Watanzania tujenge utamaduni wa kuandaa Wosia ili kuepuka kadhia hii

Amicus Curiae

JF-Expert Member
Sep 12, 2012
1,940
2,000
Awali ya yote nimpe pongezi Wakili Msomi Mathias Nkingwa aliyemtetea na kumpa ushindi mjibu rufaa katika rufaa hii.

Ipo dhana kwamba kuacha Wosia ni kujichulia, jambo ambalo halina ukweli wowote ule. Kimsingi, unapoacha Wosia unajiweka kwenye nafasi nzuri ya kugawa mali zako utakavyo na hivyo kuepusha migogoro isiyo ya lazima inayoweza kupelekea kubaribu kabisa mahusiano ya wategemezi wako; pengine hata kuuana wao kwa wao.

Hili limetokea kwenye Rufaa ya Mirathi na. 01 ya mwaka 2019 ambapo Beatrice Shogholo (mkata rufaa) ambaye ni dada wa marehemu aliifungua dhidi ya mjane Zaituni Salimu Kasimu (mjibu rufaa), mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya Korogwe Mh. Mussa Ngalu. Mkata Rufaa alisimamiwa na Wakili Msomi Peter Wenceslaus huku mjibu rufaa akitetewa na Wakili msomi Mathias Nkingwa.

Mali iliyokuwa ikigombaniwa ni nyumba iliyojengwa kwa jitihada za pamoja za marehemu na mkewe, inayopatikana kata ya Masuguru ndani ya Wilaya ya Korogwe, ambayo mkata rufaa alijimilikisha kinyume cha sheria tangu mwaka 2017, marehemu alipofariki.

Mke marehemu (Zaituni Salimu Kasimu) alibarikiwa kupata mtoto mmoja na marehemu mume wake, ajulikanaye kwa jina la Grace Dickson (miaka 4).

Ushahidi wa pande zote mbili ulisikilizwa na Mahakama kumpa ushindi mjibu rufaa. Sambamba na ushindi huo, pia Mahakama iliamuru mkata rufaa kuhama mara moja katika nyumba hiyo ili kumpisha mke wa marehemu na mtoto wake.

Jamani, huu ni ushauri wa bure. Tuandae Wosia. Ni kwa usalama wa wategemezi wetu. Ndugu zetu ni wema kwetu tukiwa hai tu, tukishatangulia tu mbele za haki wanageuka mbogo.

I humbly submit.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom