuu ya USHOGA hivyo tuwaonyeshe kwamba sisi as a Nation tuna msimamo hatuyumbishwi hiyo ndio kitu iliyopo mezani nyingine ni danganya toto tu.
 
Hilo la ushoga ni lako mkuu
swala la mabinti kurudi shule ni jambo la muhimu kwa mustakabali wa mabinti na maisha yao kwa ujumla, sababu za mimba za utotoni nyingi ni ubakaji na ushawishi wa wanaume wenye tamaa. Kwa mabinti wa shule, Haki za mabinti kurudi shule ni muhimu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tuangalie na kwa upande mwingine hata mtoto atakayezaliwa naye anakuwa na haki zake hivyo mtoto akoshakuwa mzazi anapaswa kutimiza kutulia na kutimiza haki za mtoto aliyemzaa .
 
Mimba kwa mtoto wa kike mara nyingi sana haitokani na hiari yake. Tazama jogoo amfukuzapo mtetea hata akipanda mtini anaye tu.
Mabinti wengi wanajikuta katika mazingira hatarishi. Wale wanaopenda huo mchezo hawapati mimba sababu wanajua kuikwepa.
Kwa hiyo kuwafukuza shule hakuzuii mimba kwa wengine bali malezi bora ndio msaada mkubwa kwa mtoto wa kike.
Hilo la ushoga ni lako mkuu
swala la mabinti kurudi shule ni jambo la muhimu kwa mustakabali wa mabinti na maisha yao kwa ujumla, sababu za mimba za utotoni nyingi ni ubakaji na ushawishi wa wanaume wenye tamaa. Kwa mabinti wa shule, Haki za mabinti kurudi shule ni muhimu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimba kwa mtoto wa kike mara nyingi sana haitokani na hiari yake. Tazama jogoo amfukuzapo mtetea hata akipanda mtini anaye tu.
Mabinti wengi wanajikuta katika mazingira hatarishi. Wale wanaopenda huo mchezo hawapati mimba sababu wanajua kuikwepa.
Kwa hiyo kuwafukuza shule hakuzuii mimba kwa wengine bali malezi bora ndio msaada mkubwa kwa mtoto wa kike.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mtoa mada unaona watu wanavyojenga hoja...nafikiri kwa level yako ya thinking huna capacity ya kuanzisha uzi humu ningekushauri uwe msoma michango ya watu labda inaweza kukusaidia kupanua uwezo wako wa kufikiri.
I'm out.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mmmmh.. mtoto wa kike akipata mimba asisome eee? kwani kumruhusu akasoma wewe kama mtanzania utapungukiwa nini? hao wanafunzi wanaopata ujauzito siyo watanzania? je tuwatenge mama zetu kisa walituzaa? Unamjua lebron James Mama ake alimzaa akiwa na miaka 16 tu je kama jamii ingemnyanyapaa huyo jamaa si mimba yake ingefanyiwa abortion? why tunakuwa wabaguzi kwa ndugu zetu wenyewe?
na huo ushoga wewe unakuhusu nini mpaka uingilie faragha za watu?
Umeanza vizuri ila pointi za mwisho umeharibu kiongozi.....yaani ushoga ni wa kupingwa kwa nguvu zetu zote hata waweke vigingi vipi, tuko tayari turudi kwenye maisha ya Ujima ila si kuukubali ushoga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na

Nakosa imani na uzalendo wa Zitto Kabwe ,mtu kama yule inpaswa achunguzwe kuhusu uraia wake .

Hata kama ni siasa ila mashara mengine hakupaswa kuvuka mipaka kiasi hicho cha kuandika barua kwa WB ,yeye anachochea ili watoto wetu wasisome.
Kwa hiyo Mtanzania mzalendo anayepinga fedha za Mabeberu wanaotaka ushoga ukubaliwe kama Msumbiji ndie achunguzwe uraia tena?!...hahahaa

Mbona mnakoment kwa kutumia makalio?
 
Mabeberu hajawahi kulazimisha watoto wawe mashoga wala mabinti kupata mimba. Wengi wenu ni wanafki, mimba za watoto wenu zilitolewa tena na ma gynaecologist wazuri tu na mliwalipa pesa.
 
Tafakari pia namna hii. binti yako kajazwa mimba.
bado hautotaka arudi shule kama yuko tayari.
 
Boss TheDreamer Thebeliever Suala la Ushoga hata mimi siliafiki kabisa, kwanza ni kinyume na maandiko yetu, pili si tamaduni zetu, tatu si mila zetu, nne si desturi zetu. Haya mambo ya kuiga iga kila kitu si mazuri.

Hili la Wanafunzi wanaopewa mimba ni la kulifikiri vizuri, Je wanafunzi wanaobakwa na kupewa mimba? Nao utawanyima haki yako ya msingi ya kusoma? Afadhali miaka hii sheria kali, ukimpa mwanafunzi mimba ni mvua miaka 30.
Kusomesha wajawazito ni kuipa mzigo serikali usio na lazima ,waache tu wakaolewe watunze familia .Kahela kenyewe wanachotoa hao waisani ni katillioni moja harafu masharti kibao wakati hata kupiti pesa za ndani tunaweza tukapata hiyo hela,nikawaida yao kutikisa kiberiti hao.
 
Hilo la ushoga ni lako mkuu
swala la mabinti kurudi shule ni jambo la muhimu kwa mustakabali wa mabinti na maisha yao kwa ujumla, sababu za mimba za utotoni nyingi ni ubakaji na ushawishi wa wanaume wenye tamaa. Kwa mabinti wa shule, Haki za mabinti kurudi shule ni muhimu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna haki kwa mwenye dhambi,ingekuwa baadhi ya nchi za arabuni walitakiwa kupigwa mawe mpaka kufa.Ila serikaili yetu ya kidemokrasia wanapewa nafasi ya kuishi na kujiendeleza kielimu kwa mifumo mingine.
 
Umeanza vizuri ila pointi za mwisho umeharibu kiongozi.....yaani ushoga ni wa kupingwa kwa nguvu zetu zote hata waweke vigingi vipi, tuko tayari turudi kwenye maisha ya Ujima ila si kuukubali ushoga

Sent using Jamii Forums mobile app
Black Mirror: Wewe nawe umekuwa kama hao wengine waliotangulia ,mnapinga ushoga mitandaoni ingali mitaani na makazini kwenu kuna watu wenye hizo tabia .Je? Ulishawahi kuchukua hatua zozote kwao au mnakuja kutupigia kelele tu hapa jamvini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoa mada wapi wamesema watunyima mkopo kwa sababu ya ushoga .Watanzania achene kukariri.Tena hawajawanyima ,ni kuwa kuna wanaharakati wametuma barua kupinga watoto wakike kutorudi shuleni Acheni kuwasingizia mabeberu uwongo mbaya.
 
Wakati wa kujibu hoja lazima mtangulize ushoga, why? sisi tunasema mtoto wa kike kwa nini mmpatie adhabu yote peke yake? Apate mimba under 18 (bado mtoto mdogo). alee mtoto wa shinda sasa hata shule umzuie aaaaa huu si uungwana kabisa.

Tunataka Taifa walau lim-support huyu binti apate elimu tu baada ya kujifungua....hapa tatizo ni lipi? kwa nini mzigo wote wa dhambi atwishwe huyu binti mwenye umri wa chini ya 18?

Sasa hilo la ushoga watanzania hawalijui ni lenu.
 
Mtoa mada wapi wamesema watunyima mkopo kwa sababu ya ushoga .Watanzania achene kukariri.Tena hawajawanyima ,ni kuwa kuna wanaharakati wametuma barua kupinga watoto wakike kutorudi shuleni Acheni kuwasingizia mabeberu uwongo mbaya.
Usisome juu juu pipitia kwa umakini maada ndio uchangie.Nimesema ajenda za mabeberu ni mbili nimeorodhesha .Ukikubali ya kwanza kwa kisingizio cha kupata hela next time watakwambia ili sasa upate hizo hela ukubali na ajenda ya pili hivyo ndivyo ilivyofanyika kwa Mozambique .Nimetumia MZ kama case study ila zipo nchi nyingine.
 
Back
Top Bottom